Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

Kama kawa, mti wenye matunda hurushiwa mawe. Hongera Lusekelo, huo ndio kweli wenyewe. Walioanzisha timbwili la kumng'oa Gadafi nao wanajuta, wameshindwa kukipata kile walichoona wanakikosa kwenye utawala wa Gaddafi. Mungu ibariki Tanzania.
 
Kaisha ahidiwa barabara,ningeshangaaa sana kama angekua kinyume na mtukufu aliyetukaa ambae anataka kusikia tu ule wimbo wa hossana ndie mbarikiwa.
 
Mchungaji anae kosoa wapinzani kanisani ni RUKsa kabisaaa tena huyu hachanganyi dini na siasa.ila mchungaji anae kosoa serikali ya mtukufu huyo anachanganya dini na siasa na ni mchochezi anae wagawa wananchi.

Kwa akili hizi kama taifa bado tunaishi utumwani.
 
huyu mzee wa upako anatakiwa APAKWE UPAKO ili ajitambue
Anaelewa kwamba bila kuwananga wapinzani kula yake haitakuwepo.Anajua namna ya kutumia ile asilimia 99 iliyobaki
 
Katika hatua nyingine Mchungaji Lusekelo alimtaka Dr.Magufuli asisumbuke kubadili pesa za nchi kwani fedha zipo mtaani na maisha ni mazuri tu hakuna ugumu wowote.

ni kweli mtaan kwake hakuna ugumu kwa kua yeye c anapiga misadaka yetu wakristo, kakalisha miguu home misadaka mpesa, tigopesa, airtelmoney na banks account inaingia daily ,
Huyu ni wa kupuuzwa
 
Lusekelo

Alikula rambirambi za askofu Moses Kulola na kumsababishia mjane na familia majonzi makuu,bado LAANA haijamwacha

Hajawahi toa mtu pepo tangu nianze ona na kuhudhuria ibada zake kipindi fulani

Hana tofauti na wasanii kwa kutunzwa fedha madhabahuni kama yuko shoo

Ni mwongo kuliko shetani,mafundisho yake ni hadithi tuuuu mwanzo mwisho sijui ndio udigital

Kila anachoongea hata kama ni madudu wale waumini ni makofi tuu sijui wamelishwa nini pale

Hatumjui mama mchungaji wala hamtambulishagi maana nyendo zake tunazijua pamoja na kujisifu sana

Kwahiyo aache UNAFKI akae KIMYA aendelee kuvua hizo sadaka kwa hao anaowadanganya

Na ninaona kuna mtikisiko ataupata pale maana asidhani wote wanaoenda pale ni vichwa panzi hawawezi kuchanganua
 
'Nyakati za mwisho watatokea manabii wengi wa UONGO wakiwahadaa kwa jina langu' Hongera mzee wa Upako na mpakwa mafuta, himiza waamini wako waongeze utoaji sadaka mara dufu!
 
Yeye kwanini anajitangaza kupitia channel mbalimbali na kwanini ukipita pale ubungo river side kuna Bango lake ? Au hiyo ndio biashara yake
 
MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO MAARUFU KAMA MZEE WA UPAKO AMEWATAKA WAPINZANI WASIVURUGE AMANI YA NCHI YETU.

Mzee wa upako aliyasema hayo katika Ibada takatifu tarehe 18 September 2016 na baadae, mahubiri hayo kurushwa hewani na Channel ten tarehe 22 September 2016.

Mchungaji Lusekelo aliwaambia waumini wake kuwa kwa sasa maisha yanaenda vizuri na Rais Magufuli anafanya tulichokuwa tunataka kwa miaka mingi kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma.

Kuhusu suala la pesa kukosekana mtaani Mchungaji Lusekelo alisema ninanukuu "Pesa zipo mtaani kama kawaida lakini kwa watu wanaofanya kazi na sio wavivu, na zamani pesa zilizagaa kwa sababu ya ubadhirifu wa mali za umma" pia kasema yeyote anayelalamika ni yule aliyekuwa anapata pesa kwa njia zisizo halali.

Katika hatua nyingine Mchungaji Lusekelo alimtaka Dr.Magufuli asisumbuke kubadili pesa za nchi kwani fedha zipo mtaani na maisha ni mazuri tu hakuna ugumu wowote.

Pia aliwataka waumini wake wasijaribu kushiriki katika maandamano yeyote yale na wala wasidanganyike kuchezea amani ya nchi kwa watu wenye uroho wa madaraka na kuwadanganya kuwa Magufuli kabana demokrasia wakati sio sahihi kabisa.

Mchungaji Lusekelo, alitoa mifano miwili ili kuwaelimisha waumini wake, wa kwanza ni nchi ya Gaboni mzee wa upako aliwaambia nchi hii imeharibiwa na watu wasiozidi elfu 3,000 kwa kuingia barabarani na kuanzisha maandamano na sasa nchi ile imevurugika.

Mfano mwingine katolea nchi ya Brazili, kuwa Taifa hili limevurugwa na watu wasiozidi elfu 10,000 baada ya kuingia barabarani na kuandamana na kusababisha machafuko na nchi kutotawalika.

Mzee wa upako alilaaani vikali oparesheni UKUTA iliyokuwa imetangazwa kufanyika tarehe moja September mwaka huu kwa kusema, ilisababisha Taifa kukosa watalii kuja kuangalia kupatwa kwa jua kule Mbeya kwa kuhofia machafuko nchini nakuwataka wapinzani wasirudie kitendo hiki.

Mwisho Mzee wa upako ametangaza kutumbua majipu mpaka kanisani na ikiwezekana kukata mguu wenye jipu ili jipu litoke na mtu aweze kuishi, baada ya hapo alimalizia kwa kuimba wimbo wa Tanzania.

Hongera sana mchungaji Lusekelo hakika umenena vyema.
Imeandaliwa na wenu,
MWITA NYARUKURURU
Mchumia tumbo Huyo...amezoea kuwaibia wajinga na wafia imani hao na pia naona anatukana na kudharau madhehebu mengine kwa bidii zote lkn ajue Mungu si wa kuchezea huyu hana tofauti na kibwetere pale Uganda.
 
Jamaa linawaponda wanaume wanaopewa ela na wanawake wakati huo yeye naye anapokea za haohao wanawake
NJAA MBAYA SANA

Duuuh kama hali yenyewe ndio hivyo ni bora kuanzisha kanisa sasa kumbe inalipa duuh.watu wanamchangai mchungaji wanawaacha masikini omba omba mtaani wanahangaika duuuh hii ni hatari kabisa.tumuogopeni Mwenyezi Mungu alie tuumba
 
Kuna

Tafiti imesema watanzania wanatumia asilimia moja ya akili zao.
Yaaani kweli hili ni zigo tumebebeshwa sisi waafrika vichwani mwetu jamaaa yupo kazini hapo harafu anawaambia vijana wakafanye kazi ile wakipata wamletee
 
Wakati nikiwa mtoto nilikuwa nawashangaa watu wazima wasio na hela. Nikapenda nikiwa mkubwa niwe mwana mazingaombwe ili niwe natengeneza hela maana nilikuwa naona wanaokota magazeti halafu wanatengeneza hela.
Enhe sasa hivi upo vipi?
 
Kama kawa, mti wenye matunda hurushiwa mawe. Hongera Lusekelo, huo ndio kweli wenyewe. Walioanzisha timbwili la kumng'oa Gadafi nao wanajuta, wameshindwa kukipata kile walichoona wanakikosa kwenye utawala wa Gaddafi. Mungu ibariki Tanzania.

acha hzo na kufikiri kama kifaranga nani kakwambia anataka kumngoa rais madarakani?
usichanganye vitu watu wanaposoma na kuelewa uhalisia wa mambo huwezi kuwadanganya ndo zama hizi watz wengi wana elimu na hawadanganywi?
 
Ukiangalia michango ya watu humu ndani. Utagundua asilimia kubwa ya watanzania walikuwa wanaishi sivyo halali. It either hakusoma kha lala, au kupata kazi kihalali, au kupata pesa kihalali. Mbaya zaidi tunajifanya hatujui kuwa yasiyohaki yote hayatoki kwa Mungu! Hatumwogopi Mungu! Hatuna dini sijui? Badala ya kutubu na kuacha tunalalamika kama Israel jangwani.

Ndiyo maana Kenya na majirani zetu wanatuzarau kwenye ajira East afrika watanzania hawachomozi sababu hata elimu yetu ni figisu.

Humu ndani wana otoscope ni wale walioiba mitihani toka darasa la 7 , for 4, 6 na chuo ni wadesaji wakubwa. Wakapata kazi zisizo haki yao , mbaya zaidi wa kawa wapiga dili wakubwa. Unafikiri Mungu atasimama na watu gani?
LUSEKERO anapoongea roho zinawauma vibaya sana.

Mimi nasema hivi kama vile Mungu anabariki na kusimamia kwenye haki basi utawala wa MAGUFULI utawashangaza wengi. ..kwani atasimama naye. Mnamtafutia sababu, mnamkashifu na kusema vibaya.Lakini mtaumbuka kwa ubaya wenu wanafiki ninyi
 
MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO MAARUFU KAMA MZEE WA UPAKO AMEWATAKA WAPINZANI WASIVURUGE AMANI YA NCHI YETU.

Mzee wa upako aliyasema hayo katika Ibada takatifu tarehe 18 September 2016 na baadae, mahubiri hayo kurushwa hewani na Channel ten tarehe 22 September 2016.

Mchungaji Lusekelo aliwaambia waumini wake kuwa kwa sasa maisha yanaenda vizuri na Rais Magufuli anafanya tulichokuwa tunataka kwa miaka mingi kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma.

Kuhusu suala la pesa kukosekana mtaani Mchungaji Lusekelo alisema ninanukuu "Pesa zipo mtaani kama kawaida lakini kwa watu wanaofanya kazi na sio wavivu, na zamani pesa zilizagaa kwa sababu ya ubadhirifu wa mali za umma" pia kasema yeyote anayelalamika ni yule aliyekuwa anapata pesa kwa njia zisizo halali.

Katika hatua nyingine Mchungaji Lusekelo alimtaka Dr.Magufuli asisumbuke kubadili pesa za nchi kwani fedha zipo mtaani na maisha ni mazuri tu hakuna ugumu wowote.

Pia aliwataka waumini wake wasijaribu kushiriki katika maandamano yeyote yale na wala wasidanganyike kuchezea amani ya nchi kwa watu wenye uroho wa madaraka na kuwadanganya kuwa Magufuli kabana demokrasia wakati sio sahihi kabisa.

Mchungaji Lusekelo, alitoa mifano miwili ili kuwaelimisha waumini wake, wa kwanza ni nchi ya Gaboni mzee wa upako aliwaambia nchi hii imeharibiwa na watu wasiozidi elfu 3,000 kwa kuingia barabarani na kuanzisha maandamano na sasa nchi ile imevurugika.

Mfano mwingine katolea nchi ya Brazili, kuwa Taifa hili limevurugwa na watu wasiozidi elfu 10,000 baada ya kuingia barabarani na kuandamana na kusababisha machafuko na nchi kutotawalika.

Mzee wa upako alilaaani vikali oparesheni UKUTA iliyokuwa imetangazwa kufanyika tarehe moja September mwaka huu kwa kusema, ilisababisha Taifa kukosa watalii kuja kuangalia kupatwa kwa jua kule Mbeya kwa kuhofia machafuko nchini nakuwataka wapinzani wasirudie kitendo hiki.

Mwisho Mzee wa upako ametangaza kutumbua majipu mpaka kanisani na ikiwezekana kukata mguu wenye jipu ili jipu litoke na mtu aweze kuishi, baada ya hapo alimalizia kwa kuimba wimbo wa Tanzania.

Hongera sana mchungaji Lusekelo hakika umenena vyema.
Imeandaliwa na wenu,
MWITA NYARUKURURU
Kiongozi wa dini kazi yake Ni moja; kuwatangazia watu neno la mungu. Haya mambo mengine wawachie wanasiasa maana siku hizi kuna hali inaanza kujitokeza kwamba unashindwa kutofautisha viongozi wa dini na wale wa siasa. Kuna tukio kubwa la kidini mgeni rasmi ni mwanasiasa. Mwanasiasa anaanza kumwaga sera za chama chake na wakati mwingine vijembe Kwa wasiasa wa upande mwingine kitu ambacho sidhani kama waumini Kwa siku ndio wanataka kusikia.

Reasoning ya waumini wa kidini iko limited sana, wasipokuwa wadadisi huwa inaishia Kwa kile anachojifunza kutoka Kwa kiongozi wake, Kwa kuchanganya dini na siasa huwa mara nyingi kumezaa vita vya kishenzi ambavyo huwa havina kichwa wala miguu.

Mwisho ningeomba viongozi wa dini wafanye kazi yao ya kueneza neno na wanasiasa wafanye kazi yao ya uongozi (na wala Sio utawala) wasiwatumie viongozi wa dini kutimiza mambo yao ya kisiasa watatupeleka kubaya.

Pia kama viongozi wa dini wanalazimika kuongelea mambo ya siasa basi wasichukue upande maana kwenye makanisa yao kuna waumini wa itikadi tofauti tofauti, wanawakwaaza.
 
Back
Top Bottom