Waliosimamishwa KKT Hai: Barua zetu za maombi ya fedha mchungaji alizichana

Jul 30, 2018
13
12
WhatsApp Image 2024-02-05 at 08.22.30_d6c59cd0.jpg
WhatsApp Image 2024-02-05 at 08.22.30_27aad361.jpg

Mwenyekiti wa Uamsho ,Mweka Hazina wa Faragha ya Hai mjini ,Clotilda Massawe na Katibu wa Uamsho Joseph Robert wamesema mgogoro ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Hai mjini ulianza muda mrefu na kwamba walikaa kimya ili ushughulikiwe ndani ya kanisa.

“Huu mgogoro haukuanza juzi baada ya sisi kupewa barua isipokuwa umekuwa ni wa muda mrefu hata kwenye kikundi cha Daikonia pia ,tulikaa kikao cha Daikonia tukakubalina kwenye utaratibu ambao tuko nao toka awali kwa namna ya ku- handle Yatima na Wajane ,” alisema Shoo.

“Tulikaa kikao tukaandika maombi ya fedha ambazo zinatakiwa kwenda kwa wahitaji lakini yeye Mchungaji alishinikiza kwamba kuna mama ana mtoto na yeye aingizwe kwenye wahitaji ,akachana ile karatasi tuliyoandika sisi kama kamati wakati wa kikao na akasema atafanya maamuzi magumu na kweli alifanya maamuzi magumu akachana ile karatasi “ aliongeza Shoo.

Alisema alienda kuandikabarua nyingine akaweka hizo fedha ambazo anataka yule mama apewe takribani kama shilingi laki tatu na nusu akasaini na kumtajka Mwenyekiti wa Daikonia pia ni Saini .

“Alinitaka na mimi ni Saini nikamwambia hapana hiki si kilichopitishwa,mwisho wa siku hilo jambo nafikiri lilifika jimboni, mkuu wa jimbo akasuluhisha hilo jambo na akatamka mbele ya kikao cha baraza kama kamati Ilisha kaa na ikapanga kiasi gani kitoke kiasi kilichoongezwa na mchungaji kiondolewe .” alisema Shoo.

Alisema hoja nyingine ilikua ni ya barua iliyoandikwa kwenda kwa mtunza Hazina kwa ajili ya kupaua nyumba maombi na kwamba licha ya kuaindika tangu Februari 23 mwaka 2023 na bado haikujibiwa hadi pale walipoamua kuifuatilia.

“Tuliamua kuuliza sababu za kutokupitishwa kwa barua yetu , mchungaji aliichana barua hiyo kwa mikono yake na kutuambia twende kokote.” alisema Ndeakomfoo Shoo Mwenyekiti wa kikundi cha faragha aliyesimamishwa.

Mtunza Hazina wa Faraghay a Hai mjini Clotilda Massawe alisema sababu ya kinachoendelea Usharika wa Hai mjini ni ripoti ya fedha iliyosomwa mwezi wa Saba na viongozi hao kuona kwamba fedha zao kiasi cha shilingi 4,349,300 hazipo kwenye ripoti hiyo.

“Nilipomuuliza Mchungaji kuhusu kutoonekana fedha hizo kwenye taarifa ,Mchungaji alijibu “Ukichimba Udongo Utakuta Udongo" kauli ambayo sikuielewa na hadi sasa fedha za Uamsho zilizopo ni 7,836,300.”alisema Massawe.

Clotilda alisema Mchungaji amekuwa na tuhuma za kuwanyanyasa akieleza kuwa kitu chochote kinachohusu kanisa hakiwezi kufanyika hata kiwe cha usafi hakitafanyika mpaka ruhusa itoke kwake na kwamba ameamua kuyaweka bayana ili Usharika ujue,na kanisa lijue juu ya unyanyasaji huu.

Mchungaji Kiongozi Dominic Mushi wa Usahrika wa Hai Mjini alipotafutwa kuzungumzia tuhuma dhidi yake alisema ufafanuzi wa tuhumza hizo mwandishi akazifuate kwa wale waliomtuhumu na kwamba hawezi zungumzia suala hilo.

“Si msemaji wa jambo hilo ….huku akiondoka ….msemaji wa jambo hilo labda huyo aliyekueleza, Mh naomba tu uondoke ,hili ni kanisa la utaratibu wake“ alisema Mchungaji Dominic Shoo akimtaka mwandisi kuondoka eneo la kanisa.

MWISHO
 
Muumini ukitaka gari unaombewa, wao wakitaka gari inafanyika harambee.

Haya makanisa yana uovu mwingi wanajifichia kwenye kivuli cha imani na ukihoji unaonekana una mapepo.
 
Back
Top Bottom