mchumba wangu ataongeza mke wa pili

mchumba wangu ataongeza mke wa pili

Yah, maana ukishaolewa nae basi umeenda upande wake, ameshaonyesha lengo na ninaamini atalitimiza.
Hata ukisaini MONOGAMY, kama akikiuka suluhu yako ni kuachika, sasa ya nn mfike mbali huko (pengine wakati huo una watoto) ili hali tatizo umeliona mapema!?
Olewa na mtu ambae hatakuweka njia panda

Kweli kabsa tanx
 
mi naona bora huyo jamaa ataamua kumtambulisha kwako
maana wengi wao siku hizi wanatamani nao iman yao ingewaruhusu lkn ndo hvyo tena
mke unaishia kuzungukwa bila we kujua mwisho wa siku anakuletea magonjwa ndani
bora huyo ambae anakuleletea mwenzio ili umtambue!

Hyo ngumu kumesa
 
Unaogopa kuvunja uchumba wakati wenzio wanavunja na ndoa kabisa kama wanaona hawaenjoy? Sasa ya nini kuingia huku unaumia. Ndoa unatakiwa ufurahie na kwa muda uliobaki ungekuwa unatamani tu huo muda ufike. Kimbilia kwa shehe mapema. Ipi bora ugharamike kwa muda wa mwezi mmoja kwa sababu ya kuvunj uchumba au ugharamike maisha yako kwa kuishi kwenye ndoa ambayo haufurahïi

Umenigusa sana
 
je niwahi kwa ostazi atakae funga ndo kutoa taarifa au nifanye nn?uke wenza siwezi
Ustaadh..!!!??
Fruitless.
Ye Usataadh ndo kakolea kwenye dini, wategemea utaambiwa nini?
Tena waweza kuta huyo ustaadh ana wake watatu, sasa hapo unafikiri atakuwa na msaada gani na wewe?
Na wazazi wako washapokea mahari, kwa jinsi unavosema kuwa taratibu zote tayari.
Licha ya hiyo ni waumini wa hiyo dini... watakuwa na msaada kwako?
Mtu pekee wa kukupa msaada Madam zero, ni wewe mwenyewe!​

  1. Kama uko tayari kuwa na ndoa ya za wake wengi (kumbuka baada ya huyo wa pili ataongeza tena, na tena...who knows?), basi kubali olewa uishi na mumeo na wapende wake wenza wako.​
  2. Kama hauko tayari kwa hilo, Madam zero, bado hujaolewa... ni uchumba tu. Hakuna talaka kwenye uchumba. Maisha ni yako, raha ni yako, tabu ni zako, wivu ni wako... si wazazi, si shehe wala yeyote atakaye feel maisha yako. FANYA UAMUZI.​
 
Last edited by a moderator:
Naumia sana.wiki mbili zijazo ntafunga ndoa na mchumba wangu lakini leo ameniambia kua baada ya mwaka kuisha ataongeza mke wa pili yaani tuwe wawili mm na mke mwenzangu mbaya zaidi et tutaishi nyumba mmoja !!!!mimi nitakua mke mkubwa lakin yule mwenzangu atakae letwa atakua mke wa pili yaani roho inaniuma sana hata kama imani ya dini inaruhusu hivo mm nashindwa kukubaliana nae?naombeni mchango wetu hapa nipo na mawazo ya kuvunja huu uchumba na nikiangalia taratibu zote za ndoa zimefanyika je nifanye nn?nikatae au nikubali?maana hili swala ameniambia baada ya kuvaa pete ya uchumba na family zote wanajua?je niwahi kwa ostazi atakae funga ndo kutoa taarifa au nifanye nn?uke wenza siwezi
Huyo mchumba wako atakua anakutania tu ingawa kweli sheria inasuhusu lakini kwa sasa hayupo serious..!! Kama kweli anakupenda basi endeleeni na mipango ya arusi wala usiwe na shaka, na akisema anataka kuongeza mwambie sawa kwavile dini inaruhusu..!! Kitakacho mfanya aongeze mke mwengine ni namna ambavyo utaishi nae! ukiitumikia kweli ndoa yako hataongeza kamwe..!!
 
Ustaadh..!!!??
Fruitless.
Ye Usataadh ndo kakolea kwenye dini, wategemea utaambiwa nini?
Tena waweza kuta huyo ustaadh ana wake watatu, sasa hapo unafikiri atakuwa na msaada gani na wewe?
Na wazazi wako washapokea mahari, kwa jinsi unavosema kuwa taratibu zote tayari.
Licha ya hiyo ni waumini wa hiyo dini... watakuwa na msaada kwako?
Mtu pekee wa kukupa msaada Madam zero, ni wewe mwenyewe!​

  1. Kama uko tayari kuwa na ndoa ya za wake wengi (kumbuka baada ya huyo wa pili ataongeza tena, na tena...who knows?), basi kubali olewa uishi na mumeo na wapende wake wenza wako.​
  2. Kama hauko tayari kwa hilo, Madam zero, bado hujaolewa... ni uchumba tu. Hakuna talaka kwenye uchumba. Maisha ni yako, raha ni yako, tabu ni zako, wivu ni wako... si wazazi, si shehe wala yeyote atakaye feel maisha yako. FANYA UAMUZI.​

Umemaliza kila kitu mkuu Sigma..sasa akili kichwani mwake.
 
kwenye ndoa ya ki islam mwanamke hana haki...na mafundisho wayajua sasa unatakaje hapa?

Si kweli maneno yako blogger! Ni haki gani ambayo mwanamke wa kiislam ananyimwa katika ndoa yake..?? Hebu toa mifano japo miwili kuitetea kauli yako..
 
Very simple.. She needs to be strong, she has to make a hard decision..!! I like your precise comment..
"Strength" ndo kila kitu.
Mental strength, ya kukabiliana na yatakanayo na maamuzi yake huyu mwali wetu Madam zero.
Challenge aliyo nayo ni kuwa,
  1. akimpiga chini huyu mchumba "honest" aliemwambia beforehand kuwa ataoa mke wa pili...
  2. Akampata mchumba mwingine ambaye "si-honest" asimwambie kuwa ataoa tena, na akaolewa nae, huyu mume akamwolea mwali wetu Madam zero mke wa pili mbele ya safari... unanpata hapo? .
Swali ni je... Utarudi tena hapa JF, utafanyaje mama?
Hili swala lina religious implications, na kwa msimamo wa Madam zero (mume wake yeye pekeyake), she is unlikely to find a happy end.
Only wishing for the best "UNLESS............................................................"
 
kwenye ndoa ya ki islam mwanamke hana haki...na mafundisho wayajua sasa unatakaje hapa?

sio kweli. Mwanamke wa kiislam ana haki sana ila km hujui uislam utaandika hivyo. Huyu anatakiwa afanye maamuzi ya kukubali au kukataa. Ni bora kuwa na wake wawili kuliko kuwa na nyumba ndogo mia. Ndio wakristo wengi walivyo na wanawake wa kikristo wanalalamika sana waume zao kuwa na malaya ila yanamalizwa na viongozi wao wa dini na pengine wanamegwa huko
 
Hapo mambo ya imani ya Dini tuu ndio jamaa atakapokushindia
 
Tatzo nampenda nikiachana nae nitaumia sana pia wanaume wapo lakin nitaumia
Ni bora ukaumia kwa muda mfupi kwa kummwaga huyo mchumba, kuliko kuumia kwa kuishi na mke mwenza kwa maisha yako yote yaliyobaki hapa duniani. Kama una masikio na usikie. Pole
 
Back
Top Bottom