Mchungaji wa Vurugu za kidini Mto wa Mbu Amefariki

mlisema hivyo hivyo kuwa dr balele amefariki lakini kesho yake tunaambiwa he is alive and kickin'..hebu tusubiri taarifa ya habari ya usiku

Huyo mchungaji amefariki. Msiba uko Kiboroloni,Moshi kwa mtu anaitwa baba Dan. Mtu yeyote aliyepo Moshi akifika hapo kituo cha Taxi Kiboroloni akiulizia kwa baba Dan atapelekwa.

Mazishi yatafanyika baada ya mwili kufanyiwa uchunguzi na daktari wa polisi. Kama siyo uchunguzi wa mwili,ndugu wa marehemu walikua wamepanga kwenda kuzika kijijini kwa marehemu huko Njoro,Same.
 
Mungu ailaze Roho yake Peponi....Amina
Mungu aiguse mioyo ya wote waliofanya hili jambo ili watubu...AMina
Mungu arudishe upendo yumkini uliotoweka mjini mto wa mbu...Amina
Mungu aondoe kila namna ya udini unaoleta mifarakano ....Amina
Mungu afunike anga la mto wa mbu amani irudi kama mwanzo...Amina
Mungu awafundishe wote waliofanya jambo hilo kweli yake...Amina
Mungu awafundishe wote wanaoleta machafuko ya kidini...Amina

Na alaaniwe atakayekasirika baada ya kusoma maneno haya

Ndugu Mageuzi, kama wewe ni mkristo basi yakupasa kubariki na wala si kulaani! Ubarikiwe.
 
Nadhani ni vema tukafahamu pia nini kilitokea kikasababisha vurugu kabla ya kulaumu waislamu ili tuweze kujipanga vema ili siku za baaadae balaa kama hili likatokea. Kama magazeti yaliripoti ukweli walisema kuwa hawa jamaa waliitukana koran....kama ni kweli hapa pala la kujifunza. Kwanza siwaungi mkono wahubiri ambao wakiwa majukwaani badala ya kumtangaza "BWANA WETU YESU KRISTO' wa hushupalia kusimanga imani za watu wengine ikiwemo uislamu.....jamani ni kweli ndio agizo alilotuachia BWANA YESU KRISTO...INJILI NI NINI? NI KUSHAMBULIA DINI ZA WENGINE??? kwa maoni yangi si kweli...tusiache misingi ya imani.....kwa kufanya hayo hatuwasaidii tunaowahubiria bali tunatupa watu mbali zaidi....ni approach ya kishamba na isiyo na tija kutangaza HABARI NJEMA KWA KUTUKANA WENGINE
PILI.....kwa kusema haya simaanishi kuwa walistahili kufanyiwa furugu no lakini walijiweka katika hatari ya mashambulizi yasiyo ya lazima
TATU....Je ndugu zangu waislam kweli hakukuwa na njia mbadala ya kufanya baada ya hili tukio zaidi ya kufanyavurugu.....mna maan kuwa popote tukisikia mihadhara inayo tukana imani ya kikristo nasi tuchukue mapanga? patakalika kweli..
mix with yours

Naomba ninukuu neno hili la Mungu wetu
'....Ili niwaonye kwamba MUISHINDANIE IMANI Walio kabidhiwa watakatifu mara moja Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walio andikiwa tangu zamani hukumu hii, MAKAFIRI, Wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na bwana wetu Yesu Kristo. Yd1;3-4.

Hivyo basi tutaihubiri Injili kwa wakati unaofaa na wakati Usiofaa.
Maana Kuishi ni Kristo kufa ni faida.
AMINA.
 
Tatizo ni Uislam kujipa haki zote hapa duniani na kujiweka juu ya imani zingine zote. Uislam unaamini quran ndicho kitabu pekee sahihi, Imani zote ni za kikafiri isipokuwa Uislam, Mungu anawaadhibu watu wote wasio waislam hapa duniani kwa kutumia mikono ya waislam na mwislam akiua kafiri (mtu asiyeamini uislam) hana hatia na akifa wakati wa shambulio anaenda peponi moja kwa moja. Kwa mtazamo huo hakuna namna yoyote unayoweza kumsaidia mwislam anayefuata mafundisho ya dini yake.

Hii ni dini iliyozaliwa na kuenezwa kwa vita na hadi leo ipo kwenye vita isiyoisha dhidi ya dini zingine na itaendelea kufanya hivyo hadi siku ya kiama. Ili kukidhi haja zao za kuua na kudhalilisha dini zingine wanajitafutia visababu vya uongo na ukweli, utasikia eti wamekashifu uislam, wamemtukana mtume, wameidharau quran nk nk. Kinyume chake wao wanafanya watakavyo juu ya imani zingine na hakuna wa kuwakemea.

Cha msingi hapa ni wewe pamoja na familia yako kujilinda kiimani dhidi ya hizi nguvu za giza. Kesheni na kuomba ili msitiwe majaribuni!
Mkuu.
Kwa mchango wako huu hapa wewe huna tofauti na hao wachungaji na waislamu wa tukio la Mto wa mbu.

Unataka tuamini kuwa wewe binafsi huna marafiki waislamu, au ndugu zako, jirani zako ambao ni waislamu? Unaishi wapi wewe?
Kama unaishi Tanzania basi ni lazima unaishi kwa kujitenga.

Kama unaishi mtaani basi unawajuwa waislamu na nina uhakika hawajakuadhibu bila sababu. Unasaidiana nao kila siku. Kwa ulivyoieleza dini yao katika mchango wako basi unawakana rafiki zako, jirani zako na pengine ndugu katika familia yako.

Suala la dini mbili kuu Tz ni kitu ambacho kinachukua mkondo ambao kama wewe, mimi na kila mmoja wetu hatutachukua juhudi za makusudi kujizuia kuchochea hisia hizi za kidini nchi yetu itajikuta inaingia pabaya.

Vita si kitu kizuri lakini vita vya kidini ni vibaya zaidi. Sote tuna wajibu wa kuzuia kuitumbukiza nchi yetu katika vita hivyo. Kauli zetu zitolewe kwa tahadhari. Fikiria vita vya kidini Tanzania vitamuacha nani? Nani atasalimika?

Tuchunge ndimi zetu. Na tusemezane,tuambiane sote wakristo na waislamu kuwa kuheshimu dini za wengine ni wajibu wa kila mmoja wetu. Tukishindwa kufanya jambo hili basi na sisi tutakuwa ni sehemu ya watu wanaoridhia kuona udini unatumika kutugawa.
 
Ooops so sad, RIP

Jamani tuanze kushika linalotuhusu, lisilotuhusu tuachane nalo.

Muislamu jisomee Biblia kwa matumizi yako binafsi, siyo kutafuta mapungufu.
Halikadhalika Mkristo jisomee Kuran kwa matumizi yako binafsi, siyo kutafuta huko mapungufu.

Kubwa zaidi chonde chonde viongozi wa dini, kuweni makini na kauli zenu zozote mnazotoa kwa waumini wenu.

Sehemu kubwa ya Jamii ina tabia ya kuamini kila kinachosemwa na viongozi wa dini zao ni sahihi.
 
Ww km hujui nn uislam shut ur mouth up ktk ulimwengu huu wakristo ndo wachokozi na uislam unakataza kuua au kujiua au huoni mulimchora mtume ktk ukatuni je mlitaka 2nyamaze nyinyi ktk nchi zenu munapitisha sheria munazotaka husikii SAUDIA,OMAN wala COMMORO kusema chochote lkn waislam wakitekeleza sheria za dini utasikia obama au cameron kasema hapa la msingi ni kudhibiti na kujichunga na mambo ya uchochezi

hii ndo sampuli ya muislam, ebu angalia lugha yake...ni ya ushari hasa!
 
Its painful and am real sad, whoever caused the death will pay in body and spirit. Amen
 
Mkuu kichwa cha habari hakiheshimu wachungaji. Hakuna mchungaji wa vurugu za kidini.
 
hii ni hatari sana kwenye nchi yetu, inaonekana ni jinsi gani serikali imeshindwa kulinda raia wake
 
Mmoja wa wachungaji waliopigwa mto wa mbu katika vurugu za kidini amefariki leo...
Source..nipo mto wa mbu
 
Wauwaji wanafahamika. Serikali ionyeshe kuwa haijaingizwa kwenye Ushabiki wa Kidini kwa Kuwachukulia hatua.

Hilo tu.
 
Back
Top Bottom