Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

Huyu ndiye aliyejengewa barabara yenye kiwango cha lami na Mtukufu mpaka mlangoni mwa kanisa lake na kuacha barabara kuu ya kule kibangu inayotumiwa na wakazi wengi wa eneo hilo?Sasa kwa hali hiyo kwa nini hasimtumikie mjenzi?.
Miongoni mwa "wachungaji" wasaka fursa ni huyo. Kila kauli anayoitoa inapaswa kufanyiwa "uchunguzi"!
 
Mtoa mada ina maana hujaona mengine aliyoyahubiri Mtumishi lusekelo? tena hayo uliyoyaandika kaongea kwa dak chache sana,,,yule jamaa siku hizi yuko vizuri sana anatumia muda mwingi kuwafundisha watu neno la Bwana, ili wapone kupitia neno na imani...sio kama hao wachawi wanaopiga watu mieleka na kuwaroga...jitahid ukifatilia jambo basi chukua nyeti acha makapi
 
Najua sana Maswala ya Imani za Kipentecoste, Wapo wachungaji ambao kweli Nia yao Ni Kusaidia Wakristo walio makanisani mwao kiroho na Kijamii. Ila Nasema Mbele za Mungu na ananisikia, Nina Uhakika 900,000% Kuwa Anthony Lusekelo ni TAPELI. ajaribu Kubisha kuna Nyeti zake mahali fulani!

Huyu jamaa alishawahi kusema kwamba apo kanisani kwake yeye ndio steering siku akifa ndo picha limeisha,
sasa swali akifa waumini wake atawacha na nani kama mchungaji wao?
 
Lazima mbegu ife ili ikue haiwezekani nchi iwe imeliwa na katika kuliwa kwake isimame ghafla iendelee.
Lazima tupitie ugumu ili tupate ubora wa maisha siasa na wanasiasa ila kiuhalisia unapofumua uozo lazima harufu itoke kwanza lakini baada ya muda itakwisha na raha tutaipata ya mateso yetu.
Maendeleo hayaletwi kwenye kisahani
 
Mimi na mheshimu sana mtumishi Antony Lusekelo.Lakini baada ya kutoa onyo kwa chadema nilitegemea angetoa ushauri kwa serikali si dhani kama serikali haina udhaifu mahali popote.Nawashauri watumishi wa Mungu waige mfano wa Yohana Mbatizaji ili utumishi wenu tusiutilie mashaka.
 
Prosperity gospel is totally masonic, so hatushangai kusikia hayo toka kwake na off course haishi mtaani ndiyo maana hajui kuwa maisha yamekuwa magumu muno mtaani
 
Mzee wa Upako Ni Tapeli, sawa Na Huyu Hapa Mshirika Wake! huyu, Angalia Hii Video Utashangaa


Ukweli Ni Kuwa Mimi Nimekuwa Mpentecoste Tangu 1991, Nimeokoka, Nimeona Wachungaji Wengi ambao Ni Mithili ya Malaika Kwa Upendo wao Kwa Mungu, Bila Kujali Madhehebu hasa. Mfano wa Hao Ni Marehemu Kulola, Mwakasege, Marehemu Mzee ABC Mabondo, Mch. Hiza, Mch. Kyara, Mch. Ufwiki, Na Wengine wengi, Lakini Kwa Kiasi cha kutisha cha Asilimia 98% Michungaji Mingine Ni Mbwa Mwitu na Mbweha. Wanatafuna Maisha ya Watu, Roho akili hata Mifupa.
Na Kwa Uchunguzi wangu Lusekelo Ni Mmjawapo wa Matapeli hao. Gwajima am Not Sure kuwa Ni Mwovu Kwa Kuwa Mungu aniue leo, Miaka kama 18 iliyopita Nilishirikiana naye sana, Na anasali Kiasi cha Kufa. Anaupendo wa Kiukweli. Na Nimeona Kweli Mungu akimtumia, na Kama Insider, sijawahi kuona akitunga au kustage kitu cha Uwongo sasa hiyo Ni miaka 18 iliyopita.
 
Chadema wanafanya usanii.

Wanataka tufikirie nchi iko katika hatari kubwa,kumbe yakifanyika maandamano,ni Chadema tu ndio watakaodhurika.
Hakuna hatari yoyote kwa nchi. Mazungumzo yao ya maandamano,labda kuna perceived injustice ambazo zinafanya wachanganyikiwe akili,wasione hatari za kuandamana wakati numbers hazitoshi.
 
MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO MAARUFU KAMA MZEE WA UPAKO AMEWATAKA WAPINZANI WASIVURUGE AMANI YA NCHI YETU.

Mzee wa upako aliyasema hayo katika Ibada takatifu tarehe 18 September 2016 na baadae, mahubiri hayo kurushwa hewani na Channel ten tarehe 22 September 2016.

Mchungaji Lusekelo aliwaambia waumini wake kuwa kwa sasa maisha yanaenda vizuri na Rais Magufuli anafanya tulichokuwa tunataka kwa miaka mingi kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma.

Kuhusu suala la pesa kukosekana mtaani Mchungaji Lusekelo alisema ninanukuu "Pesa zipo mtaani kama kawaida lakini kwa watu wanaofanya kazi na sio wavivu, na zamani pesa zilizagaa kwa sababu ya ubadhirifu wa mali za umma" pia kasema yeyote anayelalamika ni yule aliyekuwa anapata pesa kwa njia zisizo halali.

Katika hatua nyingine Mchungaji Lusekelo alimtaka Dr.Magufuli asisumbuke kubadili pesa za nchi kwani fedha zipo mtaani na maisha ni mazuri tu hakuna ugumu wowote.

Pia aliwataka waumini wake wasijaribu kushiriki katika maandamano yeyote yale na wala wasidanganyike kuchezea amani ya nchi kwa watu wenye uroho wa madaraka na kuwadanganya kuwa Magufuli kabana demokrasia wakati sio sahihi kabisa.

Mchungaji Lusekelo, alitoa mifano miwili ili kuwaelimisha waumini wake, wa kwanza ni nchi ya Gaboni mzee wa upako aliwaambia nchi hii imeharibiwa na watu wasiozidi elfu 3,000 kwa kuingia barabarani na kuanzisha maandamano na sasa nchi ile imevurugika.

Mfano mwingine katolea nchi ya Brazili, kuwa Taifa hili limevurugwa na watu wasiozidi elfu 10,000 baada ya kuingia barabarani na kuandamana na kusababisha machafuko na nchi kutotawalika.

Mzee wa upako alilaaani vikali oparesheni UKUTA iliyokuwa imetangazwa kufanyika tarehe moja September mwaka huu kwa kusema, ilisababisha Taifa kukosa watalii kuja kuangalia kupatwa kwa jua kule Mbeya kwa kuhofia machafuko nchini nakuwataka wapinzani wasirudie kitendo hiki.

Mwisho Mzee wa upako ametangaza kutumbua majipu mpaka kanisani na ikiwezekana kukata mguu wenye jipu ili jipu litoke na mtu aweze kuishi, baada ya hapo alimalizia kwa kuimba wimbo wa Tanzania.

Hongera sana mchungaji Lusekelo hakika umenena vyema.
Imeandaliwa na wenu,
MWITA NYARUKURURU
Huyo ni Mchungaji au mburudishaji? Sijawahi KUONA Mchungaji yoyote anayetunzwa wakati wa mahubiri. Msaka Tonge.
 
Hili jamaa linajuwa kuwatapeli wateja wake hivyo visadaka ni mipango imepangwa anaanza mtu wake wa Mipango wateja wanafuata MAUCHAWI tu hahaahaaaaaa mkorogo kwenye USO unavyo bembelezwa kwa sponji lainii duh nabii luseke nomaa MAUJANJA tu
 
Akili ndogo kabisa hii. Cdm wanasababisha vipi uvunjifu wa amani? Tangu cdm waijue katiba, watu wanatafsir kwamba ni wavunjifu wa amani. Huu ni ujinga wa karne
 
Back
Top Bottom