Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,033
- 9,923
Mchungaji Komando Mashimo amemuomba Rais Samia awalipie deni Simba na Yanga ili waweze kushinda katika michuano ya CAF. Mashimo amesema mwaka 2022 Mungu alitenda kwa ajili ya simba na yanga lakini hawakumtolea mungu walichoahidi ambacho ni kiasi cha Tsh milioni 20.
Amesema sadaka hiyo itatumika kufuta makosa ambayo Simba na Yanga wameyafanya mbele ya Mungu. Ambapo wasipotoa sadaka hiyo hawataweza kushinda kwenye michuano ya CAF mbali na fedha ambazo Rais ameahidi kwa kila goli katika michuano hiyo.
Mchungaji Mashimo amekuwa ni mtu wa kuziombea timu kushinda na kuwadai washabiki sadaka. Mwaka 2022 aliziombea Simba ikashinda moja ya mechi zake na pia aliiombea Yanga ikashinda mechi, lakini hakupewa sadaka kwa ushindi huo.
Ieleweke kwamba timu hizo hazikuwa na makubaliano ya kumpa Mashimo chochote.