Mdada katendwa kabakia haamini kama ni yeye ...

cacico mdada kabiki amechanganyikia ila duniani kweli kuna mambo ya ajabu sana
Nikiwaza huyo mmewe wa ndoa leo anamtamkia bila kumuoa fulani najiua
Wakati unasema hayo hukumbuki watoto,mke ,na ndugu zako
Inashangaza sana

Dada yangu FirstLady1,

Ndo maana watu wazima walijitahidi kumshauri atulize ball kwa sababu wao wana uzoefu. Binadamu yeyote ana element ya ukichaa ingawa tunatofautiana sana....Na ni kiumbe ambaye ni very elusive/dynamic..Tukiwajua haya basi hatakaa mbele za watu na kuongea upu.pu kama huo aliokuwa anauongea huyo mama!

Bahati mbaya kifo hakitoi fundisho...naamini kama angeweza kumrudisha huyo mume wake walau katika robo ya maisha yao ya zamani, hakika angekuwa na adabu sana!!

Kwa sasa hana jinsi....kama unaweza kumshauri, mwambie akubali kuishi kwenye mitala huku akiombea zamu yake kama fisi anayesindikiza mlevi!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
pole yake huyo mdada....
Alikuwa hawajui wanaumeeeeee...

Ndo maana JD aliimba 'usiusemee moyo wa mwenzi wako......'
 
Mimi namuamini Eiyer poleni wenye wanaume shingo Feni! Kongosho unalooo?

Wewe Kaungahuogopi kukosa mlango wa kuponyokea kama huyo dada?

Nadhani sie binadamu tunatakiwa kujifunza kumshukuru Mungu kwa mema tuliyopewa na kuwaombea wale walionyimwa badala ya kuwaona kama vile wamekosa kwa sababu ya uzembe wao....!

Kutesa kwa zamu...siku likihamia kwetu au wao wakainuliwa, tunabaki kuhangaika bila kujua mahali pa kuficha nyuso zetu!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Sawa ila sasa huyo mwanamke alikuwa anajimwagia misifa kwa watu ili iweje?

Hata wakimsimanga kwa sasa sitamuonea huruma!! Kama angechukulia mambo yake na mume wake kivyake vyake, kwa sasa angekuwa na mambo kidogo tu ya kumshughulisha....Ila sasa inabidi aanze kuhangaika na jinsi ya kudeal na hao majirano aliokuwa anawakoga....Malipo ni hapa hapa duniani!!

Babu DC!!
Babu DC, nakubaliana na wewe, na ndio maana tunaambiwa kila jambo tufanye kwa kiasi, hata majisifu tufanye kwa kiasi..... lakini sasa hilo limeshatokea, amemsifia sana mumewe kwa mashoga na sasa mume kamgeuka, Je ajinyonge? au aendelee kubugia uchungu wa kusalitiwa? Kuna wanawake wengi wanakufa huku wakiona, na hii ni mojawapo ya sababu hizo....Mtu anamuona mumewe ni muasherati lakini kutwa kwenye maombi, eti anamuombea muasherati ili ajirudi. Ataomba wee mpaka aletewa UKIMWI, lakini yumo tu na maombi mpaka anaenda kaburini. Mtu wa namna hiyo sidhani kama atauona ufalme wa mbinguni........ Mungu aliposema, "Wanaadamu wanaangamia kwa kosa maarifa" hakukosea, mwanamke anayeangamia kwa ujinga wa namna hii si kukosa maarifa huko............!
 
cacico mdada kabiki amechanganyikia ila duniani kweli kuna mambo ya ajabu sana
Nikiwaza huyo mmewe wa ndoa leo anamtamkia bila kumuoa fulani najiua
Wakati unasema hayo hukumbuki watoto,mke ,na ndugu zako
Inashangaza sana
sweetheart FL1 yaani cku hizi bila sala na hizi ndoa, zinazidi kuwa mitihani, yaani watu wanapuliza usiku na mchana! ndio hivyoooooooo unakuta mume anabebwa mzima bila woga!
 
Babu DC sijui kwanini namuamini Eiyer, acheni nimiamini akinitenda si nitakuja mtanicouncil!

Halafu si huwa mnatushauri tuwaamini wapenzi wetu without reservation, sasa nikiwa na reservation maisha nitauafurahiaje?

Pamoja na hayo, nakubaliana nawe kuhusu kujisifia, nimefanya hivyo kwa Kongosho tu maana ameninyanyasa sana huko nilipokuwa nashare naye!
LOL
 
Last edited by a moderator:
Huyu mdada ni jirani yangu..

Alikuwa na ka mtindo fulani kila siku anamsifia husband wake ooh ndoa yangu ni imara na ni kama paradise ndogo
Mme wangu hawezi kurudi saa mbili usiku kama waume zenu wanavyofanya nashangaa mie.!
Akitoka kazini moja kwa moja home
Nawahurumia nyie waume zenu kurudi home saa tano..sita ,akiwahi sana saa nne mnawezaje haya maisha ..?
Sifa nyingi zilimiminika kwa huyu dear husband
..Mama mmoja wa makamo alikuwa mara nyingi akimwambia temea mate chini mdogo wangu,
Haya mambo omba mungu aendelee kumtunza mmeo
LOL sasa limezuka la kuzuka
Ghafla mme kaanza kurudi saa mbili eti ooh nilikuwa na washikaji
Ikaenda saa sita kulikuwa na vikao vya dharula kazini nisamehe my wife
Ikafikia sasa anarudi asubuhi ooh nilikuwa night shift siku hizi nimekuwa potential sana kazini wife
Ghafla picha ya mrembo mmoja kwenye screen ya simu..oops
Simu inakumbatiwa wakati zamani ilikuwa inakaa popote pale
Mara trip za hapa na pale zikaendelea

Vunja kazi mzee kamtakia wife Mie bila kumuoa huyo dada wa kwenye screen ya simu nitajiua ..makubwa ……
***Based on true story ****
Jamani tuendelee kuwaweka kwenue maombi wenza wetu
Tuziombeee ndoa na familia zetu
Amani itawale daima

Nawakilisha

FL1- Mama Mwenye Nyumba

Wahenga husema "usitukane wakunga uzazi ungalipo ma usimcheke mamba kabla hujavuka mto" Mtambuzi asante kwa kutukumbusha
 
Last edited by a moderator:
Ukiona fahali moja limejitenga na mafahali wengine si kitu cha kushangilia.
Hata ukiona simba dume moja limeasi kundini 'Be eyes' hiyo huwa ni 'misfit'
Na haya ndo ukikutana nayo lazima likuue haijalishi lina njaa au limeshiba

Lile fahali bana, haliogopi mafahali wenzie, sasa hilo lako linalokaa jikoni, watch Part 2 of the story.

Mimi namuamini Eiyer poleni wenye wanaume shingo Feni! Kongosho unalooo?
 
Babu DC, nakubaliana na wewe, na ndio maana tunaambiwa kila jambo tufanye kwa kiasi, hata majisifu tufanye kwa kiasi..... lakini sasa hilo limeshatokea, amemsifia sana mumewe kwa mashoga na sasa mume kamgeuka, Je ajinyonge? au aendelee kubugia uchungu wa kusalitiwa? Kuna wanawake wengi wanakufa huku wakiona, na hii ni mojawapo ya sababu hizo....Mtu anamuona mumewe ni muasherati lakini kutwa kwenye maombi, eti anamuombea muasherati ili ajirudi. Ataomba wee mpaka aletewa UKIMWI, lakini yumo tu na maombi mpaka anaenda kaburini. Mtu wa namna hiyo sidhani kama atauona ufalme wa mbinguni........ Mungu aliposema, "Wanaadamu wanaangamia kwa kosa maarifa" hakukosea, mwanamke anayeangamia kwa ujinga wa namna hii si kukosa maarifa huko............!

Nakubaliana na wewe ndugu yangu Mtambuzi.

Sisi sote ni binadamu tulioumbwa kwa nyama na siyo stainless steel...Kwa hiyo akili ya kawaida lazima kwanza itupeleke kwenye kushusha hasira zetu. Kwa hiyo ni lazima tutampa vidonge vyake...live au mafichoni!!

Baada ya hapo, tunarudi kwenye busara kama hizo unazopendekeza weye...

Huyo mwanamke anaweza kuamua kuishi mitala au kutimua...Inabidi sasa awe mbayu wayu!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Babu DC sijui kwanini namuamini Eiyer, acheni nimiamini akinitenda si nitakuja mtanicouncil!

Halafu si huwa mnatushauri tuwaamini wapenzi wetu without reservation, sasa nikiwa na reservation maisha nitauafurahiaje?

Pamoja na hayo, nakubaliana nawe kuhusu kujisifia, nimefanya hivyo kwa Kongosho tu maana ameninyanyasa sana huko nilipokuwa nashare naye!
LOL

Ni sawa Kaunga ila mpaka muwatangazie majirani au kutoa press release/press advert eti mnawaamini waume zenu?

Hilo ndilo linalonikera mie,

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Wahenga husema "usitukane wakunga uzazi ungalipo ma usimcheke mamba kabla hujavuka mto" Mtambuzi asante kwa kutukumbusha

Umeona na wewe charminglady!!,

Watu wengi wana tabia ya kujisahau kama Riziwani ambaye hata hakumbuki kuwa baba yake atakuwa Magogoni hadi 2015 na siyo zaidi!

Wangeyakumbuka hayo, naamini wangekuwa na staha mbele za walimwengu!!

I wish huyo dada angepewa second chance!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom