Mchungaji Msigwa aboronga Bungeni

Mchungaji Msigwa aboronga Bungeni

Kuna mwenye CV yake atusaidie kutuwekea hapa jamvini? Maana bunge letu lina hadi waganga wa kienyeji na darasa la saba kibao achilia mbali wenye vyeti vya kuforge.

Kwani hao 'waganga wa kienyeji' na 'darasa la saba' walizaliwa humo Bungeni !? Si walipigiwa kura wakachaguliwa na mbu mbu mbu wenzako!
 
hawa si midomo tuu kwani unadhani kuna chochote, alimradi ametoa arufu mdomoni

Ww mwenyewe umeandika tu kuvifanyisha kazi vidole vyako, huku shirukisha ubongo wako uliolala!
 
Wadau, naangalia Bunge Live kupitia TBC1. Mchungaji msigwa ameuliza swali la kutaka mkakati wa serikali kukabiliana na uharibifu wa mazingira kutokana na wananchi wengi kutumia nishati ya kuni kama chanzo cha nishati ya kupikia. Mchungaji msigwa amesema kuwa kwa takwimu alizonazo ni kuwa Watanzania wanakata wastani wa Ekari 300 kwa siku sawa na Hekta 800. Kwangu nilipata shida sana kumuelewa na nikajiuliza kama kweli Mchungaji Msigwa anajua anachokisema au kuna mtu amemkaririsha.

Nijuavyo ni kuwa Ekari 300 ni sawa na Hekta 121.407. Kwa wale wataalam wa kukokotoa wanaweza wakatusaidia. Hii ni kutokana na ukweli kuwa Hekta moja ni sawa na Ekari 2.5. Hivyo kwa Ekari 300, haiwezi kuwa Hekta 800. Hata kama anaweza kujitetea kuwa alibadili hivyomvipimo bila ya kujijua, Hekta 300 haiwezi kuwa sawa na Ekari 800 bali ni sawa na Ekari 741. Kutokana na ufafanuzi huo, nimemdharau sana mchungaji Msigwa na napata shida kubaini uelewa wake.

Natoa angalizo kwa wanasiasa kutokurupuka kutoa hoja ambazo hawajui undani wake. Ni vema mchungaji Msigwa angeuliza kwanza ili apate ufafanuzi wa hivi vipimo vya Hekta na Ekari ili kukwepa aibu hii iliyomkuta.

Nawasilisha.

Tatizo wanameza tu hata wakidanganywa!Unadhani kuna wanchojua hao kundi la mbowe!Jembe kundi la zito, Kitila,Baregu,Marando etc,huwezi kuwasikia wakitema pumba hizo!
 
Acha kuonyesha ujinga katika jambo dogo lama hilo. Ekari 800 ni sawa na hekta 323.7 hivyo katika kueleza kuna jambo la kuchanganya kaanza na kipi kati ya ekari na hekta ila msingi wa hoja yake haikuwa hivyo vipimo bali maudhui ya alichokisema. Ungejadili hilo watu wangekuona una la maana.

Mkuu, umevurugwa wewe. Msigwa kasema kuwa EKARI 300 ni sawa na HEKTA 800. Mbona unamlisha maneno wewe?
 
mwanzo nilijua walio bungeni wote niwajuzi wa mambo kumbe wengine huenda bungeni kwa upepo tu kama ulivyomkumba msigwa.
 
Wadau, naangalia Bunge Live kupitia TBC1. Mchungaji msigwa ameuliza swali la kutaka mkakati wa serikali kukabiliana na uharibifu wa mazingira kutokana na wananchi wengi kutumia nishati ya kuni kama chanzo cha nishati ya kupikia. Mchungaji msigwa amesema kuwa kwa takwimu alizonazo ni kuwa Watanzania wanakata wastani wa Ekari 300 kwa siku sawa na Hekta 800. Kwangu nilipata shida sana kumuelewa na nikajiuliza kama kweli Mchungaji Msigwa anajua anachokisema au kuna mtu amemkaririsha.

Nijuavyo ni kuwa Ekari 300 ni sawa na Hekta 121.407. Kwa wale wataalam wa kukokotoa wanaweza wakatusaidia. Hii ni kutokana na ukweli kuwa Hekta moja ni sawa na Ekari 2.5. Hivyo kwa Ekari 300, haiwezi kuwa Hekta 800. Hata kama anaweza kujitetea kuwa alibadili hivyomvipimo bila ya kujijua, Hekta 300 haiwezi kuwa sawa na Ekari 800 bali ni sawa na Ekari 741. Kutokana na ufafanuzi huo, nimemdharau sana mchungaji Msigwa na napata shida kubaini uelewa wake.

Natoa angalizo kwa wanasiasa kutokurupuka kutoa hoja ambazo hawajui undani wake. Ni vema mchungaji Msigwa angeuliza kwanza ili apate ufafanuzi wa hivi vipimo vya Hekta na Ekari ili kukwepa aibu hii iliyomkuta.

Nawasilisha.

Umejikita zaidi kwenye upinzani wa CHADEMA na kusahau hoja ya msingi "uhalibifu wa mazingira".

Hoja ya msingi ni kama serikali na mkakati wa kupambana na uharibifu wa mazingira. Ukiingilia mahesabu ukasahau hoja ya msingi si sawa
 
hii inalingana na ,mada iliyopo hewani?

Lizaboni:Ujumbe apo ni kwamba hicho alichokosea Msigwa(vipimo vya Hekta na Ekari ) kinaondoa vipi hoja ya msingi serikali kukabiliana na uharibifu wa mazingira? :A S 39:
 
My Friend, Hesabu zako ni ukubwa wa Ekari na Hekta tuu au ni eneo ukubwa wa eneo lilikatwa miti. Kwa hiyo umekubali alichosema ukiacha hoja ya ukubwa wa eneo?
 
Wakuu, hapa hoja ya msingi ni huku kuboronga kwa Mchungaji Msigwa. kutokana na data zake kutoeleweka, ni wazi kuwa hata kile alichokuwa anakusudia kukisema ni porojo tu al mradi siku iende
Nadhani hana tofauti na mkuu wenu kuudanganya ulimwengu kuwa mandela alikuja Tanzania january 1961
 
Wadau, naangalia Bunge Live kupitia TBC1. Mchungaji msigwa ameuliza swali la kutaka mkakati wa serikali kukabiliana na uharibifu wa mazingira kutokana na wananchi wengi kutumia nishati ya kuni kama chanzo cha nishati ya kupikia. Mchungaji msigwa amesema kuwa kwa takwimu alizonazo ni kuwa Watanzania wanakata wastani wa Ekari 300 kwa siku sawa na Hekta 800. Kwangu nilipata shida sana kumuelewa na nikajiuliza kama kweli Mchungaji Msigwa anajua anachokisema au kuna mtu amemkaririsha.

Nijuavyo ni kuwa Ekari 300 ni sawa na Hekta 121.407. Kwa wale wataalam wa kukokotoa wanaweza wakatusaidia. Hii ni kutokana na ukweli kuwa Hekta moja ni sawa na Ekari 2.5. Hivyo kwa Ekari 300, haiwezi kuwa Hekta 800. Hata kama anaweza kujitetea kuwa alibadili hivyomvipimo bila ya kujijua, Hekta 300 haiwezi kuwa sawa na Ekari 800 bali ni sawa na Ekari 741. Kutokana na ufafanuzi huo, nimemdharau sana mchungaji Msigwa na napata shida kubaini uelewa wake.

Natoa angalizo kwa wanasiasa kutokurupuka kutoa hoja ambazo hawajui undani wake. Ni vema mchungaji Msigwa angeuliza kwanza ili apate ufafanuzi wa hivi vipimo vya Hekta na Ekari ili kukwepa aibu hii iliyomkuta.

Nawasilisha.

Siwezi kusema sana ila ukisoma post hii utagundua kuwa huyu ni moja ya watu wanaoumizwa sana na umakini wa mtu then anakuwa anavizia vikosa vdogo ili airidhishe nafsi yake kwa kumdiscredit mtu. Ndo maana kashindwa kuona mantik zima. Inawezekana hata yeye hakusikia vzr. Kama Hekta 1 ni sawa na heka 2.5 then Hekta 300 ni sawa na hekari 750. Shuleni tulifundishwa kukaribisha katika mamia, maelfu au makumi yaliyo karibu. So750 inakuwa 800.Lakini suala hapa ni uharibifu wa mazingira na sio hzo figa.
 
Hili umeliskia na kulirusha haraka sana lakini wakati naibu waziri wa elimu alipotamka kuwa ,muungano wa Tanzania na zimbabwe' mbona hukurusha humu? Unafiki tu unakusumbua
 
Halafu mchungaji nae si division one fulani hivi!

Machadema mnachekesha sana! Yaani yule naibu waziri alivyokosea kuhusu muungano wa Tanzania, hapakukalika JF kwa thread za kumponda.

Leo hiki kibonzo cha Msigwa ni business as usual!!!!!! Viongozi inabidi wawe makini kabla ya kusema bhana. Nukta.
 
Wadau, naangalia Bunge Live kupitia TBC1. Mchungaji msigwa ameuliza swali la kutaka mkakati wa serikali kukabiliana na uharibifu wa mazingira kutokana na wananchi wengi kutumia nishati ya kuni kama chanzo cha nishati ya kupikia. Mchungaji msigwa amesema kuwa kwa takwimu alizonazo ni kuwa Watanzania wanakata wastani wa Ekari 300 kwa siku sawa na Hekta 800. Kwangu nilipata shida sana kumuelewa na nikajiuliza kama kweli Mchungaji Msigwa anajua anachokisema au kuna mtu amemkaririsha.

Nijuavyo ni kuwa Ekari 300 ni sawa na Hekta 121.407. Kwa wale wataalam wa kukokotoa wanaweza wakatusaidia. Hii ni kutokana na ukweli kuwa Hekta moja ni sawa na Ekari 2.5. Hivyo kwa Ekari 300, haiwezi kuwa Hekta 800. Hata kama anaweza kujitetea kuwa alibadili hivyomvipimo bila ya kujijua, Hekta 300 haiwezi kuwa sawa na Ekari 800 bali ni sawa na Ekari 741. Kutokana na ufafanuzi huo, nimemdharau sana mchungaji Msigwa na napata shida kubaini uelewa wake.

Natoa angalizo kwa wanasiasa kutokurupuka kutoa hoja ambazo hawajui undani wake. Ni vema mchungaji Msigwa angeuliza kwanza ili apate ufafanuzi wa hivi vipimo vya Hekta na Ekari ili kukwepa aibu hii iliyomkuta.

Nawasilisha.
sasa na wewe kama gari ya dizeli ukishiwa point lazima wakutoe upepo ndio uanze tena.Mimi nikajua kaaribu kweli kumbe kakosea kutoa tuu data.Poa ila ndio akili yako ilipoishia.
 
Kwani hao 'waganga wa kienyeji' na 'darasa la saba' walizaliwa humo Bungeni !? Si walipigiwa kura wakachaguliwa na mbu mbu mbu wenzako!

Kuwa na heshima mkuu, kulikoni kuniita mbumbumbu as if unanijua? Mbona onatumia lugha chafu bila sababu?

Hebu tuheshimiane tafadhali! Hunijui sikujui.
 
Hekta 300 haiwezi kuwa sawa na Ekari 800 bali ni sawa na Ekari 741.

Alichokosea hapo ni nini? alichofanya Mch. Msigwa ni kukadiria ili watu waelewe kwa urahisi, 741 kwa 800.
unajua hesabu za makadrio wewe au unaropoka tu? Usipotoshe umma
 
Hii ni sawa na data alizokuwa anazitoa Prof Muhongo pale UDSM kwenye mdahalo....zimejaa giza
 
Huyu mchungaji na Lema Lao moja.

Utakuwa umemsikia vibaya, Acha kurukaruka kama kikuku kinachotoka kuatamia. Kinyume cha hichi ulichoandika (yaani eka 800 ni karibu hekta 300). Sasa na wewe huelewi nini au umekosa cha kuandika juu ya CDM?

The Great thinker gani kama wewe ----- tu.
 
Back
Top Bottom