Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Shida ni mkuu wa nchi alimuamini mno mno mno Bashite! Kumbe waliofanya vetting walimdanganya labda purposely!
na asipomshughulikia watasema ni kwasababu mtu kutoka kanda yake, msukuma, homeboy, mtihani hapo. kuna watu wengi wamekimbia kazi hivi juzi baada ya udahili/upekuzi vyeti maofisini, lakini jamaa ameshagundulika alikuw na magumashi, kwanini asiachishwe kazi au kwasababu ni mkuu wa mkoa.
 
Mkuu wakati mwingine usipoteze muda kuongea na Mtu mwenye ubongo wa panzi. Huyu hajui jinai ya kughushi cheti huwa inaenda mbali. Bashite alipotumia cheti cha Paul Christian aliomba pia cheti cha kuzaliwa kule RITA, Pasipoti Uhamiaji, kitambulisho cha kupiga kura NEC, kadi za Benki nk kote huko katumia jina la magumashi na kumbuka kila Taasisi ina sheria zake za adhabu kwa wale wanaotoa taarifa za gongo hivyo kwa muktadha huu nashangaa watu wanavyomtetea huyu mtu. Mimi nawashauri jambo wajaribu kufanya kama jinai ya Bashite halafu waone kama watabaki uraiani
 
Wadau nawashangaa baadhi ya watetezi wa Paulo Makonda Juu ya utumiaji wa vyeti vya MTU mwingine.Watetezi hao wanamtuhumu Askofu Gwajima eti anahubiri siasa.Napenda kuwakumbusha watetezi hao kuwa Serikali imekuwa inawaomba viongozi wa dini kuhubiri Na kukemea maovu Kwa waumini wao maovu kama wizi, rushwa madawa ya kulevya n.k.Leo Askofu Gwajima anakemea tabia chafu iliyoonyeshwa Na mmoja wa viongozi ya kugushi vyeti Ndugu Paulo Makonda anaambiwa anafanya siasa.Madhara ya vyeti feki kila MTU anayajua Serikali iko ktk zoezi la kubaini watumiaji wa vyeti feki Paulo Makonda ni sehemu ya serikali Na mtumiaji wa cheti feki je asisemwe? Mwacheni Askofu Gwajima ahubiri ili watu waongope.
 
Mkuu ni maajabu kuwa GT wengi humu JF wanashindwa kuliona hilo kwa vile mambo mengi hawayajadili kwa kutumia akili bali moyo. Wanashindwa kujua kuwa moyo hautakiwi kutumiwa katika jambo lolote zaidi ya kusukuma damu na imani ya uabudu tuu.
 
Achana na hayo mambo. La muhimu hebu tuletee live updates kutoka huko Kanisa la Ufufuo na Uzima kuhusiana na sakata la baadhi ya watendaji wakuu wa Serikali kutumia vyeti feki/hewa, elimu feki/hewa, na majina feki/bandia/hewa.
 
Updates za kanisani plz,wageni toka koromije wapo?
 
Ndio wakati halisi ambao matamko tamko yanapotokea puani. Wafalme zamani walikuwa wakitoa tamko lilikuwa halipingwi, ukilipinga unauwawa. Sasa tamko la vyeti fake limefika mahala pake hasa. Mlolongo aliopitia Mh Makonda sio mbaya maana angekuwa zero kabisa it means asingefanya vizuri hatua alizo malizia ktk kupata shahada. Mimi sioni sababu ya kusumbua Mh Makonda. Ila matamko ya walio juu yake ndio yanayo mcost sasa hivi. Wanachotakiwa ni kutekekeza kama walivyofanya kwa wengine. Hapa ndio tujue vizuri kuwa muundo wa elimu yetu sio mzuri kabisa, mhanga mmojawapo wa mfumo huu ni Mh Makonda na akina sisi hapa. Waziri wa elimu asikimbilie kufukuza walio na vyeti fake Bali alitakiwa aangalie muundo mzima wa elimu yetu upo vipi? Na kwanini mwanafunzi akifeli asiendelee na jina lake lile lile huku akiwa anayarudia masomo? Umeona hapo baada ya miaka miwili Makonda alikuwa full charge na alifanya vizuri tuu. Kwa hiyo hili lisiwe la Makonda bali waziri wa elimu alifanyie kazi hili, na wote waliondolewa kwa vyeti kama kweli alivyopitia Makonda warudishwe kazini. Tuyatafakari matamko yetu vizuri kabla ya kuyatoa kwa hadhira. Haya nimeyaandika baada ya kuelewa vizuri vile Mhe Makonda alivyopitia.
 
Paskali njaa inakuaibisha maana sasa unaongea bila kujitambua; kifupi nyaraka yoyote ya serikali ambayo alipewa mtu kwa utambulisho ikitumika vibaya serikali inaweza kumnyang'anja mtu huyo na kubatilisha maamuzi ya awali tofauti iliyopo hapa ni kwenye upande wa elimu maana hapa unaweza kunyang'anywa cheti lakini kilichopo kichwani kinabaki. Mimi kuanzia Ordinary - Adv. level nilisoma Azania Sec nawajua walimu wengi wa pale tangu wa enzi ya Mchwampaka, na Mkuu wa Shule Andrew Kwayu wakina Sebastian Ndege na kundi lake wanawajua hawa na ukiniuliza maswali kuhusu masomo nayajua mpaka leo na bahati kwenye kazi yangu sitoi maamuzi bila hesabu aka Namba kama tulivyoziita enzi zile sasa muulize Bashite kama anajua chochote kule anakodai alipitia. Tuliza njaa wewe!
 
Namkubali Makonda kwa uchapakazi.

Agenda zote za serikali ambazo huanzishwa, yeye hukamata kijiti na kuwa Imara. Iwe ni agenda ya watumishi hewa, kutengeneza madarasa na madawati n.k.

Ila katika pitapita zangu sijaona akifuatilia kwa ukaribu uhakiki wa vyeti vya watumishi.

Kiongozi toa vyeti hadharani mambo yaishe. Ukimya mbaya.

 
Ila kweli. La watumish hewa alikuwa kiherehere. Ilipofika kwenye vyeti hewa akawa kama mbwa kakutana na chita, Mkia anauweku mkunduni
 
anazunguka mbaali na kusema ni maneno ya mtandaoni bas atuwekee vyeti vyake apa mtandaoni
 
Mange kimambi ndiye aliyeibua hoja ya RC Paul Makonda kuwa alipofeli kidato cha nne, alitumia cheti cha mtu mwingine kwenda Chuo. Haijajulikana vyanzo vya habari za Mwanadada huyu anayeishi ughaibuni, lakini anaonekana kuwa "active" sana kupata habari za moto moto kutoka Bongo na kuzisambaza.

Askofu Gwajima kwakumwamini sana Mange Kimambi, alizichukua habari zile na kuzisanifu vizuri na kuongezea mbwembwe na kuzihubiri madhabahuni pa Bwana mbele ya wanakondoo wa Mungu. Huku akitegemea kupata "Updates" zingine kutoka kwa Mange, Juu ya vyeti halisi vya Mh. RC kijana zaidi nchini Tanzania aliyepewa dhamana na Mh.Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. JP Magufuli kuliongoza Jiji lenye "population" kubwa zaidi ya watu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati, Jiji la Dar es Salaam Mh.Paul C. Makonda...(mwanzilishi wa vita na mpambanaji dhididi ya madawa ya kulevya) na akahaidi kuviweka hadhalani baada ya siku tatu kwakuwa anavyo ofisini kwake.
Wataaram wa kufasiri mambo wanasema kitendo cha Askofu kumtaka RC amwombe msamaha ndani ya siku tatu lasivyo ataweka vyeti wazi, ndiyo ilikuwa inatambulisha kuwa hana, na ama alikuwa anategemea mtu ampe.

Mange Kimambi naye kule alikotegemea kupata vyeti ili aviweke mtandaoni na kumpa Askofu Gwajima NETWORK imekata.
Mange amenukuliwa ameandika hivii katika acc. yake ya Instagram "I wish I could be NECTA ningesha maliza mchezo"
Kwa kauli hii, Mange hana vyeti na Gwajima hana vyeti..wanategemea huruma ya NECTA..
GWAJIMA AMEACHWA KWENYE MATAA NA MANGE KIMAMBI.
UBARIKIWE MTUMISHI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…