Mchumba wangu ana karama ya unabii, ananitisha!

Mchumba wangu ana karama ya unabii, ananitisha!

Mteja wako yeye kafikwa na majanga gani?.
Swali zuri.

Yeye alikuwa amefunga, si unajua tena mwezi huu; so hakunywa wala kula chochote.

Jamaa tuliwakamata na nimewatoa kwa dhamana. Wamekiri kosa. Naendelea kutafakari niwafanye nini. Kesi sitaki, ila nataka wapate funzo in a hard way.
 
Yaani umesema ulienda kupata kinywaji na watu ambao ndo washindani wako kwenye kesi. ulifata ule msemo wa mchawi mpe mwanao amlee.
dah!

Kitu ambacho wengi hamjui ni kwamba kesi sio vita mkuu.

Ni vile tu hawa ndio walitaka kufanya vita baada ya kuona nimewavuruga Mahakamani.
 
Binafsi naogopa Sana watu waonaji( watabiri)
Yaani unakuta mtu anakutabiria kwamba utakutwa na Jambo zito Sasa badala ya kukupa muongozo jinsi ya kuliepusha lisitokee yeye anajikalia tu kimya.
Very pathetic!
akikuambia ameona kuwa safari yako ya kwenda Tanga Ina vita na maumivu mengi maana yake USIENDE TANGA, yaani ahirisha!
 
binafsi nimekupata. zaidi sana umenikumbusha neno la kwenye kitabu cha Marko "... hata mkinywa kitu cha kuwafisha hakitawadhuru".

TUSIACHE KUMTEGEMEA NA KUMWAMINI MUNGU
Na hili ndio andiko mchumba wangu amenipa baada ya kutoka hospitalini.

Ubarikiwe sana mkuu.
 
Wewe ni wakili mpumbavu. Huyo mchumba wako ukimwoa atampenda "baba yake wa kiroho" kuliko wewe. Halafu acha tabia ya kupenda kufakamia kila kitu.. huo ni ulafi.
 
kama umeokoka, Mungu akubariki. kwa waliookoka hiyo ni jambo la kawaida, Mungu hua anagawa vipawa, na Roho Mtakatifu huwa anaongea kwa namna mbalimbali, anaongea na huyo dada pia. binafsi wakati niko misri, mke wangu alikuwa mtu wa imani sana, hadi leo ni mtu wa imani. ilikuwa hata nikicheat, anajua, anaonyeshwa kwenye ndoto. kuna siku nimesafiri nikafanya ujinga, niliporudi akaniambia ameota ndoto ambayo anaona ni ya kimungu, akaeleza mazingira yooote sawasawa na niliyokuwa, na jinsi mwanamke yule alivyonilaghai, hadi kiasi cha pesa alfu hamsini alichochukua.

nilipokuja kuokoka, hadi leo hii, kama kuna jambo baya lipo mbele yangu, huwa nalijua, nikilala usingizi hasa mida ile ya asubuhi saa kumi na moja au kumi, huwa naoteshwa au naona kama maono kitu kilicho mbele yangu, aidha direct kabisa au indirectly kuwa na uzito kwamba kuna jambo baya limetegwa au linanikaribia, kazi sasa huwa ni kulisambaratisha kwenye ulimwengu wa roho, kama sitafanya hivyo, huwa linatokea kweli ndani ya wiki mbili, na hata nikisambaratisha huwa kufeli kwa hilo jambo kunaonekana. kwa kifupi, Mungu huwa anaongea, na akiongea kama wewe ni mtu wa Mungu utajua huyu ni Mungu na huyu sio MUngu. kuna ndoto za ugali tu umeshiba, ndoto za mambo uliyofikiria mchana au yaliyojaa kichwani mwako, ila kuna ndoto za Mungu kabisa, anakuonyesha, na ziko tofauti, zile za Kimungu ni kama mhuri umegongwa, zina upako wake haufutiki, mimi kuna ndoto nilioteshwa mwaka 2000 nikionyeshwa na kundi la malaika wakiimba wimbo, hadi leo huwa siisahau hadi huo wimbo upo kichwani hadi leo.

Yohana 10:27 inasema, Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele, wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.

Yoel 2:28 Hata itakuwa baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili na wana wenu waume kw awake watatabiri na wazee wenu wataota ndoto na vinana wenu wataona maono.

Yohana 10:5 Yesu alipokuwa akiongelea kondoo wake alisema, Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.

kwa ninyi ambao hamjaokoka, hayo ndiyo marupurupu ya wokovu (mojawapo tu, yapo mengi), wakati wengine wanahangaika kupambana kimwili sisi Mungu ameshatuonyesha rohoni nini kinakuja, tunapiga magoti tunasambaratisha kwa Jina la Yesu, wewe huku nje unapambana na sisi kimwili au kwa kutumia wanadamu, utashindwa na tunajua mwisho wako hata kabla haujaufikia. vita vyetu ni vya rohoni. pia Mungu huwa anaongea nasi kwa maono na ndoto, just to mention a few.

Yesu anasema, kondoo wake wanaijua sauti yake, wanamfahamu, wapo wachungaji wengi wana discourage kwamba ndoto huwa sio za kimungu, NO, zipo za kimwili na za kishetani, ila zipo za Mungu kabisa, na wale walio na Mungu moyoni wataijua sauti ya Mungu, hautakuwa na haja kwenda kuuliza kwa mtu tafsiri yake or whether hii ni ndoto ya Mungu au sio? hautauliza kwasababu jambo la kimunguni dhahiri na lina amani ya Kristo na utaona kama linasema moyoni kabisa kwa ule utamu wa Roho Mtakatifu, automatically utatafsiriwa na utaijua kuwa hii ni sauti ya Mungu na hii ni sauti/ndoto ya adui. ziko tofauti kabisa. ndio maana Yesu alisema kondoo wake wanaijua sauti yake, akiongea Yesu utajua huyu ni Yesu kama wewe ni kondoo wake, na akiongea mwizi utajua huyu sio Yesu kama wewe ni kondoo wa Yesu.
ubarikiwe sana mtumishi wa Bwana. AMEN.
 
Ni kweli mkuu, uko sahihi. Tatizo mimi nikachukulia kawaida. Ila nimejifunza.
Mimi kwa mke wangu ni kawaida sasa. vijidada vinavyojipendekeza (hata kama hajaviona kwa macho ya damu na nyama) kwangu huwa anavijua na kunionya kabla ya kufika mbali.

jambo hili limenisaidia sana. Ninamshukuru Mungu kwa kunipatia mke wa namna hii.
 
Wakuu habarini za wakati huu...

Niliwahi kuleta Uzi humu kuhusu mchumba wangu ambaye ni Mcha Mungu, bikira, mpole, mkarimu, mzuri n.k.

Nimegundua kwamba huyu mwanamke ana karama ya unabii pia (muonaji). Zamani manabii waliitwa waonaji.

Kwanini nimefikia hii conclusion? Mjomba wangu alikuwa anaumwa, yaani kaka yake mama yangu. Siku Moja kabla ya kifo cha mjomba wangu, mchumba wangu akanipigia simu kunimbia anaona huzuni KUBWA Kwa mama yangu, kesho yake mjomba akafariki, kweli mama aliumia sana!

Mimi ni Wakili, nilikuwa na kesi Tanga Jana, kabla sijaondoka akanipigia simu kuniambia anaona vita KUBWA kwenye hiyo kesi, na ananiona Niko hospitalini! Baada ya kesi, ule upande wa pili wakaniomba tuonane nje ya Mahakama nikiwa na mteja wangu ili tufute kesi tuyazungumze, kweli tukaenda kuonana nao, nikawekewa sumu kwenye kinywaji changu, nikapelekwa hospitalini kweli na nikalazwa, Sasa hivi ndio wameni-discharge.

Hayo ni machache tu kati ya mengi. Ama kweli, ukimtanguliza MUNGU mbele HUWEZI kuikataa taasisi ya NDOA. NDOA ni baraka.

Huyu nikimuoa inabidi niwe makini sana

Muwe na jioni njema.
Huyo usimnyandue ukimnyandua tu unabii wote kwisha
 
anaeza pia akawa na pepo la utambuzi cc Mshanajr
nina baba yangu mdogo yeye ni mganga,anaonyeshwaga mikasa akiwa amelala. kama kuna jambo baya linatokea hasa kwa watu anaowafahamu anaonyeshwa
 
Wakuu habarini za wakati huu...

Niliwahi kuleta Uzi humu kuhusu mchumba wangu ambaye ni Mcha Mungu, bikira, mpole, mkarimu, mzuri n.k.

Nimegundua kwamba huyu mwanamke ana karama ya unabii pia (muonaji). Zamani manabii waliitwa waonaji.

Kwanini nimefikia hii conclusion? Mjomba wangu alikuwa anaumwa, yaani kaka yake mama yangu. Siku Moja kabla ya kifo cha mjomba wangu, mchumba wangu akanipigia simu kunimbia anaona huzuni KUBWA Kwa mama yangu, kesho yake mjomba akafariki, kweli mama aliumia sana!

Mimi ni Wakili, nilikuwa na kesi Tanga Jana, kabla sijaondoka akanipigia simu kuniambia anaona vita KUBWA kwenye hiyo kesi, na ananiona Niko hospitalini! Baada ya kesi, ule upande wa pili wakaniomba tuonane nje ya Mahakama nikiwa na mteja wangu ili tufute kesi tuyazungumze, kweli tukaenda kuonana nao, nikawekewa sumu kwenye kinywaji changu, nikapelekwa hospitalini kweli na nikalazwa, Sasa hivi ndio wameni-discharge.

Hayo ni machache tu kati ya mengi. Ama kweli, ukimtanguliza MUNGU mbele HUWEZI kuikataa taasisi ya NDOA. NDOA ni baraka.

Huyu nikimuoa inabidi niwe makini sana

Muwe na jioni njema.

Unaporwa wewe na Mwanamke keshajua ujinga wako, anaweza kuwa mshirikina
 
Aisee huyo ni GUARDIAN ANGEL, hutakiwi kumuogopa kabisa maana once mkianza kuishi pamoja kama familia, utawajua mpaka marafiki wanafiki ambao kwasasa wewe unahisi ni watu wako wa karibu sana kumbe sio.

Nasema hivi kwasababu mimi wife wangu ni wa aina hii, baada ya kuanza kuishi nae rasmi nimegundua vitu vingi ambavyo binafsi nisingevijua kabisa.

Na amekuwa msaada sana maana kuna muda unaweza ukajikuta life linakuwa tight sana na mishe zote zinakwama kumbe wanaokwamisha ni washikaji zako wa karibu sana na huwezi hata kuwafikiria.

Hivyo wife wa aina hii ni rahisi sana kukuambia nini kinaendelea na hatua gani ufanye au watu gani unatakiwa uachane nao kabisa.

Maana kama adui yako ni rafiki yako wa karibu na wewe hujui lolote lile. Kutoboa kwenye maisha ni ngumu sana kwasababu unamuamini na unamshirikisha mambo yako mengi sana kumbe mwenzio anaenda kukuharibia bila hata huruma wala sababu ya msingi.

Kuoa mke wa aina hiyo kuna Advantages zake, lakini pia haimaanishi kwamba ukioa mke ambaye sio muonaji maisha hayawezi kwenda, yataenda tu kama wote mtamtegema MUNGU kwa kila jambo.

MAONI YANGU NI HAYO TU.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom