Uwezo wa kufanikiwa kimaisha Mungu aliuweka ndani ya kila mmoja wetu na upo katika kuanzia chini.

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
424
1,044
20220504_211027.jpg

Usitake kuiga uwezo wa wengine, jenga uwezo wako kidogo kidogo. Nimeona watu wengi mno badala ya kujenga uwezo wake kidogo kidogo

Sikia....

Mzee Mengi enzi za uhai wake alikuwa na gazeti linaitwa ALASIRI. Halikuleta faida. Gazeti la Dar Leo vile vile. Jingine liliitwa THIS DAY. Ushindani wa magazeti mengine ulikuwa mkali. Wasomaji wakabadilika. Internet zikaingia nk.

Pamoja na ukongwe wake wote kwenye media industry hayakumpa faida.
Akaachana nayo.

Halafu wewe eti unataka ufundishwe biashara ambayo hutaki kupoteza hela. Kaa na hela zako tu kwa kweli.

Hivi unadhani Novida ilienda wapi. Kama Coca Cola wanakosa soko la bidhaa yao wewe je?

Lakini CocaCola wamefilisika? Mengi alifilisika? Jibu ni HAPANA.

Okay, tufanye hivi, ule ukumbi wa Sinema pale Mwenge ITV ulikufa kifo cha fasta. Competition. Century Cinemax ilileta upinzani. Wenye mradi wakajifunza.

Kuna matajiri wengi tu walipoteza sana pesa.

Mabasi ya Scandinavia yapo tena? Kuna maduka mengi tu Kariakoo yamefungwa kipindi hiki.
Ni kawaida kwenye ulimwengu wa biashara. Si uliona Landmark Hotel Ubungo ilibadilishwa ikawa hostel. Umeona jinsi ambavyo tayari amerejea na kuwa hoteli ya kisasa zaidi.

Alishajifunza. Sijui unaelewa?

Dar Village hapo Rose Garden Kijitonyama haijajengwa hadi leo. Mradi wa mabilioni uliingia mdudu miaka zaidi ya 9 sasa. Wewe unataka utakachoanza nacho kisife. Hela zako hutaki zipotee. Aisee you're not an entrepreneur. Kaa tu na hela zako.

Bora ukazinywee Pepsi baridi tu au kula nyama choma kama unataka. Umekuwa mtu wa kutaka mafanikio yasiyo na changamoto yoyote. Ndo maana unasubiri ukiambiwa aisee biashara ya Matikiti inalipa hatari huyo umo. Ukiambiwa mayai ya kware yanalipa huyo. Hutaki kutulia kwanza ujifunze

Hakuna biashara isiyolipa. Ila kuna akili zisizo za kibiashara ambazo lazima kuzibadili zijue biashara faida na hasara ni kawaida kabisa. Wanasema SOMETIMES YOU WIN AND SOMETIMES YOU LEARN.

Sasa wewe hutaki kulearn utafikaje kwenye mafanikio kibiashara?

Mi biashara tatu tofauti nilizoanza nazo zilikufa. Pesa nyingi tu nilipoteza. Lakini ilikuwa ADA hiyo. Nilijifunza nikaanza moja vizuri zaidi. Sikukasirika wala kukata tamaa maana ninajua story za watu waliofanikiwa. Hivi una habari Bakhressa kuna biashara alishafanya na akaachana nazo. Una habari Dangote kuna wakati alipoteza dola bilioni 10 in one year? ($10 billion lost in a year!)

Trump mwenyewe licha ya kuanza biashara kwa mtaji mkubwa wa $1 million (zaidi ya BILIONI mbili za Kitanzania) alikuja kufilisika kabisa. Akabaki mtupu.
NIL.
Zero.

Rock bottom.
Halafu akarudi NEGATIVE. Akawa anadaiwa kila kona.

But wapi yupo now?
Kama haupo tayari kupoteza pesa basi kazinunulie nguo mpya sikukuu zikifika uvae upost Instagram upate LIKES angalau roho yako itulie.

Sisemi LAZIMA pesa ipotee. No. Ila nasema kama hauko tayari kupoteza you are not ready for the business world.

Na hiyo ndo maana kuna matajiri wachache. Wenye moyo wa UTHUBUTU na utayari wa kupoteza katika jamii huwa ni wachache tu.

Narudia sisemi uwe careless tu. No do your research. But uwe tayari kupoteza hela licha ya research zako

Kwani wewe unaweza kufanya research zaidi kuliko Dangote?

If you're afraid to lose money NEVER INVEST.

Baki na hela zako.
 
Back
Top Bottom