Mdada katendwa kabakia haamini kama ni yeye ... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdada katendwa kabakia haamini kama ni yeye ...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by FirstLady1, Jun 6, 2012.

 1. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Huyu mdada ni jirani yangu..

  Alikuwa na ka mtindo fulani kila siku anamsifia husband wake ooh ndoa yangu ni imara na ni kama paradise ndogo
  Mme wangu hawezi kurudi saa mbili usiku kama waume zenu wanavyofanya nashangaa mie.!
  Akitoka kazini moja kwa moja home
  Nawahurumia nyie waume zenu kurudi home saa tano..sita ,akiwahi sana saa nne mnawezaje haya maisha ..?
  Sifa nyingi zilimiminika kwa huyu dear husband
  ..Mama mmoja wa makamo alikuwa mara nyingi akimwambia temea mate chini mdogo wangu,
  Haya mambo omba mungu aendelee kumtunza mmeo
  LOL sasa limezuka la kuzuka
  Ghafla mme kaanza kurudi saa mbili eti ooh nilikuwa na washikaji
  Ikaenda saa sita kulikuwa na vikao vya dharula kazini nisamehe my wife
  Ikafikia sasa anarudi asubuhi ooh nilikuwa night shift siku hizi nimekuwa potential sana kazini wife
  Ghafla picha ya mrembo mmoja kwenye screen ya simu..oops
  Simu inakumbatiwa wakati zamani ilikuwa inakaa popote pale
  Mara trip za hapa na pale zikaendelea

  Vunja kazi mzee kamtakia wife Mie bila kumuoa huyo dada wa kwenye screen ya simu nitajiua ..makubwa ……
  ***Based on true story ****
  Jamani tuendelee kuwaweka kwenue maombi wenza wetu
  Tuziombeee ndoa na familia zetu
  Amani itawale daima

  Nawakilisha

  FL1- Mama Mwenye Nyumba
   
 2. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  FL1, pole yake! ila pia fundisho, ni kama uwe na mtoto wa kike ndani, halafu we kutwa kunanga majirani wenye watoto wa kike vicheche, wallah huwa yanarudi hapa hapa duniani, vyako vinakuwa si vicheche tena, bali nungunungu!
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  Duh...kwa hiyo solution ni nini?
  Wapeni waume zenu mapenzi msiwabanie ila mkiombwa mchezo mmbaya kataeni kwani mtaharibiwa tu na kukimbiwa
   
 4. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  duuu.. m simwamini wangu hata siku moja...hahahaa pole yake huyo mtu...wanaume bana hta kama cheating ni nature inabidi tuibue na sisi cheating ni ATIFISHO mambo gan haya.
   
 5. marrykate

  marrykate JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  mi ndo maana sipendi kusemea nafsi ya mtu,
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  "...Enyi akina mama waheshimuni waume zenu..."
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Duh, Eiyer atabisha
  Lazima aseme mke aombe talaka.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. condorezaraisi

  condorezaraisi JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  makubwa haya mambo ya kusifia sifia ovyo ni vyema kukaa kimya na kumshukuru mungu kwa yote
  Hii ndoa yangu ni paradise ndogo hii naona sasa inamtokea puani
  Apige goti chini na kuomba mungu
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nilishawahi kusema hapa wakati fulani kwamba wanawake wengi wanaumia kwenye ndoa kwa sababu ya kuwasifu waume zao kwa mashoga kupita kiasi, si vibaya kumsifia mumeo kwa mashoga lakini pale yanapotokea mabadiliko kama haya usione aibu kusema umeshindwa na kuangalia mustakabali wako upya, kila mtu ameoa au kuolewa kwa utashi wake na hamna sababu ya mahusiano yenu au ndoa yenu kushikiliwa na majirani, marafiki au ndugu, kama yamekushinda bwaga manyanga anza maisha mapya, mambo ya kuanza kuwaza eti,...... "hivi majirani, ndugu au marafiki watanionaje?" yamepitwa na wakati, ndoa ni yako na sio ya kwao, anayeumia ni wewe na wala sio wao, na kama wakikuzodoa kwa kukusimanga wakikwambia ........ "kiko wapi ulichokuwa ukiringia...." Wao haiwahusu kwani wao wana maisha yao na wewe una maisha yako, kama alikuwa na tabia nzuri ni wakati ule,.......... Sasa kama amebadilika na kuwa na tabia za kiasherati wewe ufanye nini.......? Mtu hukuzaliwa naye tumbo moja, amelelewa kwao na wewe umelelewa kwenu, mmekutana ukubwani, kisa cha kutoana roho kwa sononi na msongo wa mawazo ni nini....!?
  Kila mtu anaweza kuchukua ustaarabu wake kwani huo sio mwisho wa maisha.... na maisha ni popote, hata kama ukisemwa au kusengenywa na mashoga thamani yako iko pale pale wala haiondoki, ni wewe tu unayeweza kuiondoa kwa kujishusha na kujiona dhalili mbele ya binadamu wenzio..............
   
 10. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  wanaume kitu gani bwana...upuuuzi mtupu..
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  FL1,

  Mpe pole sana huyo dada. Bahati mbaya ni too late ila huu wimbo unamfaa sana!!  Babu DC!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  umenikuna haswa! umeongea ki.com haswaaaaaaaa! kudos babu mtambuzi!
   
 13. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  wanawake ndo kila kitu....
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  cacico mdada kabiki amechanganyikia ila duniani kweli kuna mambo ya ajabu sana
  Nikiwaza huyo mmewe wa ndoa leo anamtamkia bila kumuoa fulani najiua
  Wakati unasema hayo hukumbuki watoto,mke ,na ndugu zako
  Inashangaza sana
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sawa ila sasa huyo mwanamke alikuwa anajimwagia misifa kwa watu ili iweje?

  Hata wakimsimanga kwa sasa sitamuonea huruma!! Kama angechukulia mambo yake na mume wake kivyake vyake, kwa sasa angekuwa na mambo kidogo tu ya kumshughulisha....Ila sasa inabidi aanze kuhangaika na jinsi ya kudeal na hao majirano aliokuwa anawakoga....Malipo ni hapa hapa duniani!!

  Babu DC!!
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Saint Ivuga kwani tunawanyima nini wakiomba ?ila wakishaonja huko nje ndo matatizo yanaanza ..
  Kuna kaka mmoja huwa anasema jamani mie nikioa mke wangu ruksa kuniwekea Libwata maana haka ka tabia niliko nako sijui kama nitakaacha....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Vaislay huyu baba ukimuona na vituko vyake ni vitu viwili tofauti kweli maisha hayatabiriki...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  watu wengi wanaosifiwa kupita kiasi huwa wana jambo zito wanalolificha.. nampa pole huyo dada
   
 19. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wewe.... Tema mate chini..
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi umeongea maneno mazuri na yenye hekima sana ikiwa na maana inatupasa tujitambue na tujue tunahitaji furaha maishani mwetu,,umenigusa moyoni barikiwa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...