Mchungaji Anthony Lusokelo apinga ndoa za mke mmoja

Mchungaji Anthony Lusokelo apinga ndoa za mke mmoja

Tatizo wakiristo kwao kuishi bila ndoa jambo la kawaida, mwanaume akikisudia kuoa mpaka siku anaoa anapitia a lot of complications, mara vikao kuchangishana mara sendof ,kitchen na receiption mpaka mtu anakuja kuoa kashakonda kwa mawazo khaa!! Mtu kama huyu lazima ndoa aone mzigo,ndoa inatakiwa iwe simpo ,mwanamke anatakiwa apewe stara yake kitchen prty ilikuwa tosha kabisa
 
Tungekuwa katika position nzuri zaidi "kutiririka" kama tungesikiliza audio. Hii screenshot kutoka Facebook haina uzito unaostahili na inawezekana ikawa uzushi tu.
 
Safi... Oa wawili, watatu, wanne, huwezi basi mpate mmoja
 
Mbona hayo ni maandishi na siyo sauti ya matamshi yake?Labda wewe unauelewa Mdogo sana.
 
Halafu waumini wake wanashangilia kama mazuzu
Sio kama mazuzu mkuu, ni mazuzu kabisa hawa wako na mawazo mgando sana. Asemacho mchungaji kwao ni sawa tu. Mfano, kuna jirani amerudi toka kanisani anaanza kuazima simu, tunamuuliza vipi simu yako? Eti nimetoa sadaka kanisani sikuwa na hela (mchungaji alisisitiza mtu lazima atoe chochote alichonacho)
 
Kwa ufahamu wako bila kujali dini unafikiri ndoa ipi nzuri, KUOA MKE MMOJA, KUOA WAKE 2, KUOA KUANZIA WAKE WATATU NA KUENDELEA, KUOA NA KUMUACHA THEN UNAOA MWINGINE, KUOANA JINSIA MOJA? Na je ni sababu gani unafikiri ni bora
Mimi bado sijapata jibu la kuniridhisha je ndoa ipi ni njema
 
Maslahi ya kuoa wake wengi ni mengi kuliko kuoa mke mmoja, na hili la kuoa wake wengi unaweza prove biologically, socially na economically.
 
Kwa mtazamo wangu naona hili swala linawawia vigumu upande WA pili nikitolea mfano una mke lakini si mwaminifu kwa maana anatoka nje ya ndoa, umefanya juhudi mbalimbali ikiwemo kwenda kwa viongozi wa dini lakini imeshindikana na imani yako inakataza kuacha wala kuoa mwanamke mwingine.
 
Ukweli upi sasa. Hakuna ukweli wowote hapo.

"Basi kwa habari ya mambo yale mlioandika, ni heri mwanamume asimguse mwañamke. Lakini kwa sababu ya zinaa kilà mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe." 1KOR 7:1-2.

Mungu alimuumbia Adamu mke mmoja (Hawa), Mungu alikuwa ana uwezo wa kumuumbia zaidi ya huyo mmoja, ila hakufanya hivyo, kwa kuwa alijua Adamu ana moyo mmoja.

Huyu "anayejiita" mchungaji halafu anapotosha Neno la Mungu ni hatari sana. Tuchukue tahadhari!
Usisahau Aulo alisema 'lile nilisemalo silitendi bali ......!
 
Kaongea ukweli mtupu wenye akili wataelewa.utalazimishaje mtu kudumu na mtu mmoja ilhali mapenzi hakuna kati yao
 
mimi naona ni bora uoe ukishindwa acha oa mwanamke mwengine mtindo wa kuoa wanawake zaidi ya mmoja waliumudu babu zetu pekee ila sisi hatuwezi kamwe....ndoa hizo zinachangamoto kubwa sana kuanzaia kwa wanawake wenyewe adi kwa watoto ni mara chache sana kukuta hawa wanawake walioolewa mitala wakipendana...na ata kama wakipendana basi ni upendo wa kinafiki...maranyingi inatakiwa ukioa wanawake wawili uwe na upendo sawa kwao...uwape matunzo sawa kadri ya uwezo wako...wala usipendelee ila kwa jamii ya hivi sasa swala hilo haliwezekani ata kidogo...cha msingi ni kuoa na kuacha mkishindwana
 
Mungu hajasema muoe mke mmoja ni watu anayekesha na Bible anawaambia hamtaki
 
Ukweli mtupu kwanza mke mke mmoja hudumaza akili
 
Hata kwa kuangalia sababu za kawaida za ki asili mchungaji mzima anashindwa kuona kwanini ni muhimu ikawa mme-mmoja-mke-mmoja!!!
 
Back
Top Bottom