Tatizo lenu mnajiona mmesoma sana na kudharau wazazi wenu, hebu muulize mzazi sababu za kukataa ni nini na uone kama zina logic kisha ukiona ni suala la hulka basi jaribu kusema naye taratibu, kwa vyovyote vile msilete uzungu kwa masuala haya yenye historia na tamaduni, kumbuka unaunganisha koo hapo na wanaouliza unaoa wewe au unaoa ukoo hawajui kuwa pamoja na kuwa mke ni wako lakini anakuwa sehemu ya jamii unayomleta na wao anakuwa ndugu yao, sasa ukileta jeuri tu ukasema maisha ya kisasa mama amezeeka au amepitwa na wakati, angalia urembo na mnato wa huyo unayemuita mchaga then puuzia wazazi then utarudi kutupa report hapa. Wengine wanachangia hata ndoa hawaijui hata hawajawahi kuwa na mahusiano yanayozidi wiki moja. Changanya na zako ila at the very end mwamuzi ni wewe, kikubwa hekima na umtangulize Mungu.