Mchumba wangu ana karama ya unabii, ananitisha!

Mchumba wangu ana karama ya unabii, ananitisha!

Binafsi naogopa Sana watu waonaji( watabiri)
Yaani unakuta mtu anakutabiria kwamba utakutwa na Jambo zito Sasa badala ya kukupa muongozo jinsi ya kuliepusha lisitokee yeye anajikalia tu kimya.
Very pathetic!
Hapo itakuwa yeye mwenyewe anakuwa hajui hilo jambo hasa ni lipi ndio maana anakuwa hawezi kukupa muongozo wa kujiepusha nalo, ila kama maono yake ameona ajali na wewe una mpango wa kusafiri hapo atakwambia usisafiri.
 
Wakuu habarini za wakati huu...

Niliwahi kuleta Uzi humu kuhusu mchumba wangu ambaye ni Mcha Mungu, bikira, mpole, mkarimu, mzuri n.k.

Nimegundua kwamba huyu mwanamke ana karama ya unabii pia (muonaji). Zamani manabii waliitwa waonaji.

Kwanini nimefikia hii conclusion? Mjomba wangu alikuwa anaumwa, yaani kaka yake mama yangu. Siku Moja kabla ya kifo cha mjomba wangu, mchumba wangu akanipigia simu kunimbia anaona huzuni KUBWA Kwa mama yangu, kesho yake mjomba akafariki, kweli mama aliumia sana!

Mimi ni Wakili, nilikuwa na kesi Tanga Jana, kabla sijaondoka akanipigia simu kuniambia anaona vita KUBWA kwenye hiyo kesi, na ananiona Niko hospitalini! Baada ya kesi, ule upande wa pili wakaniomba tuonane nje ya Mahakama nikiwa na mteja wangu ili tufute kesi tuyazungumze, kweli tukaenda kuonana nao, nikawekewa sumu kwenye kinywaji changu, nikapelekwa hospitalini kweli na nikalazwa, Sasa hivi ndio wameni-discharge.

Hayo ni machache tu kati ya mengi. Ama kweli, ukimtanguliza MUNGU mbele HUWEZI kuikataa taasisi ya NDOA. NDOA ni baraka.

Huyu nikimuoa inabidi niwe makini sana [emoji28]

Muwe na jioni njema.
Fungueni kanisa, mke wako ni mgodi unaotembea
 
Wakili wa hovyo kabisa(kwa sauti ya mwinjaku)[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
kama umeokoka, Mungu akubariki. kwa waliookoka hiyo ni jambo la kawaida, Mungu hua anagawa vipawa, na Roho Mtakatifu huwa anaongea kwa namna mbalimbali, anaongea na huyo dada pia. binafsi wakati niko misri, mke wangu alikuwa mtu wa imani sana, hadi leo ni mtu wa imani. ilikuwa hata nikicheat, anajua, anaonyeshwa kwenye ndoto. kuna siku nimesafiri nikafanya ujinga, niliporudi akaniambia ameota ndoto ambayo anaona ni ya kimungu, akaeleza mazingira yooote sawasawa na niliyokuwa, na jinsi mwanamke yule alivyonilaghai, hadi kiasi cha pesa alfu hamsini alichochukua.

nilipokuja kuokoka, hadi leo hii, kama kuna jambo baya lipo mbele yangu, huwa nalijua, nikilala usingizi hasa mida ile ya asubuhi saa kumi na moja au kumi, huwa naoteshwa au naona kama maono kitu kilicho mbele yangu, aidha direct kabisa au indirectly kuwa na uzito kwamba kuna jambo baya limetegwa au linanikaribia, kazi sasa huwa ni kulisambaratisha kwenye ulimwengu wa roho, kama sitafanya hivyo, huwa linatokea kweli ndani ya wiki mbili, na hata nikisambaratisha huwa kufeli kwa hilo jambo kunaonekana. kwa kifupi, Mungu huwa anaongea, na akiongea kama wewe ni mtu wa Mungu utajua huyu ni Mungu na huyu sio MUngu. kuna ndoto za ugali tu umeshiba, ndoto za mambo uliyofikiria mchana au yaliyojaa kichwani mwako, ila kuna ndoto za Mungu kabisa, anakuonyesha, na ziko tofauti, zile za Kimungu ni kama mhuri umegongwa, zina upako wake haufutiki, mimi kuna ndoto nilioteshwa mwaka 2000 nikionyeshwa na kundi la malaika wakiimba wimbo, hadi leo huwa siisahau hadi huo wimbo upo kichwani hadi leo.

Yohana 10:27 inasema, Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele, wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.

Yoel 2:28 Hata itakuwa baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili na wana wenu waume kw awake watatabiri na wazee wenu wataota ndoto na vinana wenu wataona maono.

Yohana 10:5 Yesu alipokuwa akiongelea kondoo wake alisema, Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.

kwa ninyi ambao hamjaokoka, hayo ndiyo marupurupu ya wokovu (mojawapo tu, yapo mengi), wakati wengine wanahangaika kupambana kimwili sisi Mungu ameshatuonyesha rohoni nini kinakuja, tunapiga magoti tunasambaratisha kwa Jina la Yesu, wewe huku nje unapambana na sisi kimwili au kwa kutumia wanadamu, utashindwa na tunajua mwisho wako hata kabla haujaufikia. vita vyetu ni vya rohoni. pia Mungu huwa anaongea nasi kwa maono na ndoto, just to mention a few.

Yesu anasema, kondoo wake wanaijua sauti yake, wanamfahamu, wapo wachungaji wengi wana discourage kwamba ndoto huwa sio za kimungu, NO, zipo za kimwili na za kishetani, ila zipo za Mungu kabisa, na wale walio na Mungu moyoni wataijua sauti ya Mungu, hautakuwa na haja kwenda kuuliza kwa mtu tafsiri yake or whether hii ni ndoto ya Mungu au sio? hautauliza kwasababu jambo la kimunguni dhahiri na lina amani ya Kristo na utaona kama linasema moyoni kabisa kwa ule utamu wa Roho Mtakatifu, automatically utatafsiriwa na utaijua kuwa hii ni sauti ya Mungu na hii ni sauti/ndoto ya adui. ziko tofauti kabisa. ndio maana Yesu alisema kondoo wake wanaijua sauti yake, akiongea Yesu utajua huyu ni Yesu kama wewe ni kondoo wake, na akiongea mwizi utajua huyu sio Yesu kama wewe ni kondoo wa Yesu.
Mkuu, asante sana kwa mawasilisho haya, umenibariki mno.

Umeeleza vizuri, kwa hatua. Kila mwenye macho na asome!

Mungu azidi kukubariki na kukuzidisha.
 
Kwa mawakili kama hawa wanaoamini unabii, safari yetu ndefu.

Wakili kama huyu anaweza kukupa ushauri wa kisheria kwa sababu mchumba wake ana karama ya unabii kamuambia atoe ushauri huo.
"Safari yetu", wewe na nani?

Kwa comment yako ni dhahiri kwamba mimi na wewe tunasafiri kwenye ulimwengu tofauti. Siwezi kusafiri na wewe kwenye ulimwengu mmoja, kwahiyo kama ni kuchelewa utachelewa wewe, usinilishe maneno mdomoni mkuu.

Otherwise, haya ni mawazo yako, na hayanabudi kuheshimiwa, ingawa huu sio uhalisia wangu when it comes to my profession.
 
Wengi sana huwa tunataarifiwa hayo kupitia ndoto ama fikra, tatizo letu huwa tunadharau. Ni mambo ya kawaida kupashana habari kati yako na roho kujua yajayo kukuhusu wewe katika ulimwengu wa roho.

Kujua hayo si unabii.
Umeeleweka vizuri sana mkuu.
 
Ila hakuona kama mchumba wake atanyweshwa sumu.
Kwenye karama ya unabii, au neno la hekima au la kinabii, kuna baadhi ya mambo inaweza ikatokea unafichwa na Mungu nyakati fulani, kwasababu anazozijua Mungu mwenyewe. Kwahiyo Mungu anakuwa hakufunulii kila kitu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom