Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

Hongera sana Mch Lusekelo a.k.a Transformer! Ingawa kanisani si pa hala pa siasa ila ni muhimu kuwaelewesha kwani amani ikikosekana hata wewe huwezi kutoa huduma. cc BAK, Daudi Mchambuzi, Nyani Ngabu na wale wanafiki wote wa kila chama kilichokufa siku nyingi
Ukumbuke kwamba amani ni tunda la haki na wala haliji Kwa kupiga kelele majukwani kwa kuapa kwamba tutailinda amani kwa nguvu zetu zote wakati upande mwingine unakanyaga haki za watu.

Maendeleo ya watu huru ni muhimu sana kuliko 'maendeleo' ya kuambiwa na watu wengine kwamba tumeendelea.
 
Kama tunazungumzia uchochezi basi Lusekelo ni mchochezi namba moja.
JE itakuwaje iwapo kila anayejiita kiongozi wa kidini wakitoa matamko ya kisiasa kama ya huyu Bw.Lusekelo?
Ninaamini viongozi wa dini wanapaswa kutokuwa na upande katika mambo ya kisiasa isipokuwa wanatakiwa kutetea wananchi pale haki zao zinapominywa.
Nilitegemea Lusekelo angetumia ukaribu wake na Rais kumshauri Rais aruhusu vyama vyote vifanye siasa kwa mujibu wa katiba.
 
Wachungaji wa shilingi wa kidigitali

Yeye anasema maisha yametulia sababu anajua ana uhakika wa kula kwa wale anaowadanganya kila siku
Ambao bado wanawafuata wachungaji matapeli wa imani wana matatizo ya akili inabidi wapimwe.
 
Hongera sana Mch Lusekelo a.k.a Transformer! Ingawa kanisani si pa hala pa siasa ila ni muhimu kuwaelewesha kwani amani ikikosekana hata wewe huwezi kutoa huduma. cc BAK, Daudi Mchambuzi, Nyani Ngabu na wale wanafiki wote wa kila chama kilichokufa siku nyingi
Mkumbushe Dr. Mwakyembe aliyetangaza kuwa atakayehubir siasa makanisani wakamatwe hivyo anaweza kuanza na huyu anayekula kwa kuwadanganya waumini wake
 
juzi hapa umekuja na habari ya kumlaani padri kwa kuikosoa serikali kanisani leo unakuja na porojo za mchungaji kuuponda upinzani kanisani.halafu unachekelea kama zuzu vile.
 
MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO MAARUFU KAMA MZEE WA UPAKO AMEWATAKA WAPINZANI WASIVURUGE AMANI YA NCHI YETU.

Mzee wa upako aliyasema hayo katika Ibada takatifu tarehe 18 September 2016 na baadae, mahubiri hayo kurushwa hewani na Channel ten tarehe 22 September 2016.

Mchungaji Lusekelo aliwaambia waumini wake kuwa kwa sasa maisha yanaenda vizuri na Rais Magufuli anafanya tulichokuwa tunataka kwa miaka mingi kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma.

Kuhusu suala la pesa kukosekana mtaani Mchungaji Lusekelo alisema ninanukuu "Pesa zipo mtaani kama kawaida lakini kwa watu wanaofanya kazi na sio wavivu, na zamani pesa zilizagaa kwa sababu ya ubadhirifu wa mali za umma" pia kasema yeyote anayelalamika ni yule aliyekuwa anapata pesa kwa njia zisizo halali.

Katika hatua nyingine Mchungaji Lusekelo alimtaka Dr.Magufuli asisumbuke kubadili pesa za nchi kwani fedha zipo mtaani na maisha ni mazuri tu hakuna ugumu wowote.

Pia aliwataka waumini wake wasijaribu kushiriki katika maandamano yeyote yale na wala wasidanganyike kuchezea amani ya nchi kwa watu wenye uroho wa madaraka na kuwadanganya kuwa Magufuli kabana demokrasia wakati sio sahihi kabisa.

Mchungaji Lusekelo, alitoa mifano miwili ili kuwaelimisha waumini wake, wa kwanza ni nchi ya Gaboni mzee wa upako aliwaambia nchi hii imeharibiwa na watu wasiozidi elfu 3,000 kwa kuingia barabarani na kuanzisha maandamano na sasa nchi ile imevurugika.

Mfano mwingine katolea nchi ya Brazili, kuwa Taifa hili limevurugwa na watu wasiozidi elfu 10,000 baada ya kuingia barabarani na kuandamana na kusababisha machafuko na nchi kutotawalika.

Mzee wa upako alilaaani vikali oparesheni UKUTA iliyokuwa imetangazwa kufanyika tarehe moja September mwaka huu kwa kusema, ilisababisha Taifa kukosa watalii kuja kuangalia kupatwa kwa jua kule Mbeya kwa kuhofia machafuko nchini nakuwataka wapinzani wasirudie kitendo hiki.

Mwisho Mzee wa upako ametangaza kutumbua majipu mpaka kanisani na ikiwezekana kukata mguu wenye jipu ili jipu litoke na mtu aweze kuishi, baada ya hapo alimalizia kwa kuimba wimbo wa Tanzania.

Hongera sana mchungaji Lusekelo hakika umenena vyema.
Imeandaliwa na wenu,
MWITA NYARUKURURU
Duh labda mchungaji anaishi nchi nyingine siyo hii ya kwetu.
 
Ukiangalia michango ya watu humu ndani. Utagundua asilimia kubwa ya watanzania walikuwa wanaishi sivyo halali. It either hakusoma kha lala, au kupata kazi kihalali, au kupata pesa kihalali. Mbaya zaidi tunajifanya hatujui kuwa yasiyohaki yote hayatoki kwa Mungu! Hatumwogopi Mungu! Hatuna dini sijui? Badala ya kutubu na kuacha tunalalamika kama Israel jangwani.
Ndiyo maana Kenya na majirani zetu wanatuzarau kwenye ajira East afrika watanzania hawachomozi sababu hata elimu yetu ni figisu .
Humu ndani wana otoscope ni wale walioiba mitihani toka darasa la 7 , for 4, 6 na chuo ni wadesaji wakubwa. Wakapata kazi zisizo haki yao , mbaya zaidi wa kawa wapiga dili wakubwa. Unafikiri Mungu atasimama na watu gani?
LUSEKERO anapoongea roho zinawauma vibaya sana.
Mimi nasema hivi kama vile Mungu anabariki na kusimamia kwenye haki basi utawala wa MAGUFULI utawashangaza wengi. ..kwani atasimama naye. Mnamtafutia sababu, mnamkashifu na kusema vibaya.Lakini mtaumbuka kwa ubaya wenu wanafiki ninyi
Mbona padri mapunda aliposema serikali iache ubabe na iwache Uhuru wa vyama vya siasa mlimjia juu ? Kwahiyo mchungaji akiwa upande wa ccm kasema kweli ila padri akiwa upande wa upinzani hafai. Pumbavu zenu kabisa
 
Juzi hapa umekuja na habari ya kumlaani padri kwa kuikosoa serikali kanisani leo unakuja na porojo za mchungaji kuuponda upinzani kanisani.halafu unachekelea kama zuzu vile.

kati ya wapuuzi walioko humu JF mwita nyarukururu unaitaji ukatubu kwasababu padri akiwa kiongozi wa waumini ambao ni kati wtz mil 50 kaikanya serikali juu ya hatua za kibabe ukatunisha misuli kama ibilisi kumponda leo hapa Lusekelo kaisifu serikali unatunisha misuli kama goliati kumpulisize wakati watu ndo wanajua hali walizonazo huku mitaani kisa unataka kuwa promoted na serikali jitahidi ila sidhani kama utakua na nafasi coz wanaochaguliwa na rais wengi wao ni PHD holder wakati ww ulifeli chuo.

Nakuomba acha siasa katika neno la Mungu lilihakikiwa likikugeuka hata shetani atakukataa hivyo "KATUBU" na unapo post thread zako dont mix faith na politics Asante
 
Ndio maana nasema dini ni mastory ya watu
Unaweza hata kuhoji uwepo wa Mungu??Unaamini kuna maisha baada ya kifo??Kama huwezi/huamini basi tafuta namna yako ya kumfikia!Kwa sababu mpk sasa ni dini ndizo zinazoeleza unawezaje kumfikia!
 
Haki yake kuhubili siasa Kanisani analinda mkate wake! Waumini wake mmepewa onyo atawatum ua askofu wenu Kaeni macho, kunya anye kuku akinya bata taabu yaani hapo angekwa gwajima asemee upande wa pili ilikiwa shida!
 
Lusekelo

Alikula rambirambi za askofu Moses Kulola na kumsababishia mjane na familia majonzi makuu,bado LAANA haijamwacha

Hajawahi toa mtu pepo tangu nianze ona na kuhudhuria ibada zake kipindi fulani

Hana tofauti na wasanii kwa kutunzwa fedha madhabahuni kama yuko shoo

Ni mwongo kuliko shetani,mafundisho yake ni hadithi tuuuu mwanzo mwisho sijui ndio udigital

Kila anachoongea hata kama ni madudu wale waumini ni makofi tuu sijui wamelishwa nini pale

Hatumjui mama mchungaji wala hamtambulishagi maana nyendo zake tunazijua pamoja na kujisifu sana

Kwahiyo aache UNAFKI akae KIMYA aendelee kuvua hizo sadaka kwa hao anaowadanganya

Na ninaona kuna mtikisiko ataupata pale maana asidhani wote wanaoenda pale ni vichwa panzi hawawezi kuchanganua
Labda mpelekee dada yako awe mama mchungaji
 
Lusekelo

Alikula rambirambi za askofu Moses Kulola na kumsababishia mjane na familia majonzi makuu,bado LAANA haijamwacha

Hajawahi toa mtu pepo tangu nianze ona na kuhudhuria ibada zake kipindi fulani

Hana tofauti na wasanii kwa kutunzwa fedha madhabahuni kama yuko shoo

Ni mwongo kuliko shetani,mafundisho yake ni hadithi tuuuu mwanzo mwisho sijui ndio udigital

Kila anachoongea hata kama ni madudu wale waumini ni makofi tuu sijui wamelishwa nini pale

Hatumjui mama mchungaji wala hamtambulishagi maana nyendo zake tunazijua pamoja na kujisifu sana

Kwahiyo aache UNAFKI akae KIMYA aendelee kuvua hizo sadaka kwa hao anaowadanganya

Na ninaona kuna mtikisiko ataupata pale maana asidhani wote wanaoenda pale ni vichwa panzi hawawezi kuchanganua
Hawezi kupata mtikisiko labda wale mafisadi ndo watahama kusali kanisani kwake
 
Back
Top Bottom