Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

hili jamaa linawekewagwa pombe kwenye pepsi pale golden tulip...!!!
Ahya! yaani licha ya kutumika kwa mbinu ya kijasusi hivyo bado watabe mmeinyaka?....loh! kama ni kweli Mkuu wewe noma sana.
 
Jamaa linawaponda wanaume wanaopewa ela na wanawake wakati huo yeye naye anapokea za haohao wanawake
NJAA MBAYA SANA

Aisee umemshika pabaya sana....yaani anapokea pesa hapo hapo bila ya watu kugundua kwamba anajisema...duh kweli kazi ipo.
 
Mbona wakati wa JK hawakusema kuwepo huo ubadhirifu wa fedha? Tangu Magufuli alipoingia kanisani kwake na kuahidi kujenga barabara inayopita jirani na kanisa lake ameona ni kitu kikubwa sana!
 
Kuvurugika kwa amani kunahitaji idadi ipi ya watu. Chumvi kwenye mboga au Njiti ya kiberiti na msitu?
 
kuna tetesi kwamba aliombwa na ccm ili kuokoa jahazi 2015 na alikubali , sijui ikawaje akasimama monaban .
Arusha CDM sasa angekubali kuvaa shati la kijani angepoteza wateja wake baada ya uchaguzi....ila wachungaji wengi ni njaa tu nothing more.
 
MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO MAARUFU KAMA MZEE WA UPAKO AMEWATAKA WAPINZANI WASIVURUGE AMANI YA NCHI YETU.

Mzee wa upako aliyasema hayo katika Ibada takatifu tarehe 18 September 2016 na baadae, mahubiri hayo kurushwa hewani na Channel ten tarehe 22 September 2016.

Mchungaji Lusekelo aliwaambia waumini wake kuwa kwa sasa maisha yanaenda vizuri na Rais Magufuli anafanya tulichokuwa tunataka kwa miaka mingi kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma.

Kuhusu suala la pesa kukosekana mtaani Mchungaji Lusekelo alisema ninanukuu "Pesa zipo mtaani kama kawaida lakini kwa watu wanaofanya kazi na sio wavivu, na zamani pesa zilizagaa kwa sababu ya ubadhirifu wa mali za umma" pia kasema yeyote anayelalamika ni yule aliyekuwa anapata pesa kwa njia zisizo halali.

Katika hatua nyingine Mchungaji Lusekelo alimtaka Dr.Magufuli asisumbuke kubadili pesa za nchi kwani fedha zipo mtaani na maisha ni mazuri tu hakuna ugumu wowote.

Pia aliwataka waumini wake wasijaribu kushiriki katika maandamano yeyote yale na wala wasidanganyike kuchezea amani ya nchi kwa watu wenye uroho wa madaraka na kuwadanganya kuwa Magufuli kabana demokrasia wakati sio sahihi kabisa.

Mchungaji Lusekelo, alitoa mifano miwili ili kuwaelimisha waumini wake, wa kwanza ni nchi ya Gaboni mzee wa upako aliwaambia nchi hii imeharibiwa na watu wasiozidi elfu 3,000 kwa kuingia barabarani na kuanzisha maandamano na sasa nchi ile imevurugika.

Mfano mwingine katolea nchi ya Brazili, kuwa Taifa hili limevurugwa na watu wasiozidi elfu 10,000 baada ya kuingia barabarani na kuandamana na kusababisha machafuko na nchi kutotawalika.

Mzee wa upako alilaaani vikali oparesheni UKUTA iliyokuwa imetangazwa kufanyika tarehe moja September mwaka huu kwa kusema, ilisababisha Taifa kukosa watalii kuja kuangalia kupatwa kwa jua kule Mbeya kwa kuhofia machafuko nchini nakuwataka wapinzani wasirudie kitendo hiki.

Mwisho Mzee wa upako ametangaza kutumbua majipu mpaka kanisani na ikiwezekana kukata mguu wenye jipu ili jipu litoke na mtu aweze kuishi, baada ya hapo alimalizia kwa kuimba wimbo wa Tanzania.

Hongera sana mchungaji Lusekelo hakika umenena vyema.
Imeandaliwa na wenu,
MWITA NYARUKURURU

Ibada takatifu au ibada ya kitapeli?
 
anasema JPM asibadili pesa. inawezekana amesunda mahela mengi ya kitapeli sasa anahofia kubainika. halafu anaposema pesa zipo mtaani anajuaje wakati yeye anabugia tu sadaka za kondoo wa bwana ambao badala ya kuwa wamepotea yeye ndiye anawapoteza?
 
Mlemavu wa miguu (kilema) anamwambia utapona tu, na miguu yako na itakaa sawa kabisa kama wengine😀😀😀😀
 
Ni lazima aseme ivyo ili kurudisha fadhila ya kupewa barabara.
Huyu bwana angejikita katika kuhubiri injili.
 
Hivi Msigwa wa Iringa mjini (mb) ni mchungaji wa nini vile?
 
anasema JPM asibadili pesa. inawezekana amesunda mahela mengi ya kitapeli sasa anahofia kubainika. halafu anaposema pesa zipo mtaani anajuaje wakati yeye anabugia tu sadaka za kondoo wa bwana ambao badala ya kuwa wamepotea yeye ndiye anawapoteza?

Hapo ndio kaniudhi aise, sasa yeye anajuaje maisha ya watu...yeye kajifungia kanisani na wala hajui kinachoendelea mitaani...duh ipo kazi
 
Ahya! yaani licha ya kutumika kwa mbinu ya kijasusi hivyo bado watabe mmeinyaka?....loh! kama ni kweli Mkuu wewe noma sana.
Mbona inafahamika kitambo , unajua kosa kubwa tunalolifanya ni kuwafichia siri zao hawa wanafiki .
 
Back
Top Bottom