Mchina aliyepata "A" tisa NECTA

Kwa mada hii ya mchina ulemuongelea humu ndani nadhani ilistahili kumuongelea na yule mnigeria aliyepata GPA ya tano Russia yaan aliwabwaga warusi na wengineo wote waliokuwa wanasoma katika chuo hicho.
Hata hao wanigeria na huyo Daktari wao wameamua kumtangaza LKN najua ,ninafahamu na ninauhakika kuna watanzania,wanigeria,waghana,waafrika kwa ujumla wengi waliosoma urusi na wana GPA 5.
 


Sijapingana na wewe au mchangiaji mwingine yoyote yule ila nakuomba umtaje kwa maana kama ameongoza kinchi kama huyu Mchina kumbukumbu huwa ziko wazi, kumbuka huyu ni wapili siyo kishule, kikanda au sijui kimkoa bali Tanzania nzima hivyo kama yupo TanZania au Mwafrika diaspora unayemfahamu kama ulivyosema ni rahisi kumtaja hapa!
 
Hii imenifikirisha sana,kwamba waafrika tuna IQ ndogo nahisi kwa lugha nyengine rahisi ktk nchi yetu tulishawahi kuongozwa na rais mwenye IQ ndogo maana kuna siku akiwa ktk kadamnasi kwa hao wazungu alitamka kwamba "hajui kwanini Tanzania ni masikini",really...hakujua kwanini nchi anayoiongoza ni masikini?sijui na mimi niliewaza hivi IQ yangu itakuwa ktk kiwango gani.
 
Aiseee, yawezekana iwe kweli maana haiwezekani mtu awe wa pili kwa kushinda watanzania 430000
 
Asee ebu chunguzeni ayo matokeo vizuri unaweza kukuta ni ya kichina ati
 
Usipokubaliana na amri za Magufuli hata kama Ni za kipuuzi kiasi gani basi una IQ ndogo?
Oh Lord spare us!
 


Ndugu kufeli ni relative, kusema Wanafunzi wa Uingereza wanafeli Kiingereza bila kutoa frame of reference haina maana yoyote ile hoja yako ingeendana na mada yangu kama ungesema kwamba labda Wanafunzi wa Kiingereza wanafeli Kiingereza ikilinganishwa na wanafunzi wageni yaani wahamiaji ambao siyo lugha yao, hapo sasa ndiyo tungeanza kujadili lkn kusema tu wanafunzi wa Kiingereza wanafeli kiingereza inaning'inia hewani bado inakosa nyama, na isitoshe hakuna nilipohitimisha chochote bali nimeuliza swali na wala sijahitimisha kwamba sisi ni inferior haya ni maneno yako na kwanza nimesema Waasia wana IQ kubwa klk wote Duniani yaani kushinda Wazungu na wengineo, sasa huwo white supremacy wako unaoungelea unafiti vipi hapo na nilichokiandika?
 
Huyo ni Mchina by Birth maana kaja Tanzania miaka 9 iliyopita
 
nikinukuu gazeti la mwananchi huyo ni raia wa china na amezaliwa china amekuja tz miaka 9 ilopita kila kitu kajifunza hapa sasa lazima tumpe heshima kubwa na pia tujiulize Wapi watoto wetu wamekwamia ni lugha ngumu au???
 
Ndio hivyo, mchina ndo kaongoza, kuna madogo walisema hata mock aliongoza, hapo zimepigwa tu zile siasa za charity begins at home basi. Ambazo kwa kweli hata kwa mtazamo wangu sio mbaya manake hakuna namna sasa.
 

nimesikiliza redio leo japo sijajua alikuja lin tz lakin pind anakuja alikua ajui kiswahili wala kingereza na alianza kufundishwa na mwalimu wake shulen lugha hizo kama masomo ya ziada hivyo utajua alikuja akiwa mkubwa kwan inaonekana
 
Mtoa mada katoa vizuri kabisa, wewe umeharibu kwa sababu unachangia kiitikadi!
 

Wengine hawapendi kutangaza mambo yao yanaishia huko walipo. Lakini wapo naweza thibitisha.
 
Kwa mara ya kwanza YEHODAYA nakupa like kwa kuongea point mkuu na kusimamia ukweli hata kama utakuwa unampinga pro magamba na pro JPM mwenzako.
Hongera,huko ndio ukomavu wa kimawazo na kifikra.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…