Yaani madudu yote hayo USHAURI wa nini?? Something wrong in your brain... JITAMBUE Mwanaume...
piga chini huyo!!mabinti wa facebook hao na vampire diaries lol
Nje ya mada hapa: SWALI KWAKO MLETA THREAD, KWANI WANAUME WANAOA ILI WAPIKIWE NA KUFULIWA? KAMA NI KUFULIWA MBONA KUNA MADOBI NA KAMA KUPIKIWA MBONA KUNA MAMA/BABA LISHE? NI NINI HASA KINACHOFUATWA KWENYE NDOA? (EMBU TUTAFAKARI KWA PAMOJA HAPA)
Hapana lakini ningependa mke akiwa responsible kwenye mambo ya usafi/upishi. House girl anakuwa supportive especially tunavyobanwa na kazi. Mimi ningependa mfano weekend tunafua na kupika wote!
Naomba ushauri wenu. Nina mchumba wangu tumekaa muda mrefu kama miaka 5 hivi. Sasa tumeona ni muda muafaka wa kuoana. Kipindi kirefu cha uhusiano wetu hatukuwa tunaishi pamoja as yeye alikuwa anasoma mkoa mwingine nami mwingine. Lakini hii haikupunguza mapenzi yetu maana tulikuwa tunawasiliana na kutembeleana mara kwa mara.
Sasa alimaliza chuo na kuanza kazi, na mimi pia nina kwangu. Tukawa tuko close zaidi na siku moja moja tunakaa pamoja nyumbani. Hili kufanya mambo yaende kwa heshima, tukafikia hatua ya kutambulishana kwa wazazi rasmi na kuanza kujipanga kwa ajili ya mahari na ndoa
Kuna tabia ambazo nimezigundua zinanikera na ninaomba ushauri.
1. Huyu binti ni mvivu
Anapenda kukaa kuangalia moviez tu. Moviez, kuchat thats it. Nyumba chafu nasafisha mwenyewe. Kila kitu kipo ndani(jiko, chakula), hataki kupika eti mpaka awe kwenye mood kwahiyo tunaishia kula chips. Nguo zangu chafu(hata za kwake) kufua ugomvi.
2. Kisirani
Mtu wa visirani, kujibu, kununa.
Sasa tunaelekea kwenye mahari lakini kichwa changu kinawaka moto. Hivi tu kwenye ndoa bado, tukiwa ndani ya ndoa si itakuwa balaa?
Mimi pia nina mapungufu yangu kama vile ni mkali sana, pia nina maneno ya kukejeli(wengine wanasema dharau), but mara nyingi nakuwa open sana sio mtu wa kuficha ficha.
Je nifanyeje? Binti nampenda, napenda niishi nae ila kwa style hii nyumba si itawaka moto?!
Ushauri
kaka kwa maelezo yako hamtafika mbali.kama umeshindwa kumbadirisha kwa iyo miaka 5 huyo ni vigumu kubadirika.Nakushauri husitoe mahali kwanza ili umpatie kipindi cha kujirekebisha.ni ayo tu.
tabia ya mtu ya kila siku ikikusumbua, ni kosa lako mwenyewe na si mwenye tabia husika, ukishafahamu mwenzako yukoje jifunze kuishi naye........step ya kwanza ni kutambua madhaifu yake, step ya pili ni kuyakubali....step ya tatu ni kutafuta mbadala wa mapungufu hayo...ambayo tayari umeupata, kwa kuwa umesema hapo, kuwa unafagia, unafua nk.....TATIZO lako kubwa ni kuwa uimeruka step ya pili...........kama una nia ya kufunga naye pingu za maisha, na kweli unampenda...nakushauri kubali mapungufu ya mwenza wako...na ingia naye kwenye ndoa, IF naye anakupenda kama au zaidi ya umpendavyo.........for more advise on the matter of relationships and marriage...inbox me.....kwa wanaJF natoa ushaur bure............
Kaunga you are the most wise woman i have met.Hakuna kitu kilichonifurahisha kama self analysis yako na kukubali mapungufu.
You are one step ahead, ninakushauri kaa mjadili bila kutumia ukali; make her reason with you na especially hiyo ya kula junk food. Lakini kama wote ni wafanyakazi, mnaweza kuhire a help, mtu akawa anakuja anafanya usafi na kufua at least 4 times a week, huku mkijipanga jinsi ya kujitegemea.
Nina uhakika sababu ya kumpenda ni zaidi ya kuwa mfanyakazi wa nyumbani; hivyo basi, hizo shughuli mjadiliane zitafanyika vipi coz lazima zifanyike; mwambie aje na suggestion.
Hapana lakini ningependa mke akiwa responsible kwenye mambo ya usafi/upishi. House girl anakuwa supportive especially tunavyobanwa na kazi. Mimi ningependa mfano weekend tunafua na kupika wote!
WanaJF ma great thinkers,
Nimefanikiwa kuongea na mchumba wangu nikiwa ''CALM" na ningependa nishare tena nanyi kwa yaliyojiri;
Tumeongea taratibu, tukiwa wote hatuna tension(especially mimi ambaye dakika moja tu nakuwa mkali), nikagundua vitu kadhaa sababu ya kuongea kwa upole na lugha laini.
Kuhusu kupika
Binti anapenda kupika lakini mara chache anajisikia kama kauvivu. Ni kwasababu hatujakaa sana wote kwa muda mrefu(max ni 3-4 days) but anapenda na atajirekebisha kwenye hilo. Angependa sana tuwe tunashirikiana kama ikiwa weekend(ambayo mimi nilishaafiki maana sikuwa najua kupika), so nami pia najifunza.
Kuhusu moviez
Ni kweli anapenda kuangalia moviez, hiyo inatokana na kuwa idle kwa kipindi fulani(likizo) lakini kwa jinsi tulivyoongea atahakikisha mengine yanapewa priority
Uvivu
Ameadmit anahisi uvivu ila anahisi ni kwa namna alivyolelewa maana walikuwa wanapewa kila kitu. Mara nyingi nikimfokea anajisikia vibaya na kuniogopa but atabadilika
Kutokufua
Hii inaunganishwa na uvivu ila atajirekebisha
Kujibu, jeuri na kisirani
Mara nyingi approach yangu inamuoffend na nikagundua kumbe asiponijibu(nawaza kama ananidharau), kumbe mimi ndiye namfanya ajibu. Ila tukiongea nikiwa calm, anasikiliza na anaheshimu.
Kisirani na kuamua kukaa kimya kwa muda, anahisi nikikasirika nahitaji muda wa kucalm down, so anafanya hivyo ili kunipa nafasi nitulie. Ameadmit ataacha.
Hitimisho
Kusema ukweli huyu binti tunajuana sana. Kikubwa ambacho naona kimejenga tabia ambazo zinaweza kubadilika ni malezi na MIMI mwenyewe approach yangu kwake.
Nimeamua kutafuta consultation/kusali etc namna ya kutokukasirika na kupanic. Jana tumeongea mambo mazito, makubwa mno ambayo siwezi kuandika mengine(personal sana) but in open and calm way. I'm happy.
Yeye atakuwa karibu na rafiki yake ambaye ameingia kwenye ndoa muda kadhaa kujaribu kumshauri namna ya kuhandle situations, namna ya kutake care husband etc. Ukikaa na mtu unayempenda utaona kasoro, lakini kasoro ndio challenges. Nobody is perfect.
Mipango ya harusi inaendelea. Nitarudi tena kwa ushauri. Mbarikiwe
kaka ndoa haijalibiwi . fikir kabla ya kutenda