Mchumba ninayekaribia kumuoa simuelewi

Hawa watu wa facebook,movie,whatsapp,bbm na chat zingine sijui huko mbele sisi ambao hatujaoa itakuwaje. Naona kama ndoa za mkataba zinanukia hivi kwani sikihizi watoto wanaojiita wamjini ni wavivu acha mi naishi nao taabu kweli yaani unaweza ondoka mtu yuko kwenye tv ni seties mwanzo mwisho hii dunia yaani najionea huruma kwanini nilizaliwa miaka ya 1990 bora hata ingekuwa 1970 maana hizi internet zisingesumbua sana.
Broo kwa hapo ongea nae ili apretend kufanya ukimwoa sahau. Dalili ya mvua ni mawingu na panapofuka moshi jua moto unawaka hizi ni dalili za ugonjwa
 
Kwa sasa hatuishi wote maana tuko kwenye michakato ya ndoa lakini mara kadhaa anakuja na kukaa siku mbili tatu.

Kusema ukweli mimi nafanya almost vitu vyote, kwa mfano nina uhakika hajawahi kuosha vyombo!! Tukishakula(hata kama ni chips) ataacha sahani chafu mezani na kukaa sebuleni moviez. Either mimi nitoe na kupeleka kwenye sink au na mimi niache.

Mara nyingi napenda kukaa zangu chumbani au kwenye computer tu maana ananikera.

khaaaaaaa hata kutoa sahani?

Kaka hapana, kimbiaaaaaaa, hakufai huyo
 
Mwambia ukweli vitu vinavyokukera kabla hamjaingia kwenye ndoa

Ili ajue kama yuko tayari
 
ndio hizi nyumba unaingia unashindwa hata kuomba maji ya kunywa. Yaani ukiomba glass inatolewa kwenye kabati bila kufutwa wala nini, alafu ukute haikuoshwa vizuri, glass ukiisogeza kinywani inatoa harufu ya mayai mabichi.....mbona kiu itakuishia au utatapika kabisa.
mleta mada, nakushauri umuepuke huyo binti, especially unaonekana unakerwa sana na uchafu na uvivu. sasa ivi unaweza mvumilia sababu mapenzi bado motomoto, but trust me, marriage is more than that
 
Naomba ushauri wenu. Nina mchumba wangu tumekaa muda mrefu kama miaka 5 hivi. Sasa tumeona ni muda muafaka wa kuoana. Kipindi kirefu cha uhusiano wetu hatukuwa tunaishi pamoja as yeye alikuwa anasoma mkoa mwingine nami mwingine. Lakini hii haikupunguza mapenzi yetu maana tulikuwa tunawasiliana na kutembeleana mara kwa mara.

Sasa alimaliza chuo na kuanza kazi, na mimi pia nina kwangu. Tukawa tuko close zaidi na siku moja moja tunakaa pamoja nyumbani. Hili kufanya mambo yaende kwa heshima, tukafikia hatua ya kutambulishana kwa wazazi rasmi na kuanza kujipanga kwa ajili ya mahari na ndoa

Kuna tabia ambazo nimezigundua zinanikera na ninaomba ushauri.

1. Huyu binti ni mvivu
Anapenda kukaa kuangalia moviez tu. Moviez, kuchat thats it. Nyumba chafu nasafisha mwenyewe. Kila kitu kipo ndani(jiko, chakula), hataki kupika eti mpaka awe kwenye mood kwahiyo tunaishia kula chips. Nguo zangu chafu(hata za kwake) kufua ugomvi.

2. Kisirani
Mtu wa visirani, kujibu, kununa.

Sasa tunaelekea kwenye mahari lakini kichwa changu kinawaka moto. Hivi tu kwenye ndoa bado, tukiwa ndani ya ndoa si itakuwa balaa?

Mimi pia nina mapungufu yangu kama vile ni mkali sana, pia nina maneno ya kukejeli(wengine wanasema dharau), but mara nyingi nakuwa open sana sio mtu wa kuficha ficha.

Je nifanyeje? Binti nampenda, napenda niishi nae ila kwa style hii nyumba si itawaka moto?!

Ushauri

kwanz amshukuru Mungu amekuonyesha tabia zake mapema kabla hujajipiga pingu za maisha.wengine huzifisha unakuja kukutana nazo baada ya ndoa.kazi kwako.pasua kichwa zinakuwa ziaidi pale uko ndani ya ndoa tayari,halafu bint ndio anayatoa makucha..akili kumkochwa hapo mwana,chagua kusuka au kunyoa,kuachia ngazi au kufa na tai shingoni,chugua mbichi au mbivu,mbivu au mbovu. Kaaaaazi kweli kwweli uchumba plus ndoa za sasa zaidi ya ujuavyo,hiki ndio kizazi kipya cha faceboook,jf,twitter,u tube, sijui na makorokoro gani.hujakuta hapa jamvini watu na ndoa zao wako busy kule chit chat?jiulize kazi za ndani wanafanya saa ngapi kana sio housegirl kuwa mama mwenye nyumba?
 
Tigga Mumba samahani kwa Avarter yako, kwa nini unapenda vipicha vya namna hiyo, itakuwa vigumu kukushauri labda hata jikoni u mpenzi ndio maana huyu Bint anakuonea Uwe mkali na ujitambue kuwa wewe ni Mwanamume hata kwa matendo, mwandiko wako, michezo yako hata na picha za album yako ziwe za kidumedume, ukiona mtoto anapozaliwa huonyesha mapema jinsia yake, km kujipikilisha au kuvuta magari.
Huyo Bint kuna kitu kagundua mtimue atakutana na watu wa Musoma au Wasukuma
sorry sorry sana
 
Last edited by a moderator:
najua wengi mtanishambulia ila kwa ujumla huyu kaka anampenda sana huyo mchumba wake ila kwa ukweli bila kumumunya maneno kama hayo uliyoyasema kutoka moyoni ni kwamba huyo dada hafai kuwa mke ambae kesho hata ukifariki (HATUOMBEI) ataendeleza kuwalea watoto wenu katika malezi bora ya maisha na ya kujua kujitegemea na ndio maana huwa tunaambiwa mke bora hutoka kwa mungu na mungu amekuonyesha mapema kujua dalili zote ambazo unaziona sio sawa kwa msichana wa kiafrica na maadili yake so please nakushauri mahari simamisha kabisa huo ndio ukweli, kupika, kufanya usafi na hata yeye kujitunza hawezi?? no way kimbia kabisa mkuu hakuna njia yoyote ya kumbadili huyu dada ndio malezi aliyoyapata kutoka kwa wazazi wake kamwe wewe huwezi kuyabadilisha, take a word from me. usiangalie umemtambulisha kwa wangapi angalia wewe maana hawatakuja kukusaidia katik hiyo ndoa yako,
 
Nitamwambia(na anafahamu maana nilishamwambia). Akionekana kutobadilika itabidi nifanye maamuzi magumu

mkuu fanya maamuzi magumu haraka najua yanamadhara yake ila kaa mbali usije ukajuta baadae ukasema ningelijua ningeliwasikiliza wana jf.
 
kuoga anaoga au napo uvivu maana wadada wa siku hizi wanajua weka urembo sana ukiangalia kichwa kina unga
 
kaa naye mwambie mwanzo hadi mwisho ajue wajibu wake ikiwezekana wasiliana na mama yake amkalishe chini amwonye au amfunde asijekuwa mzigo kwa baadaye ndo hawa ambao huwaachia wasichana wa kazi kufua hadi nguo za ndani pole kaka yangu mi na ushahidi wa watu ambao mpaka anaingia chuo hajui kupika wengine wako rafu wavivu hadi nashangaa nasema wanaume wa na kazi kwa kuchagua wa chumba ndo hivyo usione ua lachanua kwa nje tu hasa wakina dada wa leo tena wale waliosoma ndo balaa wavivu hakuna. jamani wadada hawa wanakera tena sana

Kazi kweli kweli
 
ndio hizi nyumba unaingia unashindwa hata kuomba maji ya kunywa. Yaani ukiomba glass inatolewa kwenye kabati bila kufutwa wala nini, alafu ukute haikuoshwa vizuri, glass ukiisogeza kinywani inatoa harufu ya mayai mabichi.....mbona kiu itakuishia au utatapika kabisa.
mleta mada, nakushauri umuepuke huyo binti, especially unaonekana unakerwa sana na uchafu na uvivu. sasa ivi unaweza mvumilia sababu mapenzi bado motomoto, but trust me, marriage is more than that

Kabisaaaa,km mtu anashindwa kutoa hata sahani ya chakula ni balaa,au unaingia tu mlangoni unakutana na kijiko,yaan shagala bagala!.........thanx to my mom aisee!
 
Nakula bia sasa hapa nikitafakari ushauri ila am pissed off

Yap,una wakati mgum bt no way out!km anakukera mpaka unaamua kukaa kwny tv o computer,means u a nt happy at all,wakati ndoa ni upendo na furaha!ss ww mwenzetu muda wa kurudi nyumbani utakuwa huutamani coz huoni raha ya kurudi hom
 
Badili Tabia huyo mdada anachojua ni kufanyiwa ukaguzi tu

loh The secretary ni kweli kabisa....

Huyo binti ana kipaji maalum cha uvivu aisee.....

Sipati picha akiolewa halafu awe ananyonyesha maweeeeeeeee
nahisi atakuwa anachuruzika maziwa..... Nepi zenye nnya ya mtoto kuanzia uvunguni mwa kitanda hadi kibarazani.....

Mlima wa vyombo vichafu......
Nywele hazitamaniki....
Katoto katakuwa kananuka mikojo......tongotongo uso mzima....

Mmmmh walaahhhhhhhhh kazi ipo
 
Last edited by a moderator:
Badili Tabia huyo mdada anachojua ni kufanyiwa ukaguzi tu

loh The secretary ni kweli kabisa....

Huyo binti ana kipaji maalum cha uvivu aisee.....

Sipati picha akiolewa halafu awe ananyonyesha maweeeeeeeee
nahisi atakuwa anachuruzika maziwa..... Nepi zenye nnya ya mtoto kuanzia uvunguni mwa kitanda hadi kibarazani.....

Mlima wa vyombo vichafu......
Nywele hazitamaniki....
Katoto katakuwa kananuka mikojo......tongotongo uso mzima....

Mmmmh walaahhhhhhhhh kazi ipo
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom