Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Naomba kujua kama chadema wanakubali kuwashirikisha cuf kuunda kambi ya upinzani?
 
Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.

Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.

Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.

Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.


Mdahalo huu umeharibiwa na rose mwakitwange kwa sababu anacrush hoja za msingi kwa manufaa anayoyajua yeye. upuuzi mtupu kwa sababu hoja anazozipinga ndizo zinazoeneza nyufa za kisiasa huku uraiani.
napata mashaka kama amedhamiria kweli kufanya mdahalo huu uondoe tofauti baina ya vyama vya upinzani na kujenga nguvu kubwa bungeni.
 
Swala la Katiba mpya CUF inalifuatilia vizuri sana na inahitajika muungano wa mashirika, wabunge koz uhitaji wa katiba mpya ni mkubwa sana
 
..moderator amekosea ktk kuzuia swali la Chadema na Ukatoliki.
 
huu mdahalo unawahusu hamad na mbowe sasa lisu kimempeleka nini huko? Au anajua mbowe hamwezi hamadi ili amsaidie? Mbona mwenzake hajaomba msaada wa duni au miraji?

we huna macho? huoni pale pembeni kuna kajamaa ka CUF? ni katika kuwapa kampani tu...
 
CUF hawatasusia uchaguzi 2015 hata kama katiba haijabadilishwa.
 
Udini upo jamani, ni suala nyeti kwa mustakabali wa taifa letu, kwa nini rose anakataa lisijadiliwe????
 
Majibu:
Katiba, HR anasema watashirikisha na taasisi nyingine za kiraia, elimu ya uraia wataiadress bado majibu hayatoshelezi haya
HR analaumu mfumo wa elimu kuwa ndi sababu kubwa ya kukosekana kwa elimu ya uraia. watalishupalia hilo bungeni.
HR anasema katiba kama znzbr iliwezakana kwa nn ishindikane bara?
Uchaguzi ujao hawatasusia,sbb ni sawa na kumwachia nguluwe shamba ale peke yake, wao hata kama kataiaba haitabadilishwa hawatagoma
Wanaunga mkono harakati za rais za kupamabana na udini, Mbowe sasa
 
Kuna muda nilimuona Mbowe akiongea na simu, ina maana alikuwa anapewa majibu na jamaa baada ya maswali kuwa magumu???? just to know what happened!!!
 
Tukishirikiana kwa Pamoja kuwaelimisha wananchi katika swala la Uraia na wananchi wataunga mkono katika swala la Katiba na kama haitabadilika wao watashiriki uchaguzi ujao kwani kususia uchaguzi ni sawa na kumuachia shamba Nguruwe.......

hapa Sijui Hamad anaifananisha CCM kama Nguruwe???????
 
hivi huyu mwendesha mdahalo ni nani ? mwandishi wa habari ? mtaalam wa mambo ya siasa ? au ni vije ?
 
Mbowe: swala la kuvunja kambi ya upinzani bungeni sio swala la kutolea kauli ya kushtukiza.
CDM ina haki ya kikanuni kuunda kambi bungeni na ni unfair kuihukumu, na swala la kushirikiana na wengine ni lazima wafanye uchambuzi wa kina
 
Back
Top Bottom