Mchumba wangu katolewa kizazi

Mchumba wangu katolewa kizazi

Poleni sana,kama anampenda kwa dhati waweza kumuoa na hasa kama lengo la kuoa si watoto,Kwa Mungu hakuna jambo gumu inaweza siku moja mkapata watoto.
 
Wewe ni wa imani gani?kama ni muislamu basi "msomeshe" huyo mchumba kuwa utaoa mke wa pili baadae ili upate mtoto(Mungu akipenda),ila hakikisha mmekubaliana hilo kabla hamjaowana otherwise ukijaoa huko mbele ya safari ni mtihani!
 
usimwache hayo ni mambo ya dunia zipo njia nyingi za kupata watoto natamani nikupata tuzungumze namna ya kupata mtoto na maisha yenu yakasonga mbele kama kawaida sumu ya mapenzi ni kali kuliko ya nyoka ukimwacha utampa mateso makubwa sana kwenye maisha yake.
 
Mwaweza mkalea mtoto yatima mkamfanya kama wenu mtakuwa mmepata thawabu kubwa sana,ila usimuache ataumia sana hujafa hujaumbika.
 
(alipata tatizo ulilosababisha wewe?)

Hapana wa mjibu wa madaktari,wanadai alikuwa na uvumbe katika mfuko wa uzazi kiasi cha kujenga uwezekano wa kupata cancer
 
Habari waungwana, naomba kusaidiwa kimawazo nifanye nini katika hili.

Nina mchumba wangu ambaye tumekuwa katika mahusiano kwa takribani miaka miwili na nusu, japo sijawahi kujitambulisha kwao mpango wa utambuzi ulikuwa ni mwezi huu wa November na mipango ilikuwa ishawafikia wazazi.

Hivi majuzi mchumba wangu aliugua gafla tumbo na baada ya vipimo alilazimika kufanyiwa upasuaji uliopelekea kuondoa mfuko wa uzazi ili kunusuru maisha yake.

Ukweli nimechanganyikiwa nini nifanye, hasa ikizingatiwa tunapendana sana.

Lakini nawaza je, ndo hatutapata familia yenye watoto kabisa kama tutaoana? Tafadhali hebu nijengeni kifikra.

Kama Ni Kweli Pole Sana Mkuu ILA Kama Wewe Ni Mwenye Imani TIMILIFU Na Siyo Ya KIPOPOMA Tafadhali Mpeleke Shemeji Yetu Kwa Watumishi Wa Mungu Wenye UPAKO Kwa Mfano Kwa Nabii Frola Na Nina Uhakika Huyo SUKARI Wako Atapona Na Kizazi Kitafanya Kazi Na UKIGEGEDA Tu Utazaa Nae MAPACHA 12!
 
Muoe huyo huyo na uoe mwingine wa kuzaa Dini inaruhusu
 
Pole sana ndugu yangu.

Sijaelewa kama hicho kizazi kimeondolewa completely au partially kwa maana kizazi cha mwanamke kinajumuisha sehemu mbali mbali, na mara nyingi tuna refer UTERUS, sasa kama ovary bado zipo still kunaweza kuwa na hope kama ukiwaona ma specialist kwa maana kama anauwezo wa kuzalisha MAYAI, basi yai lake linaweza kutolewa na likapandikizwa kwa mwanamke mwingine pamoja na mbegu zako au kwa njia ya tube kwa kitaalam wanaita IVF au In-Vitro Fertilization.
 
hakuna lisilowezekana mbele za Mungu .... so kama kweli unampenda inakubidi ukubaliane na hali... then Mungu sana, inaweza ikawa ni moja ya sababu ya kuwafanya ndugu, marafiki na jamaa kuamini kuwa Mungu yupo na anatenda miujiza pale mtakapozaa... Fanya hima ni mapito tu hayo Mungu atakufungulia njia
 
na wewe jitoe kizazi ili muwe wote hamna vizazi...mnakuwa mijoka ya kibisa mnatema tema mate tu kuuma hamuumi
 
daaaa inauma sana ...fanya lile litakalokupa amani rohonimwako
 
Duh! Kweli mtihan, ila nadhan ukimuoa atakuheshim sana, so cha kufanya tafuta mtoto wa kuzingiziwa fasta halafu mipango mingine iendelee
 
nakushauri usimwache kwamaana imani yako ndo itawapa faraja na kukaaa kwa amani.kwa mungu hakuna linaloshindikana kwa maana mkiamua kukaa pa1 mnaweza hata mkawachukua watoto ktk vtuo au wanaoishi ktk mazingira magumu na mkawalea kwa furaha kama watoto wenu maana nyote mnajua nini mnafanya!!!
 
  • Thanks
Reactions: awp
Back
Top Bottom