unajua shida ya kuishi na jitu lenye maneno ya kejeli wewe? Mbona mwenzio anakuvumilia na udhaifu wako?
Ukitaka mwanamke/mwanaume perfect muumbe wa kwako, la sivyo maisha ni kuvumiliana.....
Kuhusu kufua simple si wote mna kazi changeni laki nane nane mmnunue mashine ya kufulia....
Zungumza nae kuhusu kupika (ila mmmh huyo nae uvivu kapitiliza hata kupika??????) je anarudi amechoka sana?
Kama kuna wanawake watu wazima kwao zungumza nao, waketi nae na kumfundisha majukumu ya mke kwenye nyumba.....
Na kama mna uwezo wekeni house girl, maana kumbuka wewe unafanya kazi yeye anafanya kazi, mkirudi ofisini wewe unachukua remoti na yeyeaingie jikoni kupika, aoshe vyombo, asafishe nyumba, uwanja, apige pasi mwisho ya siku atachoka ashindwe kukupa unyumba urudi hapa na thread mpya......
Swali la nyongeza, mnaporudi ofisini unamsaidia kazi? Au wewe miguu juu mwenzio ahenyeke?