Usishindwe mkuu [emoji28]
Unaweza kumtetea vizuri tu. Katiba inasema kila mtu ana haki ya kupata utetezi, no matter amefanya Kwa kukusudia au bila kukusudia.
Sasa kuna mambo mawili kwenye swali lako. Kuna yule amefanya kwa kukusudia kweli (murder), na anataka afanye confession (akiri) Mahakamani, ili kwenye maombolezo, wewe Wakili umuombee apunguziwe adhabu kwasababu amekiri na anajuta alichofanya, kwa maana nyingine hajaisumbua Mahakama hivyo imuhurumie impe adhabu ndogo.
Jambo la pili ni la yule aliyefanya kwa kukusudia kweli na anataka ufanye linalowezekana umtetee aonekana hajafanya kwa kukusudia (manslaughter). Hapa pia unaweza kumchomoa kwa kuchagua zile "defences to criminal liability' ambayo itafiti kwenye circumstance ya kesi yake. Kwa mfano kuna 'provocation'; yaani aliua kweli, ila ni baada ya kumfumania mkewe akifanywa na mwanaume mwingine kwenye kitanda chao cha ndoa, hivyo akawa provoked akajikuta hasira imempanda, ameua (kumbe wala hakuwa provoked, kwasababu baada ya kumfumania mkewe alimketisha mgoni wake, akampiga sana, hasira zikapoa, na akamwambia kabisa nakuua leo [emoji28], so alijipanga, haikuwa hasira tena).
Mkuu, Wanasheria tunafundishwa tusiipotoshe Mahakama, ila kinachofanyika kwenye scenario ya pili ni kuipotosha Mahakama, kwasababu waliofanya kwa kusudi ndio walipaji wazuri sana wa fee ya Wakili [emoji3]. Mfano mzuri ni kesi ya mke wa Bilionea Msuya. Hii kazi inabidi uwe na Mungu kweli ndio uifanye kwa weledi. Vinginevyo, manung'uniko ya watu unaodhulumu haki zao hayatakuacha salama.