Elections 2010 Mdahalo wa wagombea urais 2010

Status
Not open for further replies.
mimi nnayo VHS yake ya hule mdahalo,ulifanywa na abantu vision,ambao bado wapo....but nnaisi chombo kama NGO yenye kusimamia siasa safi na utawala bora inaweza andaa njadala kama hule,then unatuma mialiko kwa wagombea,unatafuta udhamini kwenye Tv unaenda hewani.
 
Wazo zuri ila ni gumu kiutekelezaji.... Mie naona ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko JK kukubali kuwepo katika mdahalo huo.
 
Yapi aliyoyafanya? Tusidanganyane katika matamshi na maandishi. Kiuchumi, kijamii na hata kisiasa nchi yetu imekwisha katika miaka mitano ya uongozi wake. Alifikiri anaweza kujenga nchi kwa kutumia uzoefu na urafiki na watu wa nje na kusahau kuwa juhudi za watanzania wote zinaitajika. Maendeleo ya nchi si sawa na budget ya Harusi ambayo waweza kupata mtu mmoja mwenye nazo mkafanikisha kila kitu, hapana hiyo haitoshi kwa taifa kama letu. Umaskini umezidi, umbumbumbu umeongezeka miongoni mwa watanzania, wasomi wa vyuo vikuu wamekuwa uchwara, wanasiasa wanaporomoka na nchi inakosa viongozi wenye uwezo wa kuamasisha jamii ya watanzania kupambana na umaskini. Katika Hotuba zake nakumbuka iliyokuwa inamwonyesha kama kiongozi mwenye dhamira ni ile ya kufungua bunge baada ya hapo sijui huwa anaongea nini. Sura yake uchoka anapotuhutubia mwisho wa mwezi. Japo si rahisi kumtambua kiongozi kwa kumwangalia lakini waweza kutambua jambo na kuwa na matumaini na mtu kupitia mwonekano wake. Mtazame Obama, Cameroon, Chavez, sura zao zinatoa matumaini ya maisha kwa wananchi wao. Mdaharo jamaa hawezi maana individual ability inatakikana sana. Pima alivyowajibu TUCTA na nafasi yake kama kiongozi mwenye mamlaka. Alitumia nguvu nyingi kudeal na TUCTA chama kisichokuwa na Nguvu ya kihivyo. ambayo
mwaka huu mkuu anaweza kushiriki kwa sababu anajiamini sana na kwa kweli wananchi wengi wanamuamini kwa aliyoyafanya.

na kwa ukweli sioni sababu ya kuogopa kwa maana wapinzani tayari wameshafulia
 
Ninaoopa na atakayoyasema kwa sababu baada ya mdaharo wapambe watasema raisi alidanganywa!
 
Hivi hao wagombea wengine ambao hatuwajadili, uwezo wao wa ku-debate tunaujua na kuukubali? Mimi nafikiri zao la viongozi wetu wengi ni wale waliozoea rallies kuliko hiyo midahalo na utashangaa wnegine nao wanaweza kuingia mitini (save may be for Prof. Lipumba).
 
Mimi ninadhani mfumo wetu pengine tungeboresha tukawa na "ilani ya kitaifa ya uchaguzi" [mambo ambayo yanatakiwa kufanywa na serikali iingiayo madarakani[pamoja na vipaumbele].
Hivi sasa kila chama cha siasa kina ilani yake na hakuna ilani mbili zinazofanana.
maoni yangu ni kuwa inakuwa vigumu kumpima mgombea kwani majibu yote atakayoyatoa inabidi yaendane na ilani ya chama chake,
hivyo kufanya kazi ya kupima kuwa ngumu na kubakia kila mwanachama/mpenzi kutetea ilani ya chama chake na mgombea wake tu.

Kaka nitajie matatu tu kwa kipindi cha takribani miaka mitano ambayo kikwete ameyafanya na wewe ukayakubali kuwa sasa huyu jamaa kafanya.
Nawasilisha.
 
Sina upeo mkubwa sana na siasa za uchaguzi na masuala ya midahalo na hata ilani. Lakini nina mashaka kama kuna mahali ambako kuna ilani ya kitaifa kabisa. Ilani kimsingi ni ahadi au offer unayoitoa au kuiuza kwa wapiga kura ili wao wakuchague kwa makubaliano kwamba hayo ndiyo unayosimamia kama chama ua mgombea na ndiyo utakayoyasimamia na kuyatekelza ukipewa mandate. Ndiyo nilivyoona kwa uchaugiz wa marekani na ndiyo maana midahalo ilikuwepo kupima ni ilani ipi ina-appeal kwa wapiga kura. Hivyo hivyo ndivyo uchaguzi wa Uingereza ulivyoendeshwa. Suala linabaki pale pale, midahalo haina impact kubwa katika matokeo ya chaguzi zetu hapa africa na hasa hapa kwetu! Sababu ni zile zile, hakuna elimu ya uraia hasa kwa wengi wa wapiga kura ambao wako vijijini na hawana utashi mkubwa sana wa siasa za uchaguzi.
 
Mdahalo ungelifaa sana lakini piga ua, Mkwere hatatia timu... akitia timu ajue amekwisha lazima atachemsha na ataboa. Makamba anajua kuwa hawezi, labda mgombea awe Magufuli au Shibuda.
 
Mgombea urais wa Chadema, Dr Slaa ametoa changamoto mpya kwa JK wafanye mdahalo ili wajipime mbele ya wap[iga kura kuhusu masuala mbali mbali ya kitaifa. (Tanzania Daima ya leo).

Binafsi siamini iwapo JK atakubali kwani anafahamo fika kuwa Dr Slaa ni mtu wa makombora ya ufisadi na JK hawezi kuyamudu -- kwani katika suala la vita dhidi ya ufisadi tumeshuhudia usanii mkubwa kutoka kwa JK.

Wapambe wake hawawezi kumkubalia JK kufanya kosa hilo, ambalo litakuwa ni political suicide kwake. Na akikataa, wananchi watajnua udhaifu mkubwa na usanii alionao JK.
 
39355_10150215260105389_818790388_13815894_1875698_n.jpg
 
karibuni tulisikia kauli ya kiongozi wanchi akisema (namnukuu)… “SIHITAJI KURA ZA WAFANYAKAZI” Na hadi leo sijasikia kama amebadili kauli yake ile au kuomba radhi wafanyakazi wa Tanzania. Mimi najiuliza maswali haya;-
“Je, wafanyakazi wana haja ya kumchagua mtu aliyewakana?”
“Je; Kuna haja ya kumchagua mtu ambaye kwa kauli yake ameonesha kutokujali mchango wa wafanyakazi katika ujenzi wa taifa hili?”
mail

HUNA HAJA YA KUMCHAGUA MSALITI, TUNAYE MTU MAKINI, TUNAYE MTU MBADALA
MCHAGUE SLAA AWE RAIS 2010


Mtumie mzalendo mwingine mwenye uchungu na nchii hii ili tulikomboe taifa letu
This Message has been scanned by Symantec Antivirus, EDP-UNICTR
 
Dk. Slaa: Namtaka JK

• Ataka mdahalo wananchi wawapime

na Kulwa Karedia

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, amemtaka mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, katika mdahalo wa kitaifa kabla ya Uchaguzi Mkuu ili taifa liwapime.

Akizungumza na Tanzania Daima mjini hapa jana, Dk. Slaa alisema hatua ya kufanya mdahalo ni fursa nzuri ya kuwaeleza Watanzania kile ambacho wamekusudia kukifanya kama watapewa ridhaa ya kuongoza taifa hili.

“Niko tayari kufanya mdahalo na Rais Kikwete na wagombea wengine wa urais kwa asilimia 100. Mtakumbuka mwaka 2005 tuliandaa mdahao kama huu lakini katika hatua za mwisho Rais Kikwete alijitoa. Natarajia safari hii hawezi kufanya hivyo,” alisema Dk. Slaa.

Alisema kitendo cha Rais Kikwete kukimbia mdahalo katika hatua za mwisho, licha ya mdahalo huo kuandaliwa na taasisi ya Tanzania for Center Democracy (TCD), kulisababisha Watanzania kumchagua bila kumjua vizuri.

“Wahisani walijitolea kutoa fedha kupitia TCD, maandalizi yote yakakamilika, ratiba ilipangwa vizuri na mratibu wa mdahalo lakini siku ya mwisho tukaambiwa mgombea wa CCM kajitoa,” alisema Dk. Slaa.

Alisema baada ya kitendo hicho, waandaaji wa mdahalo huo waligoma kuendelea bila ya kuwepo mgombea wa CCM.

Alisema moja ya faida za mdahalo huo, ni kutoa nafasi kwa wagombea wote kuwaeleza Watanzania njia ya kuondoa kero zao, na kufikisha ujumbe kwenye makundi ya watu wa ngazi za chini moja kwa moja.
“Unajua siku hizi hata kule vijijini wananchi wameendelea sana , wamefunga ving’amuzi vya runinga, ambavyo vinawawezesha kupata matangazo ya televisheni kila siku. Sasa kwa njia hii ni rahisi sana kusikiliza mdahalo kama huu,” alisema Dk. Slaa.


Alisema mdahalo ni fursa ya kutoa hoja zilizopangilika na huwafikia wananchi wengi, tofauti na mikutano ya wanasiasa ambayo hutumika kuzungumza mambo mbalimbali katika mpangilio usio rasmi kama wa mdahalo.

Alisema hatua hiyo ni kipimo tosha kwa wagombea; hivyo hakuna sababu ya mgombea yeyote kukimbia, kwani siasa si uadui kama baadhi ya watu wanavyofikiria.

“Tunakuwa na mdahalo kwa sababu tunataka kujadili mustakabali wa taifa letu. Sasa kwanini watu waingiwe na woga? Nimesikia kupitia vyombo vya habari kwamba wapo wagombea zaidi ya wanne tayari wamejitokeza kuwania urais,” alisema Dk. Slaa.

Tayari taasisi ya Vox Media inaandaa mdahalo utakaowakutanisha wagombea urais wote mara kampeni zitakapoanza mwishoni mwa mwezi huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vox Media, Ansbert Ngurumo, alilithibitishia gazeti hili kuwa maandalizi yanaendelea kuhusu mdahalo huo, ambao utahusisha vyombo vyote vya habari. Alisema taarifa kamili zitatolewa kwa umma katika siku chache zijazo.

Mbali na Dk. Slaa, mgombea mwingine aliyeomba mdahalo na JK ni Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi (CUF).
Dk. Slaa na msafara wake walipowasili mjini hapa wakitoka mkoani Mbeya kwa ajili ya kuomba udhamini wa wananchi, alipokewa na maelfu ya wananchi waliomsindikiza kuanzia Uwanja wa Ndege wa Songea hadi kwenye Uwanja wa Bombambili.


Wananchi walijipanga kando kando ya barabara, huku wengine wakiimba ‘muda wa mageuzi umefika.’

Kabla ya kufika katikati ya mji, Dk. Slaa alipokewa na wafuasi wa CCM zaidi ya 20 wakiwa wamevalia sare za chama hicho huku wakipunga mikono na kuonyesha alama ya vidole viwili, ambavyo kwa kawaida hutumiwa na CHADEMA kama salamu ya chama.

Naye mwanachama mpya wa chama hicho na mwanasheria maarufu nchini, Mabere Marando, akiwahutubia wananchi wa mji wa Songea kwenye uwanja wa Bombambili mjini hapa, alimjia juu Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, akisema ni kiongozi asiyekuwa na ubavu wa kupambana naye kisiasa.
“Mimi nawaambia mwaka huu ni mwaka wa mageuzi, licha ya baadhi ya viongozi wa CCM ambao wamekuwa wakibeza, napenda kumwambia Makamba hana ubavu wa kisiasa wa kupambana na mimi, tumejiandaa kuwashughulikia, nina majalada yao jinsi walivyoiba sehemu mbalimbali.

“Nawaambia mwaka huu haitakuwa burudani kwao, watatoa machozi kwa vile tunajua wazi nani kafanya nini katika taifa hili. CHADEMA tumejipanga kikalimilifu tofauti na miaka mingine,” alisema Marando.

Baada ya mkutano huo, Dk. Slaa alikwenda Mtwara ambako alihutubia mkutano mkubwa kwenye Uwanja wa Umoja, akawataka wananchi wa mkoa huo kubadilika kwa kuchagua viongozi kutoka kambi ya upinzani.

“Wana Mtwara tangu mfumo wa vyama vingi umeingia nchini, mkoa huu hamjawahi kuchagua mbunge hata mmoja wa kambi ya upinzani…. Umefika wakati sasa wa kukaa chini na kutafakari kwa kina, chagueni wabunge kutoka upinzani,” alisema Dk. Slaa huku akishangiliwa. Leo Dk. Slaa anatarajia kuwasili katika mikoa ya Morogoro na Kilimanjaro kwa ajili ya kuendelea kuomba ridhaa ya wananchi kumdhamini ili kupata sahihi za wananchi zitakazomwesha kugombea urais.
 
Mgombea urais wa Chadema, Dr Slaa ametoa changamoto mpya kwa JK wafanye mdahalo ili wajipime mbele ya wap[iga kura kuhusu masuala mbali mbali ya kitaifa. (Tanzania Daima ya leo).

Binafsi siamini iwapo JK atakubali kwani anafahamo fika kuwa Dr Slaa ni mtu wa makombora ya ufisadi na JK hawezi kuyamudu -- kwani katika suala la vita dhidi ya ufisadi tumeshuhudia usanii mkubwa kutoka kwa JK.

Wapambe wake hawawezi kumkubalia JK kufanya kosa hilo, ambalo litakuwa ni political suicide kwake. Na akikataa, wananchi watajnua udhaifu mkubwa na usanii alionao JK.

Hii kitu wala sio ya kuombea, CCM ni serikali na wanaweza wakaweka huo mdahalo na wakapandikiza watu wao wenye Maswali ambayo JK anamajibu yake na mwisho wa siku, ikawa balaa

sasa ni kipindi kigumu na cha muhimu sana kwa CHADEMA kuwa makini kuliko hapo Mwanzo
 
Tunahitaji kujua nini ambacho hawa wagombea wamepanga kwenda kufanya na kutekeleza pindi wakienda Ikulu , maana 2005 tulishindwa .
 

JK amekacha tena mdahalo -- yule propagandist wa CCM -- Tambwe Hizza katangaza rasmi hivyo leo katika Channel 10. sababu kubwa ya kukacha mdahalo ni kwamba JK anakubalika kwa wananchi, kutokana na kura za maoni za hivi karibuni za Redet na Synovate, na kwamba ilani ya CCM imeshatolewa na tayari imesha eleza yale wananchi wayategemee.


My take: Sijaona nonsensical reasons za kukwepoa mdahalo kama hizi mbili -- hasa ile ya pili. Yaani marais wanaotoka CCM huwa hawana mchango wao binafsi kiutendaji kwa wananchi wake kwani ni lazima afuate ilani ya CCM! Yaani hata awe na mazuri kiasi gani kuwafanyia wananchi wake hawezi, iwapo hayakuonyeshwa katika ilani ya CCM!
 

JK amekacha tena mdahalo -- yule propagandist wa CCM -- Tambwe Hizza katangaza rasmi hivyo leo katika Channel 10. sababu kubwa ya kukacha mdahalo ni kwamba JK anakubalika kwa wananchi, kutokana na kura za maoni za hivi karibuni za Redet na Synovate, na kwamba ilani ya CCM imeshatolewa na tayari imesha eleza yale wananchi wayategemee.


My take: Sijaona nonsensical reasons za kukwepoa mdahalo kama hizi mbili -- hasa ile ya pili. Yaani marais wanaotoka CCM huwa hawana mchango wao binafsi kiutendaji kwa wananchi wake kwani ni lazima afuate ilani ya CCM! Yaani hata awe na mazuri kiasi gani kuwafanyia wananchi wake hawezi, iwapo hayakuonyeshwa katika ilani ya CCM!

Hana cha kuongea ndiyo maana anaingia mitini, wacha Shujaa amgalagaze hapo October 31, 2010 na waanze kuangalia wapi walikosea katika kampeni zao. Nasikia wameshaanza mikakati ya wizi wa kura. Haya yanayotokea sasa hivi katika kura za maoni majimboni yatakuwa cha mtoto ukilinganisha na wizi mkubwa wa kura utakaofanywa na CCM.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom