Mchumba ninayekaribia kumuoa simuelewi

Tigga Mumba

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
746
473
Naomba ushauri wenu. Nina mchumba wangu tumekaa muda mrefu kama miaka 5 hivi. Sasa tumeona ni muda muafaka wa kuoana. Kipindi kirefu cha uhusiano wetu hatukuwa tunaishi pamoja as yeye alikuwa anasoma mkoa mwingine nami mwingine. Lakini hii haikupunguza mapenzi yetu maana tulikuwa tunawasiliana na kutembeleana mara kwa mara.

Sasa alimaliza chuo na kuanza kazi, na mimi pia nina kwangu. Tukawa tuko close zaidi na siku moja moja tunakaa pamoja nyumbani. Hili kufanya mambo yaende kwa heshima, tukafikia hatua ya kutambulishana kwa wazazi rasmi na kuanza kujipanga kwa ajili ya mahari na ndoa

Kuna tabia ambazo nimezigundua zinanikera na ninaomba ushauri.

1. Huyu binti ni mvivu
Anapenda kukaa kuangalia moviez tu. Moviez, kuchat thats it. Nyumba chafu nasafisha mwenyewe. Kila kitu kipo ndani(jiko, chakula), hataki kupika eti mpaka awe kwenye mood kwahiyo tunaishia kula chips. Nguo zangu chafu(hata za kwake) kufua ugomvi.

2. Kisirani
Mtu wa visirani, kujibu, kununa.

Sasa tunaelekea kwenye mahari lakini kichwa changu kinawaka moto. Hivi tu kwenye ndoa bado, tukiwa ndani ya ndoa si itakuwa balaa?

Mimi pia nina mapungufu yangu kama vile ni mkali sana, pia nina maneno ya kukejeli(wengine wanasema dharau), but mara nyingi nakuwa open sana sio mtu wa kuficha ficha.

Je nifanyeje? Binti nampenda, napenda niishi nae ila kwa style hii nyumba si itawaka moto?!

Ushauri
 
Tafakari upya kuhusu athari ya tabia hizo katika maisha yenu ya ndoa. Ndoa haijaribiwi.
 
Baada ya kusoma maelezo yako, nawiwa kusema moyo na nafsi yako vimeshakubali kuishi na huyo binti.
Sasa basi, kama ndio hivyo sidhani kama kuna usauri wowote utaoweza kubadili uamuzi wako na ndio maana umeweza kuishinda ile nia iliyokuwa ikikuelekeza uachane naye hata ukafikia uamuzi wa kuposa na kutoa mahari.

"Ukipenda boga, penda na ua lake"
 
Kaka hata mimi nipo kama wewe,ila ni kawaida kwa wanaume wasafi kuwa namna hiyo na hasa ukikutana na mwanamke mchafu na mvivu,anakera sana.me naona hakuna cha kukushauri maana unalijua tatizo na uamuzi tayari unao,sema unaogopa tu kuutekeleza kwa kuhofu utachukuliwaje..we tekeleza unachoona ni sahihi kwako.
 
Baada ya kusoma maelezo yako, nawiwa kusema moyo na nafsi yako vimeshakubali kuishi na huyo binti.
Sasa basi, kama ndio hivyo sidhani kama kuna usauri wowote utaoweza kubadili uamuzi wako na ndio maana umeweza kuishinda ile nia iliyokuwa ikikuelekeza uachane naye hata ukafikia uamuzi wa kuposa na kutoa mahari.

"Ukipenda boga, penda na ua lake"

Ni kweli. Je kuna namna unahisi labda nitumie kumfanya aweze kujihusisha na mambo ya usafi/kupika?
 
Naomba ushauri wenu. Nina mchumba wangu tumekaa muda mrefu kama miaka 5 hivi. Sasa tumeona ni muda muafaka wa kuoana. Kipindi kirefu cha uhusiano wetu hatukuwa tunaishi pamoja as yeye alikuwa anasoma mkoa mwingine nami mwingine. Lakini hii haikupunguza mapenzi yetu maana tulikuwa tunawasiliana na kutembeleana mara kwa mara.

Sasa alimaliza chuo na kuanza kazi, na mimi pia nina kwangu. Tukawa tuko close zaidi na siku moja moja tunakaa pamoja nyumbani. Hili kufanya mambo yaende kwa heshima, tukafikia hatua ya kutambulishana kwa wazazi rasmi na kuanza kujipanga kwa ajili ya mahari na ndoa

Kuna tabia ambazo nimezigundua zinanikera na ninaomba ushauri.

1. Huyu binti ni mvivu
Anapenda kukaa kuangalia moviez tu. Moviez, kuchat thats it. Nyumba chafu nasafisha mwenyewe. Kila kitu kipo ndani(jiko, chakula), hataki kupika eti mpaka awe kwenye mood kwahiyo tunaishia kula chips. Nguo zangu chafu(hata za kwake) kufua ugomvi.

2. Kisirani
Mtu wa visirani, kujibu, kununa.

Sasa tunaelekea kwenye mahari lakini kichwa changu kinawaka moto. Hivi tu kwenye ndoa bado, tukiwa ndani ya ndoa si itakuwa balaa?

Mimi pia nina mapungufu yangu kama vile ni mkali sana, pia nina maneno ya kukejeli(wengine wanasema dharau), but mara nyingi nakuwa open sana sio mtu wa kuficha ficha.

Je nifanyeje? Binti nampenda, napenda niishi nae ila kwa style hii nyumba si itawaka moto?!

Ushauri

Hakuna kitu kilichonifurahisha kama self analysis yako na kukubali mapungufu.
You are one step ahead, ninakushauri kaa mjadili bila kutumia ukali; make her reason with you na especially hiyo ya kula junk food. Lakini kama wote ni wafanyakazi, mnaweza kuhire a help, mtu akawa anakuja anafanya usafi na kufua at least 4 times a week, huku mkijipanga jinsi ya kujitegemea.

Nina uhakika sababu ya kumpenda ni zaidi ya kuwa mfanyakazi wa nyumbani; hivyo basi, hizo shughuli mjadiliane zitafanyika vipi coz lazima zifanyike; mwambie aje na suggestion.
 
Ni kweli. Je kuna namna unahisi labda nitumie kumfanya aweze kujihusisha na mambo ya usafi/kupika?

mwambie ukweli kwamba huwezi kuoa mwanamke asiyependa kupika, kufua, kufanya usafi na mengineyo...maana hayo anakufanyia wewe, jiulize mkianza kuwa na familia watoto si ndio watakua vimbulu!
 
Ni kweli. Je kuna namna
unahisi labda nitumie kumfanya aweze kujihusisha na mambo ya
usafi/kupika?

Yaani umeshindwa kum-face ukamweleza tabia ambazo huzifurahii na ukamshauri abadilike unakuja kushtaki jf! Halafu unajisifu we mkali.
 
mkuu mshukuru Mungu kwa kukuonyesha hilo...maisha ya ndoa si mchezo huwezi ingia katika hali hiyo...ingekuwa mimi natupa kule najipanga upya...think twice kaka...
 
Yaani umeshindwa kum-face ukamweleza tabia ambazo huzifurahii na ukamshauri abadilike unakuja kushtaki jf! Halafu unajisifu we mkali.

Nilishamwambia lakini kutokana na namna navyoweka maneno yangu, nilikuwa mkali sana! Aliniogopa, nikajishusha tukasonga mbele.
 
Yaani umeshindwa kum-face ukamweleza tabia ambazo huzifurahii na ukamshauri abadilike unakuja kushtaki jf! Halafu unajisifu we mkali.

hizo ni dalili mbaya sana...atabadilika kusave mahusiano then later atakuja na hari na kasi mpya,nyumba itakuwa uwanja wa vita...binafsi mdada akileta dharau tu hata kam nimemtambulisha namdelete
 
ahh raha kweli kweli

mpangiane zamu km vip
usiwe unafanya peke ako
wewe fanya j3 mpk j5 yeye alh mpk jumamos
jumapil afta chach muwe na genearal klniles muwe mnafanya pamoja

mhh kuna mkaka mmoja ana tatizo ilo...mkewe kutandika kitanda mwiko mashuka yapo vululu lulu ..shuka linakaa ata siku 8 kitandan na ili joto jaman dah...na choo kipo ndan bas kusafisha akuna tiles nyeussssssssssssssssss...full kunuka sink km la choo chamnaz mmoja puuuhhh!!!!!!!!!!!kinyaaaa hatar
 
inakuaje unataka kumuoa mtu ambae hauwezi kumkosoa?
Manake kwa maelezo yako haujamwambia kuwa haufurahishwi na hizo tabia.
Mkalishe chini muyazungumze na ujipe muda ujiridhishe kuwa amejirekebisha.
 
Yaani umeshindwa kum-face ukamweleza tabia ambazo huzifurahii na ukamshauri abadilike unakuja kushtaki jf! Halafu unajisifu we mkali.

hizo ni dalili mbaya sana...atabadilika kusave mahusiano then later atakuja na hari na kasi mpya,nyumba itakuwa uwanja wa vita...binafsi mdada akileta dharau tu hata kam nimemtambulisha namdelete
 
inakuaje unataka kumuoa mtu ambae hauwezi kumkosoa?
Manake kwa maelezo yako haujamwambia kuwa haufurahishwi na hizo tabia.
Mkalishe chini muyazungumze na ujipe muda ujiridhishe kuwa amejirekebisha.

Kumkosoa ninaweza. Nitakaa nae chini kiupole kumuelezea tena maana nilishakaa nae chini ila nikatumia lugha kali sana. Ila asipobadilika ataniweka kwenye wakati mgumu sana maana nakereka mno.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom