Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

Hongera yake ana Wateja kibao kwenye biashara yake. Hakosi milioni kadhaa kila Jumapili.
 
Tatizo njaa,Wanaojiita viongozi wa dini wachungaji.NJAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

Sasa nyinyi wakati Aikael anaahirisha ukuta alisema mlikuwa na mazungumzo na viongozi wa dini. Lusekelo ni mmoja wa viongozi wa dini pia. Ina maana mlitaka kukutana na viongozi wa dini wakati mnadai wana njaa?
 
Na bado tutauza utu wetu mpaka kieleweke....utakuja kushituka kama pesa hakuna kwa mtaa ukiona sadaka zimepungua....endelea tu na unabii wa kisiasa.

Sasa nyinyi wakati mnaahirisha ukuta mlitaka kuongea na viongozi wepi wa dini?
 
Watu wapuuzi wajinga kabisa. Eti anakuobea utajirike wakati yeye anakusanya elfu moja ya masikini. Si ajiombee atajirike. Mijitu inashindwa kujiuliza kama ana nguvu za hivyo mbona anakusanya hela yetu sisi masikini.

Mbona chadema wanafanyaga harambee kukusanya hela kutoka kwa sisi wanachama masikini wakati wanapata ruzuku kutoka serikalini?
 
Kuna kipindi alikuwa mchungaji pendwa wa UKAWA kama Gwajima.
Sijui kama UKAWA wataendelea kumsifia tena.
 
Bila shaka huyu mchungaji ni mzaliwa wa kanda ya ziwa na bila shaka ni Msukuma, ndiyo tabiya za wasukuma waliowengi huwa hawapendi kukosoa watu wa kwao, ukitaka kujua hili tafuta wachungaji wote wasukuma na ujalibu kuwahoji kuhusu utendaji wa mkulu utapata majibu.

NB.Hata mm ni Msukuma but inashangaza hata mtaani huku kanda ya ziwa watu wanataka hadi kugombana kwa kumkosoa mkulu. Ni shiiidaaa aiseee.
 
Sasa nyinyi wakati Aikael anaahirisha ukuta alisema mlikuwa na mazungumzo na viongozi wa dini. Lusekelo ni mmoja wa viongozi wa dini pia. Ina maana mlitaka kukutana na viongozi wa dini wakati mnadai wana njaa?

Hahhahahahahah unavituko wewe.Ulielezwa viongozi wa dini hao wengine hawako huko kwa maana wanawakilishwa na viongozi walioko kwenye muungano wa CCT.Pole ndiyo maisha hivyo huyo ni mchumia tumbo angeenda kumuuliza muwakilishi wake kwanza kabla ya kuingia kwenye media
 
Kuna kipindi alikuwa mchungaji pendwa wa UKAWA kama Gwajima.
Sijui kama UKAWA wataendelea kumsifia tena.
 
Kama Mnakumbuka Rais Magufuli alipomtembelea alionyesha Kuogopa na Kustuka sana Mwanzo. Hakuamini Kama Rais Kaja Kusali alifikiri Kuwa Amekuja Kumtumbua! Maana Biblia Inasema Waovu wanatimua mbio wakati hakuna awafukuzaye!
 
MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO MAARUFU KAMA MZEE WA UPAKO AMEWATAKA WAPINZANI WASIVURUGE AMANI YA NCHI YETU.

Mzee wa upako aliyasema hayo katika Ibada takatifu tarehe 18 September 2016 na baadae, mahubiri hayo kurushwa hewani na Channel ten tarehe 22 September 2016.

Mchungaji Lusekelo aliwaambia waumini wake kuwa kwa sasa maisha yanaenda vizuri na Rais Magufuli anafanya tulichokuwa tunataka kwa miaka mingi kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma.

Kuhusu suala la pesa kukosekana mtaani Mchungaji Lusekelo alisema ninanukuu "Pesa zipo mtaani kama kawaida lakini kwa watu wanaofanya kazi na sio wavivu, na zamani pesa zilizagaa kwa sababu ya ubadhirifu wa mali za umma" pia kasema yeyote anayelalamika ni yule aliyekuwa anapata pesa kwa njia zisizo halali.

Katika hatua nyingine Mchungaji Lusekelo alimtaka Dr.Magufuli asisumbuke kubadili pesa za nchi kwani fedha zipo mtaani na maisha ni mazuri tu hakuna ugumu wowote.

Pia aliwataka waumini wake wasijaribu kushiriki katika maandamano yeyote yale na wala wasidanganyike kuchezea amani ya nchi kwa watu wenye uroho wa madaraka na kuwadanganya kuwa Magufuli kabana demokrasia wakati sio sahihi kabisa.

Mchungaji Lusekelo, alitoa mifano miwili ili kuwaelimisha waumini wake, wa kwanza ni nchi ya Gaboni mzee wa upako aliwaambia nchi hii imeharibiwa na watu wasiozidi elfu 3,000 kwa kuingia barabarani na kuanzisha maandamano na sasa nchi ile imevurugika.


Mfano mwingine katolea nchi ya Brazili, kuwa Taifa hili limevurugwa na watu wasiozidi elfu 10,000 baada ya kuingia barabarani na kuandamana na kusababisha machafuko na nchi kutotawalika.

Mzee wa upako alilaaani vikali oparesheni UKUTA iliyokuwa imetangazwa kufanyika tarehe moja September mwaka huu kwa kusema, ilisababisha Taifa kukosa watalii kuja kuangalia kupatwa kwa jua kule Mbeya kwa kuhofia machafuko nchini nakuwataka wapinzani wasirudie kitendo hiki.

Mwisho Mzee wa upako ametangaza kutumbua majipu mpaka kanisani na ikiwezekana kukata mguu wenye jipu ili jipu litoke na mtu aweze kuishi, baada ya hapo alimalizia kwa kuimba wimbo wa Tanzania.

Hongera sana mchungaji Lusekelo hakika umenena vyema.
Imeandaliwa na wenu,
MWITA NYARUKURURU

Mchungaji Lusekelo ni kiongozi wa kiroho, maneno anayohubiri kwa waumini wake ni dogmatic statements........ hayahojiwi!!!! Ushauri: asipende sana kuzungumzia mambo ambayo ni ya kisiasa na kutoa vule judgements. Yeye ahubiri, aonye, na kutoa maelekezo bila kuzungumzia dialogue za kisiasa zinazoendela
 
Eti Mchungaji!!

Mchungaji wa nini, mtuambie.
Ni mcungaji au mchunguliaji??
 
Back
Top Bottom