Elections 2010 Mdahalo wa wagombea urais 2010

Status
Not open for further replies.
phd ya kanisa?

Weak justification Sugu, Upepo ushahama tayari, someni alama za nyakati - miaka 5 mmepewa mmechemsha. uzuri watanzania wengi wanaelewa kwa nini CCM mnakwepa mdahalo- na hiyo ndiyo itakuwa weak point nyingine.
 
Tunahitaji kuwa na viongozi ambao ni focused, wanaoelewa matatizo ya wananchi na wenye majibu ya kile ambacho wanaweza kufanya kutatua matatizo ya kimsingi ya wananchi. Hatuhitaji viongozi wanaosubiri kusemewa na kina Hiza Tambwe

  1. Kiongozi maana yake ni kuonyesha njia na wengine wakufuate kama njia yako ni sahihi.
  2. Kiongozi anakubali kusikiliza mawazo mapya.
  3. Kiongozi anakuwa tayari kukabiliana na changamoto za kila siku, za wafuasi wake na wapinzani wake.
  4. Kiongozi anasikiliza ushauri hata wa wale wasiomkubali.
  5. Kiongozi haogopi wapinzani wake kisiasa
  6. Kiongozi anatakiwa awe muadilifu
Je Kongozi wetu ana sifa kutuongoza? Tafakari
 
Kwa nini raisi kikwete unaogopa mdahalo,be a man,unaonyesha wazi kwamba ujafanya lolote la maana ndiyo sababu unaogopa mdahalo.kama wewe ni mwanaume ingia mdahalo na dr slaa
 
CCM irudishe viwanja, majengo ya umma

Tuesday, 03 August 2010 21:00
0diggsdigg
Jana tulichapisha habari kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mbeya kimekataa ombi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutaka kuutumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kufanyia mkutano wa kumdhamini mgombea wake wa kiti cha urais, Dk Wilbrod Slaa, unaotarajiwa kufanyika leo mchana.

Habari hizo zilisema kwamba baada ya kupokea ombi hilo la Chadema, uongozi wa CCM ulijibu kwamba uwanja huo ungetumiwa kwa michezo ya Umitashumta, jambo ambalo halikuwa kweli, kwani Ofisa wa Elimu wa Mkoa huo, Juma Kaponda, alipoulizwa alisema ofisi yake imepewa maelekezo ya mashindano hayo kufanyika wakati wa likizo za wanafunzi na siyo sasa. Hivyo,alisema taarifa za kufanyika michezo hiyo ya Umitashumta au Umiseta katika uwanja huo leo hazina ukweli wowote.

Ni jambo la kusikitisha kwamba viongozi wa Chadema walihaha huku na kule wakitafuta uwanja mbadala pasipo mafanikio, kwani ni Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine pekee unaoweza kuchukua umati mkubwa wa watu kama ambao wamekuwa wakihudhuria mikutano ya kumdhamini mgombea wa kiti cha urais wa chama hicho katika mikoa kadhaa katika siku za hivi karibuni.

Baada ya viongozi wa CCM kuwakatalia Chadema wasiutumie uwanja huo uliojengwa kwa nguvu na kodi za wananchi enzi za chama kimoja cha siasa, tumeelezwa kwamba mkutano huo sasa utafanyika leo jioni katika uwanja mdogo usiokuwa na usalama wa Luanda Nzovwe.

Kwamba CCM imeweza kuwa na jeuri ya kujirithisha na kuhodhi mali zote zilizochumwa na Watanzania wote kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa siyo tu ni jambo la kusikitisha sana, bali pia ni jambo lisiloingia akilini.

Pamoja na kuendeleza nyimbo na ngonjela za "amani" na "utulivu" kwa miongo mingi sasa, CCM imo katika hatari ya kuonekana kama kinara na bingwa wa kusuka na kukumbatia mifumo kandamizi inayoziba mianya ya kuwepo haki na usawa kwa watu wote.

Kitendo cha kuwazuia wanachama wa chama cha siasa kilichosajiliwa kisheria wasitumie uwanja uliojengwa kwa jasho lao – tena wakiwa tayari kulipa ada – pengine kinaweza kutafsiriwa kama uthibitisho kwamba CCM siyo tu ilianzisha mfumo wa vyama vingi shingoupande, bali pia ingependa vyama vya upinzani viangamie ili mfumo wa chama kimoja urejeshwe. Tungetegemea, kwa mfano, uongozi wa CCM-Taifa uingilie kati suala hilo kwa kuamuru Chadema wapewe ruhusa ya kutumia uwanja huo.

Lakini kama tulivyobainisha hapo juu, CCM haiwezi kuchukua hatua hiyo kwa sababu inafurahia na kufaidika na hali hiyo ya kuhodhi mali nyingi isiyohamishika ambayo ilitokana na jasho la Watanzania wote. Hali hiyo kwa vyovyote haitoi matumaini ya kuendelea kuwepo kwa "amani" na "utulivu" katika siku za usoni kutokana na ukweli kwamba vizazi vijavyo vinaweza kuwa na ujasiri wa kudai haki hata kama kizazi kilichopo hivi sasa kitakuwa na woga wa kufanya hivyo.

Tunawashauri viongozi wa chama hicho tawala kusoma alama za nyakati na kuchukua hatua za makusudi za kuleta maridhiano endelevu kwa matlaba ya kuhakikisha kwamba amani na utulivu vinaendelea kuwepo katika nchi yetu. Chama hicho kwa moyo wa dhati kione aibu ya "udhalimu" kilioufanya wa kukwapua, kumiliki na kuhodhi majengo, ardhi na rasilimali za kutisha, huku wenye haki ya mali hizo ambao ni wananchi walio wengi wakiambulia patupu.

Njia pekee ya kuepusha shari na machafuko huko baadaye ni kwa chama hicho kurejesha mali hizo serikalini ili Watanzania wote wanufaike na matunda ya jasho lao. Tuna imani kwamba chama hicho kitarekebisha hali hiyo, kwani hakitakuwa tayari kuchafua rekodi yake nzuri kiliyojijengea kwa muda mrefu sasa
 
kwanini akwepe mdahalo?lazima tupime uwezo wa rais mtarajiwa,kama alikubali kwenda marekani kufanyiwa uchungzi wa afya yake na moja ya uchunguzi ulikuwa kupimwa akili zake,kwanini akwepe watanzania kumpima akili zake kwenye mdahalo?ni wakati wa wanaharakati,vyama vya siasa,taasisi mbalimbali za dini kushurutisha kuwepo na mdahalo kwa wagombea urais
 
Sasa Wakenya wamesema basi katiba ya mkoloni.. Ni wakati watanzania tuseme basi kwa katiba ya mkoloni na viraka kibao.

Je wajua katiba ya sasa Kenya, ''MBUNGE HATAKIWI KUWA WAZIRI!!''
 
Ufisadi wa kutisha
• Trilioni 1.7/- zatafunwa serikalini

na Edward Kinabo

amka2.gif

SERIKALI ya Awamu ya Nne imeendelea kukumbwa na jinamizi la matumizi mabaya ya fedha za umma (ufisadi), baada ya kubainika kuwa imetumia sh trilioni 1.7 kwa kipindi cha mwaka 2008/2009 bila maelezo ya kina.
Uchambuzi huo ni ule uliotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la ‘Agenda Participation 2000' juu ya ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyotolewa hivi karibuni, umethibitisha kuwepo kwa ufisadi mkubwa wa fedha za walipa kodi.
Uchambuzi wa ripoti hiyo ya CAG kwa mwaka 2008/2009, umeonyesha ufisadi wa kutisha serikalini kwa kiasi cha sh trilioni 1.7 uliofanyika ndani ya mwaka huo.
"Jumla ya fedha za serikali ambazo ama zilitumiwa vibaya au wahusika wameshindwa kutoa maelezo ya kuridhisha jinsi fedha hizo zilivyotumiwa inafikia shilingi trilioni 1.7. Kwa kweli fedha hizi ni nyingi sana…", ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya shirika hilo.
Kiasi hicho kilichofujwa ni sawa na fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya bajeti ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi na ile ya Miundombinu katika mwaka huo wa fedha.
Kiasi hicho pia ni sawa na mara mbili ya fedha zilizokuwa zimetengwa mwaka huo kwa ajili ya Wizara ya Afya ambayo ilipata sh bilioni 589 na mara nne ya kiasi kilichokuwa kimetengwa kwa ajili ya Wizara za Kilimo na Maji, ambazo zilitengewa shilingi bilioni 379 na shilingi bilioni 309 katika mwaka wa bajeti wa 2008/2009.
Kwa ujumla, ufisadi huo unahusisha makadirio ya fedha zilizotumiwa vibaya katika eneo la manunuzi yasiyo ya kawaida ya sh bilioni 12.8, masuala ambayo hayakushughulikiwa tangu kaguzi zilizopita sh bilioni 95.7 na misamaha ya kodi ya sh bilioni 752. 3.
Maeneo mengine ni udhaifu katika ulipaji wa mishahara uliofuja sh bilioni 3. 078, masuala yahusuyo malipo ya marupurupu sh milioni 395.8, ukiukwaji katika ununuzi wa magari wa sh bilioni 4. 018, pamoja na kiasi cha sh bilioni 203.2 zilizotumiwa vibaya au kupotea katika serikali za mitaa.
Katika ufisadi huo, Wizara ya Maliasili na Utalii ndiyo imetajwa kama mfano wa kusikitisha wa wizara zilizotumia vibaya fedha za umma.
Sehemu ya ufisadi uliofanyika ndani ya wizara hiyo inahusisha ubadhirifu wa sh milioni 12 zilizolipwa kama mishahara zaidi ya viwango halali vya mishahara ya wafanyakazi na sh milioni 53 zilizolipwa bila kutolewa viambatanisho vya kuhalalisha malipo hayo.
Sh milioni 445 pia zilitumika kulipa wastaafu, marehemu na wafanyakazi walioachishwa kazi, fedha ambazo walengwa hawakujitokeza kulipwa lakini hazikurudishwa hazina.
"Jambo jingine la kusikitisha ni kwamba Wizara ya Maliasili na Utalii ilishindwa kueleza yalipo mapato ya jumla ya shilingi bilioni 19.6," ilisema sehemu ya uchambuzi huo wa Agenda Participation ikirejea ripoti ya CAG.
Mbali na wizara hiyo ya Maliasili na Utalii, wizara, idara au taasisi nyingine za umma zilizopata taarifa mbaya za fedha kutoka kwa CAG ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Jeshi la Polisi na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Nayo Serikali ya Norway imeendelea kudai kurudishiwa sh bilioni 2.6 zilizotumiwa vibaya na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Hata hivyo, katika taarifa ya bajeti ya wizara hiyo ya mwaka huu wa fedha, wizara hiyo ilisema kuwa ingeilipa Serikali ya Norway fedha hizo.
"Taarifa ya CAG pia inaonyesha utendaji usioridhisha katika nyanja ya mikopo iliyokuwa ikisimamiwa na taasisi za serikali kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo miongoni mwa wanawake na vijana nchini.
"Kwa mfano jumla ya sh milioni 355 zinazodaiwa kutolewa kwa wajasiriamali wanawake na vijana hazikuonyeshwa jinsi zilivyotumika. Taarifa za fedha kutoka halmashauri 41 hazikupatikana," ilieleza taarifa hiyo.
Mashirika ya umma na mamlaka kama vile Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Shirika la Bima la Taifa (NIC), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Shirika la Taifa la Umeme (TANESCO), Mamlaka ya Bandari (TPA) na Mfuko wa Hifadhi wa Serikali za Mitaa (LAPF) ni maeneo mengine ya upotevu mkubwa wa fedha.
Kwa mfano, ilithibitishwa kuwa jumla ya sh bilioni 58 zilizokuwa zimetolewa kama mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka 2006, mpaka sasa hakuna uhakika wa kulipwa kwa fedha hizo ambazo zilitolewa dhamana na serikali.
"Kinachowasikitisha wengi ni kwanini serikali bado inashindwa kuziba mianya ya baadhi ya maofisa wake kuendelea kutafuna fedha za umma," umehitimisha muhtasari wa wachambuzi wa wanaharakati hao.
Ufisadi wa kutisha
• Trilioni 1.7/- zatafunwa serikalini

na Edward Kinabo

amka2.gif

SERIKALI ya Awamu ya Nne imeendelea kukumbwa na jinamizi la matumizi mabaya ya fedha za umma (ufisadi), baada ya kubainika kuwa imetumia sh trilioni 1.7 kwa kipindi cha mwaka 2008/2009 bila maelezo ya kina.
Uchambuzi huo ni ule uliotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la ‘Agenda Participation 2000' juu ya ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyotolewa hivi karibuni, umethibitisha kuwepo kwa ufisadi mkubwa wa fedha za walipa kodi.
Uchambuzi wa ripoti hiyo ya CAG kwa mwaka 2008/2009, umeonyesha ufisadi wa kutisha serikalini kwa kiasi cha sh trilioni 1.7 uliofanyika ndani ya mwaka huo.
"Jumla ya fedha za serikali ambazo ama zilitumiwa vibaya au wahusika wameshindwa kutoa maelezo ya kuridhisha jinsi fedha hizo zilivyotumiwa inafikia shilingi trilioni 1.7. Kwa kweli fedha hizi ni nyingi sana…", ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya shirika hilo.
Kiasi hicho kilichofujwa ni sawa na fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya bajeti ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi na ile ya Miundombinu katika mwaka huo wa fedha.
Kiasi hicho pia ni sawa na mara mbili ya fedha zilizokuwa zimetengwa mwaka huo kwa ajili ya Wizara ya Afya ambayo ilipata sh bilioni 589 na mara nne ya kiasi kilichokuwa kimetengwa kwa ajili ya Wizara za Kilimo na Maji, ambazo zilitengewa shilingi bilioni 379 na shilingi bilioni 309 katika mwaka wa bajeti wa 2008/2009.
Kwa ujumla, ufisadi huo unahusisha makadirio ya fedha zilizotumiwa vibaya katika eneo la manunuzi yasiyo ya kawaida ya sh bilioni 12.8, masuala ambayo hayakushughulikiwa tangu kaguzi zilizopita sh bilioni 95.7 na misamaha ya kodi ya sh bilioni 752. 3.
Maeneo mengine ni udhaifu katika ulipaji wa mishahara uliofuja sh bilioni 3. 078, masuala yahusuyo malipo ya marupurupu sh milioni 395.8, ukiukwaji katika ununuzi wa magari wa sh bilioni 4. 018, pamoja na kiasi cha sh bilioni 203.2 zilizotumiwa vibaya au kupotea katika serikali za mitaa.
Katika ufisadi huo, Wizara ya Maliasili na Utalii ndiyo imetajwa kama mfano wa kusikitisha wa wizara zilizotumia vibaya fedha za umma.
Sehemu ya ufisadi uliofanyika ndani ya wizara hiyo inahusisha ubadhirifu wa sh milioni 12 zilizolipwa kama mishahara zaidi ya viwango halali vya mishahara ya wafanyakazi na sh milioni 53 zilizolipwa bila kutolewa viambatanisho vya kuhalalisha malipo hayo.
Sh milioni 445 pia zilitumika kulipa wastaafu, marehemu na wafanyakazi walioachishwa kazi, fedha ambazo walengwa hawakujitokeza kulipwa lakini hazikurudishwa hazina.
"Jambo jingine la kusikitisha ni kwamba Wizara ya Maliasili na Utalii ilishindwa kueleza yalipo mapato ya jumla ya shilingi bilioni 19.6," ilisema sehemu ya uchambuzi huo wa Agenda Participation ikirejea ripoti ya CAG.
Mbali na wizara hiyo ya Maliasili na Utalii, wizara, idara au taasisi nyingine za umma zilizopata taarifa mbaya za fedha kutoka kwa CAG ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Jeshi la Polisi na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Nayo Serikali ya Norway imeendelea kudai kurudishiwa sh bilioni 2.6 zilizotumiwa vibaya na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Hata hivyo, katika taarifa ya bajeti ya wizara hiyo ya mwaka huu wa fedha, wizara hiyo ilisema kuwa ingeilipa Serikali ya Norway fedha hizo.
"Taarifa ya CAG pia inaonyesha utendaji usioridhisha katika nyanja ya mikopo iliyokuwa ikisimamiwa na taasisi za serikali kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo miongoni mwa wanawake na vijana nchini.
"Kwa mfano jumla ya sh milioni 355 zinazodaiwa kutolewa kwa wajasiriamali wanawake na vijana hazikuonyeshwa jinsi zilivyotumika. Taarifa za fedha kutoka halmashauri 41 hazikupatikana," ilieleza taarifa hiyo.
Mashirika ya umma na mamlaka kama vile Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Shirika la Bima la Taifa (NIC), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Shirika la Taifa la Umeme (TANESCO), Mamlaka ya Bandari (TPA) na Mfuko wa Hifadhi wa Serikali za Mitaa (LAPF) ni maeneo mengine ya upotevu mkubwa wa fedha. Kwa mfano, ilithibitishwa kuwa jumla ya sh bilioni 58 zilizokuwa zimetolewa kama mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka 2006, mpaka sasa hakuna uhakika wa kulipwa kwa fedha hizo ambazo zilitolewa dhamana na serikali. "Kinachowasikitisha wengi ni kwanini serikali bado inashindwa kuziba mianya ya baadhi ya maofisa wake kuendelea kutafuna fedha za umma," umehitimisha muhtasari wa wachambuzi wa wanaharakati hao.

okl lkn pia dk slaa ataulizwa simple question
nini uhusiano wake na kanisa katoliki?

MS sometimes utumie hekima kwanza hata kama Dk Slaa ana uhusiano na kanisa hawezi kuongoza nchi na wakristo peke yake kwani Tanzania ni ya waislamu na wakristo. Pia kama atatumia ukristo wake kutawala hatadumu kwani watanzania wa sasa si kama wazamani lazima atapinduliwa tu. Hivyo basi usijenge hoja zisizokuwa na substance ndani yake. Tukija kwenye EPA ni muhimu kwani ni uhujumu wa pesa za walipa kodi na wananchi. Ufisadi umeharibu maendeleo nchi. mfano ukiangalia ufisadi unaconsume 20% of the country GDP sasa unajiuliza inakuwaje? 20% ya GDP inamaana kwamba infrastructure, mitaala ya elimu na maendeleo ya wananchi yanakosekana kwasababu ya kikundi cha watu wachache wanaotafuna rasilimali ya nchi. Wanafidia hilo deni kwa kukopa halafu wanagawa rasilimali ya nchi kama pipi je watanzania tutajivunia nini cha kwetu?
 
LOL!!!!!!!!!!

Au ndio mbayuwayu mjanja kukimbiza bawa lake?

Mvua ya mawe haina pa kujificha.

"Mvua njooo, kibiriti njooo............."
 
Napenda kuwashauri wale wanaoandaa mdahalo waendelee kufanya hivyo hata kama Kikwete kakimbia. Huyo anayetudanganya eti muda hautoshi, anatumia reference gani? Mbona mwaka '95 ulitosha?

Hadi sasa wapo wagombea 7 wameshachukua fom za kugombea kule TEC, (na hapo bado Slaa), kwa hiyo naamini watakuwepo wenye moyo na walio siriaz na nchi yao watakaowapa nafasi wananchi kusikia nini watalifanyia taifa hili, sio lazima awepo Kikwete...
 
IQ ya Jakaya Kiwete ni ndogo sana! Hajui hata kwanini Tanzania ni Maskini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom