Nimesoma exchange ya William Malecela na Dr. Slaa kuhusu mishahara ya wabunge. Namshangaa Dr. Slaa.
Kuonyesha kutoridhishwa na suala la mishahara ya wabunge, CHADEMA sio lazima ingojee punguzo la mishahara lipitishwe rasmi bungeni. Kama CHADEMA wanataka mishahara ipunguzwe wanaweza kuanza kutuonyesha jinsi gani wabunge wanaweza kuishi kwa mishahara midogo zaidi kwa kuchukua tu sehemu ile wanaona inatosha wabunge wao, sehemu nyingine ambayo imezidi wanaweza kuiweka katika mfuko wa kusaidia maendeleo ya wananchi.
Hapo tutaona kweli wako serious. Hizi habari nyingine za kusubiri mpaka mshinde majority ndio mbadilishe sheria, hatujui kama mtashinda majority, kwa hiyo inaweza kuwa hekaya tu.
Kama CHADEMA inataka wananchi waiamini kwamba ina nia ya kupunguza gharama ikipata madaraka, na njia moja ya kufanya hivi ni kupunguza mishahara na marupurupu ya wabunge wake, inaweza kuanza hilo sasa hivi.
Action speaks louder than words. It doesn't take CCM's approval for CHADEMA to start acting on this right now by slashing a portion of their perks and donating it to a worthy cause.
This is a challenge to see how sincere CHADEMA is.