Mchumba wangu ana madeni balaa

Mchumba wangu ana madeni balaa

amilyroley

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2015
Posts
621
Reaction score
1,200
Nina girlfriend nipo naye kwa miaka Tisa sasa. Nimeanza naye mahusiano akiwa na miaka 19. Ilikuwa mwaka 2006 mwezi wa tano Waziri Mkuu wa nchi hii akiwa Lowassa. Nampenda na ananipenda. Namuhudumia vzuri tu. Na tayari nimemchumbia. Zamani hakuwa na tabia za kukopa vitu na kubaki na madeni. Ila sasa imekuwa balaa.

Nilipoingia kwenya ajira nilianzia kazi ofisi zetu za Arusha yeye akabaki Dar na hapo ndipo alipobadili tabia ambayo hakuwa nayo mwanzo. Japo nilikiwa mbali hakuna kilichobadilika kwa kumjali kwa matumizi yake. Ila sijui tabia ya kukopa kaitoa wapi Na nilishamkataza na nikamuambia akiwa na shida ruksa kuniambia na analijua hilo. Ila anapenda tu kukopa.

Baadae nikahamia kikazi kurudi mjini DSM. Yaani kila njia tukipita japo ni ndani ya gari ataniambia hapa tusipite na tukipita usishushe kioo flani ataniaona. Nikimtaiti anasema ananidai nilikopa wigi.

Hii tabia inanishinda sasa. Anadaiwa hadi kwenye vibanda vya baga. Saluni nyingi haendi ameacha madeni. Maduka zaidi ya sita maeneo ya kwao mikocheni anadaiwa. Wanafunzi aliomaliza nao udsm mwaka huu karibia mashosti wake wote wanamdai. Nishafanya juhudi zote kumkataza na kuyalipia madeni yake ila anarudia na anakopa tena.

NIFANYEJE?
 
Miaka tisa uchumba? Mkuu hebu tuanzie hapo...

Huyo bint si anamshahara? Mwambie mwisho wa mwez huu alipe maden yake.

Anywai umuoeee sasa bwana miaka tisa duuu tangu kikwete aapishwe paka ameondoka...

Cc mito
 
Last edited by a moderator:
Amebakia kuwa mwizi

Dawa yake muache akibadilika urajua la sivyo atauza nyumba utakayojenga pia bila wewe kujua.

Hafai huyo labda ma maisha ya kuwa mke hayajui.
 
Kiongozi swala la madeni tuliweke kando kwanza, ni kwa nini unamhold binti wawatu miaka 9 bila kumuowa? yani utamu wote ule wewe umri wake akishachuja usichana ndio umpige chini halafu uowe mwingine? ndugu yangu utalogwa na wanawake wanawajuwa waganga kuliko unavyoweza kufikiri. shauri yako.
 
miaka tisa uchumba? huyo atakuwa ana frustation za kutojua msimamo wako ndio maana anakopa.

Turudi kwenye mada: are you sure anakopa au ana kautapeli ndani yake?
Umekaa nae chini na kujaribu kutafuta chanzo cha sababu?
Usimchoke ,kama unampenda fanya juu chini umrekebishe

Kikubwa MUOE
 
Mpe namba yake jamaa anaitwa mwekundu atalipa madeni yooote
 
Last edited by a moderator:
Samahan lkn! Hivi Dar kuna vibanda vya baga 'Drive thru kama Maccas, Kfc, roosters, subway. Nikija na mm mnipe address namiss sana huku sumbawanga hakuna
 
Kiongozi swala la madeni tuliweke kando kwanza, ni kwa nini unamhold binti wawatu miaka 9 bila kumuowa? yani utamu wote ule wewe umri wake akishachuja usichana ndio umpige chini halafu uowe mwingine? ndugu yangu utalogwa na wanawake wanawajuwa waganga kuliko unavyoweza kufikiri. shauri yako.

Ha ha ha...kuna jamaa mmoja mdau wa Bagamoyo aliniambia kuna waganga wawili Bagamoyo wateja wao zaidi ya 90% ni wanawake. Na matatizo yao ni ishu za mahusiano!!!

Yaani tusipokuwa makini tutalishwa mpaka kinyesi
 
Miaka tisa uchumba? Mkuu hebu tuanzie hapo...

Huyo bint si anamshahara? Mwambie mwisho wa mwez huu alipe maden yake.

Anywai umuoeee sasa bwana miaka tisa duuu tangu kikwete aapishwe paka ameondoka...

Cc mito

Duh, huyu naye kiboko kama wewe tu mkuu, uchumba miaka tisaaaaaa!!! hivi mnaogopa nini kuoa mkuu sumbai? tujuzeni na bro mkubwa Eli79 tunaweza kuwapa ushauri

cc Heaven Sent njoo uone huku uchumba sugu mwingine
 
Last edited by a moderator:
Miaka tisa uchumba? Mkuu hebu tuanzie hapo...

Huyo bint si anamshahara? Mwambie mwisho wa mwez huu alipe maden yake.

Anywai umuoeee sasa bwana miaka tisa duuu tangu kikwete aapishwe paka ameondoka...

Cc mito
Teh teh..Na jamaa wala haonyeshi kama ana mpango wa kuoa karibuni..

Huyu jamaa anaweza akawa anashikilia record ya kuwa na mahusiano ya muda mrefu hapa MMU
 
Muoe binti wa watu. bila shaka anaumia sana,, miaka tisa khaaaaaaaaaaaa. tangu 2006?
 
Nina girlfriend nipo naye kwa miaka Tisa sasa. Nampenda ananipenda. Namuhudumia vzuri tu. Zamani hakuwa na tabia za kukopa vitu na kubaki na madeni. Ila sasa imekuwa balaa. Nilipoingia kwenya ajira nilianzia kazi ofisi zetu za Arusha yeye akabaki Dar na hapo ndipo alipobadili tabia ambayo hakuwa nayo mwanzo. Japo nilikiwa mbali hakuna kilichobadilika kwa kumjali kwa matumizi yake. Ila sijui tabia ya kukopa kaitoa wapi Na nilishamkataza na nikamuambia akiwa na shida ruksa kuniambia na analijua hilo. Ila anapenda tu kukopa. Baadae nikahamia kikazi kurudi mjini DSM. Yaani kila njia tukipita japo ni ndani ya gari ataniambia hapa tusipite na tukipita usishushe kioo flani ataniaona. Nikimtaiti anasema ananidai nilikopa wigi. Hii tabia inanishinda sasa. Anadaiwa had kwenye vibanda vya baga. Saluni nyingi haendi ameacha madeni. Maduka zaidi ya sita maeneo ya kwao mikocheni anadaiwa. Wanafunzi aliomaliza nao udsm mwaka huu karibia mashosti wake wote wanamdai. Nishafanya juhudi zote kumkataza na kuyalipia madeni yake ila anarudia na anakopa tena. NIFANYEJE?

Lets assume...
Kamaliza chuo akiwa na miaka 23 (kozi ya miaka 3 UDSM)..
Miaka tisa ya uchumba: 23-9=14 years!!

Ina maana ulianza nae akiwa na miaka 14????
 
Yaani nimekujibu kimoyomoyo.
Hadi tandale kuna burgers
Samahan lkn! Hivi Dar kuna vibanda vya baga 'Drive thru kama Maccas, Kfc, roosters, subway. Nikija na mm mnipe address namiss sana huku sumbawanga hakuna
 
Kwenye maombi na kwa waganga ndio kumejaa wanawake. Mmetufanyavso desperate, kuna wadada na elimu dunia kibao wanatapeliwa hadi unashangaa!
Ha ha ha...kuna jamaa mmoja mdau wa Bagamoyo aliniambia kuna waganga wawili Bagamoyo wateja wao zaidi ya 90% ni wanawake. Na matatizo yao ni ishu za mahusiano!!!

Yaani tusipokuwa makini tutalishwa mpaka kinyesi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom