Mchungaji mwingine amuasi Kakobe

Mr.Toyo

JF-Expert Member
Feb 9, 2007
433
117
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe amezidi kubanwa na wachungaji wake, baada ya mchungaji mwingine kumuasi na kuiomba Mahakama Kuu aunganishwe kuwa mlalamikaji katika kesi inayomkabili askofu huyo.Kakobe anakabiliwa na kesi ya ubadhirifu wa pesa za kanisa hilo zaidi ya Sh14 bilioni pamoja na ukiukwaji wa katiba inayoliongoza kanisa.

Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu Dar es Salaam Juni 21, mwaka huu na na Dezedelius Patrick, Angelo Mutasingwa na Benedict Kaduma wanaodai kuwa ni wachungaji wa kanisa hilo maeneo tofauti nchini. Hata hivyo Kakobe anawapinga walalamikaji hao kuwa hawana haki ya kisheria kumshtaki kwa kuwa si wachungaji wa kanisa hilo akidai kuwa walishafukuzwa na hivyo hawana haki ya kuhoji jambo lolote kuhusiana na kanisa hilo.

Lakini wakati Kakobe akiwapinga walalamikaji hao wa awali, msimamizi wa kanisa hilo wilayani Liwale mkoani Lindi, Mchungaji Ignas Innocent ameibuka na kuiomba mahakama hiyo aungane na walalamikaji hao. Katika hati yake ya maombi aliyoiwasilisha mahakamani hapo Septemba 5, mwaka huu, Mchungaji Innocent anadai kuwa ameamua kujiunga katika kesi hiyo katika upande wa walalamikaji kwa kuwa kuna ukweli ambao anataka kuufunua.

Kwa mujibu wa hati hiyo ya maombi aliyoiambatanisha na hati ya kiapo chake yake Mchungaji Innocent anadai kuwa aliteuliwa kushika wadhifa huo Machi 1996, nafasi ambayo anaishikilia hadi sasa. Anadai kuwa katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku aliweza kugundua dosari mbalimbali kulinganisha na mpango ambao ulifanywa na msimamizi wake wakati alipoteuliwa kushika wadhifa huo.

Mchungaji Innocent anabainisha kuwa imemwia vigumu kutekeleza baadhi ya majukumu yake kutokana na sababu kwamba hakuna utekelezaji wa masharti ya Katiba ya Bodi ya Wadhamini, ambayo anaifanyia kazi. Masharti hayo ya katiba ambayo hayatekelezwi alidai kuwa ni pamoja kutokuwapo kwa mkutano mkuu, malipo ya mishahara na dosari nyinginezo nyingi ambazo zimesababisha ukiukwaji wa haki zake.

Hivyo anasema ameona ni muhimu kuungana na wenzake katika kesi hiyo ili kupigania haki zao zinazotolewa na katiba ya kanisa hilo. Hata hivyo Mchungaji Innocent anadai kuwa ameshuhudia msimamizi wake (mlalamikiwa, Kakobe) akitangaza kuwa uchaguzi mkuu umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka mitano wakati umefanyika mara moja tu tena baada ya kesi hiyo kufunguliwa.

Anasisitiza kuwa ameona ni muhimu sana kuungana na wenzake katika kesi hiyo kwa kuwa malalamiko hayo yanatokana na mtu au bodi au mamlaka moja ambayo ni mlalamikiwa na kwamba ana sababu za msingi kiukweli na kisheria kufanya. Katika kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2011 iliyofunguliwa na wachungaji hao Juni 21, wameorodhesha tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya pesa za kanisa hilo dhidi ya Kakobe na kwamba amekuwa akikiuka Katiba ya kanisa hilo.

Hivyo wanaiomba Mahakama imlazimishe arejeshe Sh2 bilioni zinazodaiwa kutumika kwa ujenzi wa makazi ya kiaskofu, Sh325 milioni zilizotumika kwenye kampeni za kisiasa na Sh960 milioni zilizochangishwa kwa lengo la matangazo. Pia wanahoji matumizi ya Sh10 bilioni zinazodaiwa kutumika kwa ujenzi wa eneo la kanisa na kwamba amekuwa hatoi taarifa ya michango anayoikusanya kwa waumini na mauzo ya CD, DVD na VCH za kanisa hilo.

Madai mengine ni Sh800 milioni alizokusanya kwa waumini ili kuanzishia kituo cha televisheni lakini sasa anawaambia kuwa mpango huo umeshindikana kwa kuwa kitaathiriwa na umeme wenye msongo mkubwa uliopitishwa eneo hilo.

SOURCE: Mchungaji mwingine amuasi Kakobe,

AMAZING!

OMEGA

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
693
300
Kakobe ana mipesa yote wakati wazazi wake pale Kakonko wanaishi nyumba ya tembe na maisha ya kubangaiza,hivi hela zote zinamsaidia nini?walahi ukiona nduguze kakobe na wazazi wake machozi yatakutoka,baba yake ni mwalimu mstaafu na mimi alinifundisha kule Muhange lakini kwa sasa anaishi kwa ka pensheni bila msaada wowote toka kwa mwanaye huyo billionea.

Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,006
598
Tuache sheria ichukue mkondo wake katika kesi hii dhidi ya Kakobe. Hakuna haja ya siasa "behind the curtain". Taarifa za hakika kutoka Mahakama Kuu, zinaeleza kwamba, tarehe hiyohiyo ya 5.9.11, kabla ya kuletwa kwa "application" hiyo ya mtu huyu anayeitwa Ignas Innocent; Jaji anayehusika na kesi hiyo, Augustine Shangwa, alikwisha kutoa "order" kwamba pingamizi la awali la kesi hii (Preliminary Objection), lianze kusikilizwa kwa maandishi (Written Submission).

Jaji alimwagiza Kakobe kuleta maelezo yake kwa maandishi, kuhusu pingamizi alilolitoa; kufikia majuzi tarehe 12.9.11. Walalamikaji, watatakiwa kujibu maelezo hayo kwa maandishi kufikia tarehe 12.10.11; na Kakobe tena atatakiwa kuleta "rejoinder", au kujibu hoja zilizoko katika majibu ya walalamikaji, kufikia tarehe 17.10.11. Baada ya hayo yote, kesi hiyo itatajwa mbele ya Jaji huyo, tarehe 21.10.11; na huenda siku hiyo Jaji akapanga tarehe ya kutoa hukumu kuhusu pingamizi hilo la awali.

Kama ni hivyo basi, tuwe na subira; bila shaka , wiki chache zijazo, pumba na mchele vitajulikana.

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
2,176
1,588
Yuda alimsaliti Bwana Yesu, sishangai mchungaji kumsaliti Kakobe.
Wanafiki hawakwepeki, rafiki mmoja unazungukwa na wanafikiki 27

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
42,494
92,865
Wajameni, kitu ninachojua kumhusu Askofu Mkuu Zakaria Kakobe, ni mtu mwenye real powers. Kanisa ni lake personal property na hiyo katiba aliitengeneza tuu ili kukidhi matakwa ya usajili, hao wachungaji wanalijua hilo na wanazijua nguvu za Kakobe sijui kwa nini wanataka kuitest his patience!.

Amini nawaambieni kesi hii haifiki popote! na akifika, subirini kitakachowafika kuanzia jaji mpaka washitaki!.

YanguHaki

Senior Member
Oct 11, 2010
129
9

Cognitivist

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
1,058
2,090

Mmmmh!

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
222

Kaka acha kutisha watu wewe hamna mtoto humu ondoa upupu wako.

moblaze

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
231
27
Yuda alimsaliti Bwana Yesu, sishangai mchungaji kumsaliti Kakobe.

Wanafiki hawakwepeki, rafiki mmoja unazungukwa na wanafikiki 27

acha kuelemea upande mmoja bila kujua. thread inajieleza bwana

moblaze

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
231
27
Wajameni, kitu ninachojua kumhusu Askofu Mkuu Zakaria Kakobe, ni mtu mwenye real powers. Kanisa ni lake personal property na hiyo katiba aliitengeneza tuu ili kukidhi matakwa ya usajili, hao wachungaji wanalijua hilo na wanazijua nguvu za Kakobe sijui kwa nini wanataka kuitest his patience!.

Amini nawaambieni kesi hii haifiki popote! na akifika, subirini kitakachowafika kuanzia jaji mpaka washitaki!.

<br /
unawashwa kwenye masaburi ww?

ESAM

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,152
532
Tuache sheria ichukue mkondo wake katika kesi hii dhidi ya Kakobe. Hakuna haja ya siasa "behind the curtain". Taarifa za hakika kutoka Mahakama Kuu, zinaeleza kwamba, tarehe hiyohiyo ya 5.9.11, kabla ya kuletwa kwa "application" hiyo ya mtu huyu anayeitwa Ignas Innocent; Jaji anayehusika na kesi hiyo, Augustine Shangwa, alikwisha kutoa "order" kwamba pingamizi la awali la kesi hii (Preliminary Objection), lianze kusikilizwa kwa maandishi (Written Submission).

Jaji alimwagiza Kakobe kuleta maelezo yake kwa maandishi, kuhusu pingamizi alilolitoa; kufikia majuzi tarehe 12.9.11. Walalamikaji, watatakiwa kujibu maelezo hayo kwa maandishi kufikia tarehe 12.10.11; na Kakobe tena atatakiwa kuleta "rejoinder", au kujibu hoja zilizoko katika majibu ya walalamikaji, kufikia tarehe 17.10.11. Baada ya hayo yote, kesi hiyo itatajwa mbele ya Jaji huyo, tarehe 21.10.11; na huenda siku hiyo Jaji akapanga tarehe ya kutoa hukumu kuhusu pingamizi hilo la awali.

Kama ni hivyo basi, tuwe na subira; bila shaka , wiki chache zijazo, pumba na mchele vitajulikana.

Ni kweli ndugu tuwe na subira ili ukweli ujulikane maana mahakamani ndiyo kwenyewe hasa. Mtumishi wa Mungu Kakobe songa mbele kwa nguvu zote na kuchapa Injili.

Ubarikiwe BABA KAKOBE

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom