Mchungaji Anthony Lusokelo apinga ndoa za mke mmoja

Mchungaji Anthony Lusokelo apinga ndoa za mke mmoja

Kwenye mioyo ya wengi wanatambua kua mchungaji kanena kweli ila humu kwenye social network baadhi ya watu watajifanya wao wakristo kweli na kumdhihaki mchungaji,uulize moyo wako kwanini unatamani mwanamke mwingine wakati una mkeo ndani?haya mambo MUNGU aliyaona sababu ndie alietuumba,anajua hali zetu wanaume akaamua kutuhalalishia zaidi ya mke mmoja,sasa kujifanya kupingana nae ni kuidanganya nafsi yako.

Kutoka 20:17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
 
Ukweli mchungu.
Ukweli upi sasa. Hakuna ukweli wowote hapo.

"Basi kwa habari ya mambo yale mlioandika, ni heri mwanamume asimguse mwañamke. Lakini kwa sababu ya zinaa kilà mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe." 1KOR 7:1-2.

Mungu alimuumbia Adamu mke mmoja (Hawa), Mungu alikuwa ana uwezo wa kumuumbia zaidi ya huyo mmoja, ila hakufanya hivyo, kwa kuwa alijua Adamu ana moyo mmoja.

Huyu "anayejiita" mchungaji halafu anapotosha Neno la Mungu ni hatari sana. Tuchukue tahadhari!
 
Kuna kitu ameona hakiko sawa. Dar ya Leo kila mwenye make mmoja lazima Ana mchepuko. Correct me if am wrong. Wanawake wengi wakishaolewa wanajisahau na hawawapi wanaume zao wanachotarajia ispokua nagging tu. Kujinusuru wanaume wanatafuta hifadhi nje. Ndio maana kuna changudoa kibao na kila barmaid Ana bwana ambae ni mume wa mtu
 
Na bado mijitu inakusanyika kanisani kwake... yani watu ubongo ukikorogwa korogwa mapema huna maamuz ya kukuweka sehemu salama.. Yesu anamuona...
 
Ameongea fact uingereza wanawake wkikiristo waliandamana kutaka ndoa ya wake wengi iwe offical ,wamechoka kuishi peke yao
 
Wengi wenye mke mmoja michepuko kibao nyuma yao. Afadhali Mchungaji ameongea ukweli japo ni mchungu.
Kuna wenye wake kadhaa na bado michepuko iko pale pale.
Baadhi ya wake walianza kama michepuko kabla ya kupanda daraja.
 
Hata Magufuli alizungumzia asili ya mwanaume wa kiafrika ni kuwa na wanawake wengi... Wengi wanaoshabikia mke mmoja hao hao wana michepuko kibao
 
Back
Top Bottom