Wazazi wamkataa mchumba wangu kisa mahari ni ndogo

Apr 11, 2022
29
75
Habari zenu wana JF,

Bila kuwachosha naenda moja kwa moja kwenye point. Nilikuwa na mchumba wangu tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa. Kwa hiyo mwaka huu huyo kaka nilimwambia aje home kujitambulisha, akasema haina shida.

Niliwataarifu wazazi wangu tarehe ambayo aliniambia anakuja wakasema aje kwetu.

Kama kawaida huyo kaka alikuja na mshenga wake pamoja na mjomba wake. Baba yangu alialika wenzake kama 6 hivi ili kujadiliana mahari. Kwa kweli ilikuwa tafrani, kwasababu baba yangu mzazi alishauriana na wenzake mahali iwe 10.5M kitu ambacho kilinishangaza sana.

Mjomba wake akasema hiyo hela hawana kwani hawanunui kiwanja. Baadae mjomba akasema wao wanaweza toa 2.5M baba akasema iongezeke japo 3M kwa shingo upande, kwamba hataki mahari ndogo akidai watakuja wengine.

Jioni yake akaniita mimi na mama akaanza kunifokea. Akaniambia mimi namdhalilisha kuleta mtu masikini na haeleweki kwa hiyo niachane naye, na nisipoachana naye mimi nitakuwa siyo mtoto wake na nikikubali kuolewa naye nisije kukanyaga kwake mpaka kaburi lake nisije kulisogelea.

Hakuishia hapo akaanza kunilinganisha na kabati ambalo anadai limenizidi, kwamba yeye alilinunua kwa bei kubwa kuliko mahali yangu. Nililia sana maana hata mama yangu alikuwa upande wa baba kwa hiyo sikuwa na support yoyote.

Aibu naipata mimi mtaani, naogopa hata kutoka kwenda sehemu kwa ajili ya wazazi wangu kunisambazia doa kubwa.

Naombeni ushauri katika huu wakati mgumu, kushauriwa kumuacha mtu uliyependana naye mkaendana siyo kitu rahisi. Japo huyo kaka hajaonesha dalili zozote za kuniacha, anawasiliana na mimi kama kawaida.

Ahsanteni sana. Napitia maoni yenu, wote nawakaribisha.
 
Pole sana kwa hilo linalokusibu, kama utakuwa tayari kuiacha familia yako na kumfuata mumeo, naomba mkae chini na kijana mpeane mikakati ya kupata hiyo 3M, sioni kama ni issue kubwa

Lakini kama utakua tayari kuishi mahusiano yako kwa kuongozwa na ndugu au familia yako nakuomba sana usiolewe ubaki ivoivo, maana hautawahi kufanikiwa kwa upande wa ndoa, inaonekana hata akipatikana mwenye kipato, atahamishiwa majukumu yote ya nyumbani kwenu, yaani ndoa itakua ni kama NGO inayosaidia kaya masikini.

Mwisho utaachika hata mara tisa kuja kusettle tayari umri wako ushakutupa mkono
 
Habari zenu wana JF,

Bila kuwachosha naenda moja kwa moja kwenye point. Nilikuwa na mchumba wangu tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa. Kwa hiyo mwaka huu huyo kaka nilimwambia aje home kujitambulisha, akasema haina shida.

Niliwataarifu wazazi wangu tarehe ambayo aliniambia anakuja wakasema aje kwetu.
Mwambie aongeze mahari, watu wanapamba na umaskini wewe unaongeza maskini kwenye ukoo ulitaka wakuchekele?
 
Ni umasikini Tu, Narudia Tena ni umasikini wa familia yako na ushamba wa Mzee wako.

Nafahamu kuwa huyo ni Baba.
Yeye ni mzazi, Na mzazi hakosei japo kwa hili amekosea mno.

Unapopishana Jambo na mzazi ni vyema kuwatumia wazee WA kidini ambao wamezidi mzazi kiumri uende uongee nao ili wamuite Mzee kumuweka sawa.

Mahari Haina maana yoyote kwa watu wenye Nia ya kufunga ndoa ili kuishi pamoja.

Machoni pa Mungu Baba yako ni mkosefu mno, maana anaweka vikwazo kwa Jambo ambalo Mungu anataka kulibaliki.

Mahari sio biashara, Mahari sio mtaji. Huwezi kuthaminisha mwili WA mtu Kwa milioni 10.

Ukweli ni kwamba Mzee amekosea Sana, Na ili Mzee ajue kosa lake unapaswa kuwashirikisha watu ambao Mzee anawaheshimu Sana.

Naami penye Nia Pana njia. Bado nafasi unayo.
 
🤔🤔🤔

Yeye baba yako alimuoa mama yako kwa mahari ya thamani gani miaka hiyo?

Lengo haswa la hiyo million ni ili apate pesa ya kufanya mambo yake?
Au ni kupima uwezo wa mwanaume anayekuoa kama ana uwezo wa kukukutunza??
Au ni kumkataa huyo mwanaume kuoa kwenye familia yake???

Kuna wazazi wengine wanakataa watoto wao wasiolewe kwa sababu zao binafsi kisingizio kikiwa mahari, wengine wanakataa watoto wao wasiolewe kwa mwanaume wanayeona hafai kwa kumlima kiasi kikubwa cha mahari

Ila wewe usiwe na haraka, mwisho wa siku kama mwanaume anakupenda kweli kweli hakuachi! Atafanya kama yako alivyokubali kadhia ya miaka 14 mradi tuu Raheli awe mke wake
 
Tafuta pesa nunua vitu mchukue mchumba wako nendeni kanisani mkafunge ndoa wawili na mashahid watatu jipelekeni honeymoon.

Hyo pesa ya mahali nunueni vitu ndani na chakula muanze maisha na ww tafuta Kazi fanya. Furaha ailetwi na baba yako na mama ako furaha inaletwa na ww jifanye kua furaha na sio laana
 
Kigezo namba moja kuwa wanawake hawana akili timamu ni kukubali kununulika kwa kigezo cha mahari na huku wana furahia hicho kitendo.

Mahari ni biashara ya utumwa ya kununua watu, dunia inapaswa kupigia kelele huu ushenzi wa mahari unao endelea mpaka sasa karne hii ya 21.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom