Mr.Toyo
JF-Expert Member
- Feb 9, 2007
- 433
- 117
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe amezidi kubanwa na wachungaji wake, baada ya mchungaji mwingine kumuasi na kuiomba Mahakama Kuu aunganishwe kuwa mlalamikaji katika kesi inayomkabili askofu huyo.Kakobe anakabiliwa na kesi ya ubadhirifu wa pesa za kanisa hilo zaidi ya Sh14 bilioni pamoja na ukiukwaji wa katiba inayoliongoza kanisa.
Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu Dar es Salaam Juni 21, mwaka huu na na Dezedelius Patrick, Angelo Mutasingwa na Benedict Kaduma wanaodai kuwa ni wachungaji wa kanisa hilo maeneo tofauti nchini. Hata hivyo Kakobe anawapinga walalamikaji hao kuwa hawana haki ya kisheria kumshtaki kwa kuwa si wachungaji wa kanisa hilo akidai kuwa walishafukuzwa na hivyo hawana haki ya kuhoji jambo lolote kuhusiana na kanisa hilo.
Lakini wakati Kakobe akiwapinga walalamikaji hao wa awali, msimamizi wa kanisa hilo wilayani Liwale mkoani Lindi, Mchungaji Ignas Innocent ameibuka na kuiomba mahakama hiyo aungane na walalamikaji hao. Katika hati yake ya maombi aliyoiwasilisha mahakamani hapo Septemba 5, mwaka huu, Mchungaji Innocent anadai kuwa ameamua kujiunga katika kesi hiyo katika upande wa walalamikaji kwa kuwa kuna ukweli ambao anataka kuufunua.
Kwa mujibu wa hati hiyo ya maombi aliyoiambatanisha na hati ya kiapo chake yake Mchungaji Innocent anadai kuwa aliteuliwa kushika wadhifa huo Machi 1996, nafasi ambayo anaishikilia hadi sasa. Anadai kuwa katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku aliweza kugundua dosari mbalimbali kulinganisha na mpango ambao ulifanywa na msimamizi wake wakati alipoteuliwa kushika wadhifa huo.
Mchungaji Innocent anabainisha kuwa imemwia vigumu kutekeleza baadhi ya majukumu yake kutokana na sababu kwamba hakuna utekelezaji wa masharti ya Katiba ya Bodi ya Wadhamini, ambayo anaifanyia kazi. Masharti hayo ya katiba ambayo hayatekelezwi alidai kuwa ni pamoja kutokuwapo kwa mkutano mkuu, malipo ya mishahara na dosari nyinginezo nyingi ambazo zimesababisha ukiukwaji wa haki zake.
Hivyo anasema ameona ni muhimu kuungana na wenzake katika kesi hiyo ili kupigania haki zao zinazotolewa na katiba ya kanisa hilo. Hata hivyo Mchungaji Innocent anadai kuwa ameshuhudia msimamizi wake (mlalamikiwa, Kakobe) akitangaza kuwa uchaguzi mkuu umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka mitano wakati umefanyika mara moja tu tena baada ya kesi hiyo kufunguliwa.
Anasisitiza kuwa ameona ni muhimu sana kuungana na wenzake katika kesi hiyo kwa kuwa malalamiko hayo yanatokana na mtu au bodi au mamlaka moja ambayo ni mlalamikiwa na kwamba ana sababu za msingi kiukweli na kisheria kufanya. Katika kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2011 iliyofunguliwa na wachungaji hao Juni 21, wameorodhesha tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya pesa za kanisa hilo dhidi ya Kakobe na kwamba amekuwa akikiuka Katiba ya kanisa hilo.
Hivyo wanaiomba Mahakama imlazimishe arejeshe Sh2 bilioni zinazodaiwa kutumika kwa ujenzi wa makazi ya kiaskofu, Sh325 milioni zilizotumika kwenye kampeni za kisiasa na Sh960 milioni zilizochangishwa kwa lengo la matangazo. Pia wanahoji matumizi ya Sh10 bilioni zinazodaiwa kutumika kwa ujenzi wa eneo la kanisa na kwamba amekuwa hatoi taarifa ya michango anayoikusanya kwa waumini na mauzo ya CD, DVD na VCH za kanisa hilo.
Madai mengine ni Sh800 milioni alizokusanya kwa waumini ili kuanzishia kituo cha televisheni lakini sasa anawaambia kuwa mpango huo umeshindikana kwa kuwa kitaathiriwa na umeme wenye msongo mkubwa uliopitishwa eneo hilo.
SOURCE: Mchungaji mwingine amuasi Kakobe,
AMAZING!