Msandawe Halisi
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 647
- 351
Wana wa JF, nimetatazika wandugu. Nina jirani yangu yeye mwalimu jinsia yake ya kike. Amejaribu sana kuwa karibu na mimi, nami niligundua dalili zote lakini nilikuwa nampotezea.
Sasa leo ndio leo mahasibu yamenipata. Mwalimu kaingia kwangu mchana wa leo tukawa tunapiga stori za hapa na pale. Punde akanieleza kuwa moyo wake umenichagua mimi ananipenda sana, ameniomba tuwe wapenzi. Akaendelea zaidi kuniambia kwamba nisinifikirie kama yeye ni malaya au nini kwa kunitamkia ukweli wa moyo wake. kwani wanawake huwa ni vigumu kusema ukweli wa ndani ya moyo wake, ameniambia amejitaidi sana kunionyesha japo nigundue hisia zake lakini mimi sijagundua. Ameshidwa na uvumilivu
Mwalimu kisha akaniuliza nina mpenzi. Nami nikamwambia ukweli nina mchumba ambaye tayari nimeshamtolea mahari nyumbani kwetu Kurio Kwamtoro Kondoa.
Lahaulaa!! Mwalimu akaanza kulia, nikachanganyikiwa. Nimejaribu kumsihi na kumbembeleza wapi.
Imenibidi nimuache kwangu, nimemwambia akijisikia vizuri aende kwake. Sasa hivi nipo Bar natafakari, nikaona siyo vibaya kuwashirikisha wana MMU.
je huyu mwalimu nimfanyaje?