Mchumba ninayekaribia kumuoa simuelewi

Yaani umeshindwa kum-face ukamweleza tabia ambazo huzifurahii na ukamshauri abadilike unakuja kushtaki jf! Halafu unajisifu we mkali.

Ennie hajaja kushitaki, kaleta mada tu, changia ama usichangie. Naona kama unauliza maswali badala ya kutoa ushauri.
 
hizo ni dalili mbaya sana...atabadilika kusave mahusiano then later atakuja na hari na kasi mpya,nyumba itakuwa uwanja wa vita...binafsi mdada akileta dharau tu hata kam nimemtambulisha namdelete

Kaka unazidi kunifanya nikose amani
 
Nimeamua kutafuta dada wa usafi anakuja mara kadhaa kwa wiki. Kwa sasa binti yuko kwao, so dada wa usafi anakuja wakati niko kazini, anasafisha na kufua na kupika. Nikirudi nakuta chakula tayari. Sijamwambia na hajui, atashangaa akija nyumba inangáa. Nafahamu kabisa atapiga vita kuwa na dada wa kufanya usafi!!!

Moviez Moviez Moviez... Amenifanya nichukie neno Moviez!!!
 
Pole sana kaka. Nakushauri kaa nae taratibu, jishushe na umuelezee namna gani unavyojisikia akiwa hivyo. Pia muelezee ungependa muwe mnafanya wote sababu usafi pia ni heshima. Nyumba chafu haipendezi.

Shirikisha rafiki yako unayemuamini aliyeko kwenye ndoa. Naamini kama unampenda na mnapendana, hivyo ni vitu vidogo sana vya kusort out.
 
mwanamke mvivu aisee sikushauri sana
for those married man like me sitegemei eti mwanamke awe mvivu
tunasaidiana ndio lakini kama hajui wajibu wake kama mama nyumba itakuwa sio nyumba
utakuja kujuta sana mbele ya safari, ndio huyo hata mtoto akijisaidia atamwacha au amwite housegal ambadilishe
atafanya chumba chenu kunuka,she will not bother.
my wife nakiri ni msomi kuliko mimi ana kazi nzuri zaidi yangu lakini sio mvivu
tunasaidiana sana lakini kuna vitu anapenda kufanya mwenyewe yeye kama mama
kaa nae chini mjadiliane ukiona habadiliki amua kivingine mapema
NDOA HAIJARIBIWI USITEGEMEE ATABADILIKA KAMA HAJABADILIKA SASA.
 
hakuna hata haja ya kuzungusha maneno,mwambie ukweli kuwa hizo tabia zake huzipendi na km hategemei kubadilika mapema unaweza ku-call off hiyo ndoa..km yuko serious utaona mabadiliko lakini akianza stori za kununa achana naye.
 
Mama weee! Huna mchumba hapo...utajuta kumfahamu ukimuoa. Yaani mko wawili keshaonyesha uvivu...akiwa na mtoto ndio hao wanawekaga used pampus juu ya TV.

Kama umeshakuwa na akili ya kuona udhaifu wake piga chini faster!

Hakuna kitu kibaya kama mke mvivu na mchafu.

Kuna rafiki yangu kaka yake ana mke wa hivyo; mpaka jamaa hataki wageni kwake kwa kuwa hali ni mbaya...ma pampus yamezagaa nyumba nzima eti kisa wana mtoto mchanga.

Maisha utayaona machungu...ndoa utaiona ndoano.

Naomba ushauri wenu. Nina mchumba wangu tumekaa muda mrefu kama miaka 5 hivi. Sasa tumeona ni muda muafaka wa kuoana. Kipindi kirefu cha uhusiano wetu hatukuwa tunaishi pamoja as yeye alikuwa anasoma mkoa mwingine nami mwingine. Lakini hii haikupunguza mapenzi yetu maana tulikuwa tunawasiliana na kutembeleana mara kwa mara.

Sasa alimaliza chuo na kuanza kazi, na mimi pia nina kwangu. Tukawa tuko close zaidi na siku moja moja tunakaa pamoja nyumbani. Hili kufanya mambo yaende kwa heshima, tukafikia hatua ya kutambulishana kwa wazazi rasmi na kuanza kujipanga kwa ajili ya mahari na ndoa

Kuna tabia ambazo nimezigundua zinanikera na ninaomba ushauri.

1. Huyu binti ni mvivu
Anapenda kukaa kuangalia moviez tu. Moviez, kuchat thats it. Nyumba chafu nasafisha mwenyewe. Kila kitu kipo ndani(jiko, chakula), hataki kupika eti mpaka awe kwenye mood kwahiyo tunaishia kula chips. Nguo zangu chafu(hata za kwake) kufua ugomvi.

2. Kisirani
Mtu wa visirani, kujibu, kununa.

Sasa tunaelekea kwenye mahari lakini kichwa changu kinawaka moto. Hivi tu kwenye ndoa bado, tukiwa ndani ya ndoa si itakuwa balaa?

Mimi pia nina mapungufu yangu kama vile ni mkali sana, pia nina maneno ya kukejeli(wengine wanasema dharau), but mara nyingi nakuwa open sana sio mtu wa kuficha ficha.

Je nifanyeje? Binti nampenda, napenda niishi nae ila kwa style hii nyumba si itawaka moto?!

Ushauri
 
Pole sana kaka, ila kiukwel km anapenda tu movies na kuchat una hasara, mwanamke huyo hajapata malez mazur kwani anaonekana kadekezwa sana. Kama hatobdlika ujue hyo nyumb kutakuwa na misundertanding kila iitwapo leo. Ni bora mkawekana sawa kbs kabla hamjaingia kwny ndoa coz mkshaingia kutoka n vgumu mno.
 
Tabia haina dawa...huna haja ya kumfundisha usafi...achana nae;
Anaweza kujidai kabadilika ili apate ndoa...ukishamuoa utajajuta...kwani kumuacha itakuwa inshu na yeye atakuwa anajua huwezi kumuacha.

Mtu mchafu hawezi badili tabia yake ukubwani...mwache atapata mchafu mwenzie.
 
Afu anasema anapika akiwa kwenye mood???? Huyu si mchafu na mvivu tu ila ni mjeuri...mimi ninawajua watu wa hivyo kaka kaa chonjo.
 
Afadhali hata huyo amekuonesha tabia zake mapema mkuu, kazi kwako kusuka ama kunyoa,ila mziki unao
 
mwanamke mvivu aisee sikushauri sana
for those married man like me sitegemei eti mwanamke awe mvivu
tunasaidiana ndio lakini kama hajui wajibu wake kama mama nyumba itakuwa sio nyumba
utakuja kujuta sana mbele ya safari, ndio huyo hata mtoto akijisaidia atamwacha au amwite housegal ambadilishe
atafanya chumba chenu kunuka,she will not bother.
my wife nakiri ni msomi kuliko mimi ana kazi nzuri zaidi yangu lakini sio mvivu
tunasaidiana sana lakini kuna vitu anapenda kufanya mwenyewe yeye kama mama
kaa nae chini mjadiliane ukiona habadiliki amua kivingine mapema
NDOA HAIJARIBIWI USITEGEMEE ATABADILIKA KAMA HAJABADILIKA SASA.

Nachukua ushauri wako. Nitakaa nae chini nitaongea nae na kumueleza(ingawa nilishafanya hivyo ila kwa ukali). Nitaongea nae kwa upole, taratibu ikiwezekana hata kwa hisia. Natumai atanielewa ila kama asipobadilika ninaweza kufanya maamuzi magumu sana!
 
Mkuu Tigga Mumba toa ajira kwa House girl / boy atafanyakazi zote mwache mke mtarajiwa ajipumzishe kazi yake kubwa ni kukuzalia watoto na kukuliwaza.
 
Last edited by a moderator:
Naomba ushauri wenu. Nina mchumba wangu tumekaa muda mrefu kama miaka 5 hivi. Sasa tumeona ni muda muafaka wa kuoana. Kipindi kirefu cha uhusiano wetu hatukuwa tunaishi pamoja as yeye alikuwa anasoma mkoa mwingine nami mwingine. Lakini hii haikupunguza mapenzi yetu maana tulikuwa tunawasiliana na kutembeleana mara kwa mara.

Sasa alimaliza chuo na kuanza kazi, na mimi pia nina kwangu. Tukawa tuko close zaidi na siku moja moja tunakaa pamoja nyumbani. Hili kufanya mambo yaende kwa heshima, tukafikia hatua ya kutambulishana kwa wazazi rasmi na kuanza kujipanga kwa ajili ya mahari na ndoa

Kuna tabia ambazo nimezigundua zinanikera na ninaomba ushauri.

1. Huyu binti ni mvivu
Anapenda kukaa kuangalia moviez tu. Moviez, kuchat thats it. Nyumba chafu nasafisha mwenyewe. Kila kitu kipo ndani(jiko, chakula), hataki kupika eti mpaka awe kwenye mood kwahiyo tunaishia kula chips. Nguo zangu chafu(hata za kwake) kufua ugomvi.

2. Kisirani
Mtu wa visirani, kujibu, kununa.

Sasa tunaelekea kwenye mahari lakini kichwa changu kinawaka moto. Hivi tu kwenye ndoa bado, tukiwa ndani ya ndoa si itakuwa balaa?

Mimi pia nina mapungufu yangu kama vile ni mkali sana, pia nina maneno ya kukejeli(wengine wanasema dharau), but mara nyingi nakuwa open sana sio mtu wa kuficha ficha.

Je nifanyeje? Binti nampenda, napenda niishi nae ila kwa style hii nyumba si itawaka moto?!

Ushauri

Sioni tatizo hapo mkuu, sio lazima mwanamke ajue kufanya yote hayo siku hizi ndio maana kuna 1.kusaidiana 2.housegirl na boy, 3.mighahawa, 4.dobi nk nk. hauko pekeyako hebu tafuta kitabu cha James Hadley Chase "Believe this, you will believe anything" kuna dada anatwa Rhoda hebu kisome hicho
 
unajua ndo c kitu cha mchezo!im sure npaka umeleta mada hapa,upo njia panda na unafikiria ukiamua kudelete hutaeleweka!bt mwambie hivi,km hatabadirika upo tayari kuachana nae uone km hata badirika?...its better kuanza upya kuliko ikucost maisha
 
Mkuu Tigga Mumba toa ajira kwa House girl / boy atafanyakazi zote mwache mke mtarajiwa ajipumzishe kazi yake kubwa ni kukuzalia watoto na kukuliwaza.

Aaah wapi,acha kumdanganya mwenzio,ndo mwisho wa siku utakuta housegal kaolewa mke katimuliwa,coz dada wa kazi anakuwa responsible to the extent mtu anaona bora huyu!,coz kuna vitu vingine km mwanamke lzm afanye ht km kuna msaidizi!
Wht abt ujeuri nao atafanyaje?huyo piga chini,kuanza upya c ujinga
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli. Je kuna namna unahisi labda nitumie kumfanya aweze kujihusisha na mambo ya usafi/kupika?

kaa naye mwambie mwanzo hadi mwisho ajue wajibu wake ikiwezekana wasiliana na mama yake amkalishe chini amwonye au amfunde asijekuwa mzigo kwa baadaye ndo hawa ambao huwaachia wasichana wa kazi kufua hadi nguo za ndani pole kaka yangu mi na ushahidi wa watu ambao mpaka anaingia chuo hajui kupika wengine wako rafu wavivu hadi nashangaa nasema wanaume wa na kazi kwa kuchagua wa chumba ndo hivyo usione ua lachanua kwa nje tu hasa wakina dada wa leo tena wale waliosoma ndo balaa wavivu hakuna. jamani wadada hawa wanakera tena sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom