Mdogo wake mke wangu anataka kunifuta machozi

Mdogo wake mke wangu anataka kunifuta machozi

''..uhusiano wetu na mdogo wake ulianza kuchukua sura mpya..''

hii sentensi braza
 
Ndugu mleta kesi katika maelezo yako ya msingi pamoja na nyongeza ya sifa za shemejiyo hakuna mahali umeainisha kwamba mtuhumiwa/mkeo anakutoa machozi wala kuwahi kukutoa machozi...

Ushahidi wa kimazingira unaonesha wazi chanjo kikubwa cha kuttetereka kwa ndoayako ni wewe mwenyewe kwa kuwa umeshindwa kututhibitishia bila kuacha shaka kwamba mkeo kaona umepoteza mvuto kwake ilihali hii ni perceiption yako binafsi!
Sasa kwa kuwa umeshindwa kuonesha ushahidi usioacha shaka ukiwa unatoa machozi, na ikathibitika kwamba ni mkeo kakutoa hayo machozi,basi hatua unayotaka kuchukua ya kutembea na shemeji yako ni kosa kisheria,na ikibainika umetembea naye adhabu yake ni moja tu...tutakata hiyo ndude!
 
Kaa na wife mjadili changamoto zenu ili kupata suluhisho.
Wewe unadhani ni kwanini my wife wako kapoteza mvuto na wewe ndani ya aka 2 tu?

mwanamke mpumbavu huvunja ndoa yake mwenyewe, fanya unaloona ni suluhisho la matatizo yako.
 
mambo mengine si ya kuomba ushauri hapa kwa magreat Thinker,
 
huna kazi wewe?mkeo amekwenda kazini wewe unafanya nini nyumbani?
 
Ndugu zangu,

Nimeoa mwaka 2009 na tumebahatika kuzaa watoto wawili.Kwa hivi sasa ndoa yangu imeyumba zaidi kwani unyumba ninapewa kwa mwezi mara mbili tena kama msaada.

Kuna dalili zote mke wangu amepoteza mvuto na mimi kwani hata nikihitaji penzi amekuwa unwilling, lakini mke wangu ana mdogo wake wa kike ambaye ni robo tatu mama mwenye nyumba kwasababu anafanya kila kitu nyumbani.

Mke wangu yeye akitoka kazini ni kusingizia amechoka basi nikuwasha Tv kuangalia tamthilia ni takribani miezi miwili sasa, uhusiano wetu na mdogo wake ulianza kuchukua sura mpya ile tabia ya kuniwekea chakula mezani imehamia kuniletea chumbani cha ajabu leo asubuhi kaja kunidekia chumbani na night dress dada yake akiwa kazini.

Moyo wangu kama binadamu umeanza kumuangukia na alichonieleza dakika ishirini zilizopita ni kwamba dada leo atalala msibani nyumba ya pili kwa hiyo atakuja kulala kwangu nimepigwa na butwaa.

NAOMBENI USHAULI NIMKEMEE PEPO AU NIFUTWE MACHOZI

Nyuzi nyingine bwana anyway hapa ni Jamvini, wewe mpaka kufikia kuoa na kujaaliwa kupata watoto naamini ni mtu mzima. Kweli unaomba ushauri au umeleta ili kukoleza "baraza"? Umetupa multiple choice (nimkemee pepo au nifutwe machozi), umeshindwa kuchagua hapo au uliishachagua unataka ulinganishe?
 
mkuu JF imeokoa ndoa yako otherwise ungeingia kwenye bonge la ambush huko falluja kitu IED mkuu.
shukuru shetani anakupenda bado!!
 
WE NI NOMA, UMKULE SHEMEJI MBONA UNAJITAFUTIA MAJANGA MKUU??
 
Acha kummendea shemeji yako ndugu yangu hebu achana na hizo fikra ni ushetani wa hali ya juu. Kaa chini uongee na mkeo mmalize tofauti zenu ndoa zina changamoto jaribu kutatua sio kuharibu zaidi
 
acha mihemuko! you might be catching a tiger by the tail.
 
we umefanya makosa mkuu, hiyo ya baadae mke kaenda msibani ni mtego. kazi ilikuwa ifanyike asubuhi hiyohiyo. baadae bora ipite tuu. ukienda na mpango wake itakula kwako
 
Kesho kumbuka mrejesho kiongozi....ila tumia condom@@kazi njema
 
we jamaa sikia, mke wako anakuzingua hivyo kwa vyovyote manii imejaa katika kiwiliwili chako na sharti iondolewe kwa utaratibu unaofaa. kama ulivyosema mwenyewe pamoja na upweke anaolazimishwa na mkeo lakini walau mdogo wake/shemeji anaziba pengo kwa baadhi ya vitu.
ni kawaida ya wasichana akikupa offer nawe ukaikataa atakuchukia, maisha yako yatazidi kuwa magumu zaidi.
hiyo ni bahati kama ilivyo bahati nyingine na hazijileti mara mbili, poza mwili Mungu atakusamehe
 
Tafakari mapungufu yako wapi kwenye ndoa yako na si kuongeza tatizo ndani ya tatizo...
 
Hii ni zaidi ya Laaaana. Jipu kama Hilo likipasuka, lazima usaha urukie kwenye nyumba za majirani.
Madhara yake ni makubwa kuliko unavyoweza fikiri.
 
Inakuwaje we hujui mkeo analala msibani ila shemejio ndo anajua. Kwanini mke wako ameshindwa kukueleza hilo? Tafakari halafu chukua hatua.
 
Back
Top Bottom