Mchumba anasema atoe mimba

Mchumba anasema atoe mimba

Wasifanye siri waeleze kuwa ana mimba ili mambo yawe haraka, kuliko kuficha maana na kutoa mimba ni dhambi hawawezi jua labda mungu ndo kawapangia mtotot huyo huyo mmoja,
 
Tayar bint kamwambia jamaa kuwa anamwambia baba yake kwani nilimshauri hivyo... mwanaume kamjibu amwambie alafu waone kati ya yeye na mwanaume wazazi watamwamini nani

Basi mwambie huyo binti azae tu, kwa sababu;

-Hajui huyo mwanaume alichoongea/alichowaambia wazazi wake hadi ndoa ikaahirishwa kwa kisingizio cha "pesa hakuna".

-Huyo mwanaume ni kama vile hamtaki anashindwa atamuachaje ndio maana kaamua kumpa mtihani wa kutoa mimba au waachane.

- Kama kweli hamtaki basi akitoa mimba tu huyo huyo mwanaume anaweza kuwaambia wazazi wake kuwa rafiki yako katoa mimba ambayo si yake (anakuwa kapata sababu) hivyo hamtaki

- Kwa sababu huyo mwanaume anajua anaaminikwa kwao huyo rafiki yako hata akienda kusema kwa wazazi wa mwanaume anaweza akakataa kuwa si yake.

*Asijaribu kutoa mimba ili apate ndoa, kwa sababu anaweza kupata madhara na asifanikiwe kupata ujauzito tena na ndoa iwe chungu
 
Pole yake huyo mdada
cha kufanya hiyo mimba asiitoe kwani akifanya hivyo
anafanya dhambi ya mauaji hivyo ailee mpaka ikue
kisha azae huyo mtoto na ndipo wafanye mikakati ya
kufunga ndoa wasiwalazimishe wazazi wao ikibidi
watamtafute mshenga wao wamwambia hilo tatizo
ndipo yeye huyo mshenga aende kwa wazazi aongee
nao kiutuuzima ili wapunguze miezi ya ndoa
ila nivyema kuwaambia wazazi kuwa wamefanya hayo
makitu na kupata mimba huyo binti ili wazazi wajue
wasiwafiche itaotea matatizo hapo baadaye
habari zenu

ninarafiki yangu wa kike anamchumba wake ilikua wafunge ndoa mwezi wa nne wazazi wa bwana harusi wamesema wamekosa hela hivyo itabidi isogezwe mbele mpaka mwezi wa saba .

Tatizo sasa bint anamimba mwez 1 wamejaribu kila njia kuwashawishi wazazi angalau waafanye mwezi wa tano ikibidi wasifanye sherehe kubwa baba ni mchungaji kakataa anasema asubiri hata kama ni mwez wa tisa.

Mwanaume kakataa kuwaambia wazazi wake ukweli alichosema bint atoe mimba kama hataki waachane akisha zaa atampelekea mtoto bint hana kazi anashindwa ataishije na huyo mtoto analia tu mi nimeshindwa hata nimsaidiaje nimeamua hili swala nililete kwenu labda mnaweza mshauri.

Samahanini kwa kuwachosha
 
Wengi hawajui kuwa ndoa ni kwa wafungaji na sherehe ni kwa ajili ya wazazi,ukikaa na kutafakari utaona kuwa cha muhimu ni ndoa kuliko sherehe hivyo kama watoto wanaona inafaa kwao kufunga ndoa wafunge tu kwa kuwa baraka za wazazi zimekwishatoka na kama wazazi wanavyotaka sherehe ije baadae kuliko kuanza mambo ya kuua kiumbe kilichopo tumboni ama kuachana.

Hii tabia ya baadhi wanaume kutesti kwanza kama binti anashika mimba kwanza ndio wanatangaza ndoa ndio hupelekea matatizo yote haya.
 
Ulimbukeni wa sherehe za harusi unatutesa sana. Kila siku kukabana na michango. Kama uwezo haupo si mfanye kinachowezekana? Usikute huyo mchungaji akamwambia binti we ni mzinzi hufai kuolewa na mwanangu
 
Mi naona bi harus mtarajiwa atoroke fasta,akajifiche mpaka atakapojifungua ndo arud kufunga ndoa,azae tu wala asitoe hcho kiumbe
 
Naomba niseme kwa kutoa mfano hai,
kuna bidada alibeba ujauzito kabla ya ndoa kufungwa,yule mwanaume akamwambia itakua aibu tukatoe mimba,
binti huyoo hospital mimba ikatolewa...
Sherehe ikafanyika yaani nderemo na vifijo..honeymoon ikaendeka kama hawajawahi kukutana vile..
Mwaka ukapita,wa pili wa tano....hakuna mtoto
kwenda kupima kumbe bidada hana kizazi..laa haula!
Visa vikaanza mara oooh ni uzinzi wako ulikufanya ukatoa mimba,(alizini na nani?)..
Watu watanionaje miaka yote hii sina mtoto!...
Bint anasononeka tu!
Mwanaume akaenda kuchapa nje,..mapenzi kwa bidada yakapotea dunia akaiona chungu:
USHAURI WANGU...
Katika maisha usipende kujiuliza hivi watanionaje,watasemaje n.k.
Jiulize je hili laupendeza moyo wangu kama ndivyo hayaa lifanye..
Ila simshauri binti atoe mimba mwanaume alie tayari mimba itolewe pasi na sababu za msingi(kiafya)aweza kukutelekea familia na kukuacha...
Binti afungue akili.
 
Binti akomae tu ajifungue mtoto wake, huenda akaitoa ikawa ndio mwisho wa kupata ujauzito mwingine.
 
Hpo pagumu ila kijana inaonekana hajitambui au hajiamini mana anaishi kutegemea sadaka, hvi kwanini watoto w wachungaji mafyatu au hamuoni hlo
 
^^
Yaani sijui mi nikoje, nisisikie nia ya mtu kutoa mimba.. Nachukia kuanzia miguu ya mtu mpaka masikio yake.
Nimeshindwa kuendelea
^^

yaan upo kama mimi huwa natamani niwaambie walaaniwe kabisa
 
Kuna huu Uzi uliletwa hapa baadaye akaja mwingine akiitwa jack 1 malalamiko yake yakielikea kwamba yeye ndie mhusika. Juzi juzi hapa kaleta thread nyingine ya kutaka kunywa sumu na watu wakatoa pole na ushauri mwingi. maimatha tunataka mrejesho ushauri wetu ulisaidia chochote kwa huyo rafiki yako?
 
Last edited by a moderator:
Kuna huu Uzi uliletwa hapa baadaye akaja mwingine akiitwa i jack 1 malalamiko yake yakielikea kwamba yeye ndie mhusika. Juzi juzi hapa kaleta thread nyingine ya kutaka kunywa sumu na watu wakatoa pole na ushauri mwingi. maimatha tunataka mrejesho ushauri wetu ulisaidia chochote kwa huyo rafiki yako?

Wanatuchezea akili cos jack 1 ndo alileta hii story juzi kasema anataka kunywa sumu...Dada Suzy na shangaziwe wakaenda guest hko wakaleta mrejesho ile Jana asubuh kuwa jack yupo salama hko arusha...
 
Last edited by a moderator:
Wanatuchezea akili cos jack 1 ndo alileta hii story juzi kasema anataka kunywa sumu...Dada Suzy na shangaziwe wakaenda guest hko wakaleta mrejesho ile Jana asubuh kuwa jack yupo salama hko arusha...

Kumbe, huo mrejesho sikuupata. Lakini on a serious note kama yaliyomtokea huyu dada ni ya kweli watu wanaomfahamu wanahitaji kuwa naye karibu. Psychologically yuko distorted anaweza kufanya kitu chochote. Ana risk factors nyingi kwa wakati mmoja, usishangae siku sio nyingi akawa psychiatric patient.
1. Amekosa ndoa
2. Mume kamkataa
3. Amefukuzwa kazi
4. Mzazi kamkataa
5. Ni mjamzito
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom