Mchezo wa draft

Mchezo wa draft

Drafti ndio mchezo ambao ninaupenda sana.kwanza inatakiwa kuwa makini sana unachotakiwa ni kuangalia pande zote mbili ujue kumkaba mpinzani kiasi kwamba unajua mpaka kete atakayo cheza upungufu wa kete au wingi sio tatizo sana mimi kunawakati napanga 11mpinzani 12 lakini namfunga au droo.
Duh!hizo dharau mkuu
 
Niliwah kwenda znz kuna sehem kuna kijiwe cha draft na bao LA kete pande za kwa mchina barabara ya kwenda kiembe samaki wanapaita sokoni
Wsle jamaa draft lao LA kawaida sana,tatizo ukiwa mgeni alafu unacheza na mwenyeji akikubana kwenye mchezo hatoi maneno ya kashfa,bali anafanya kama vile yupo anakula papuchi kitandani anakata mauno Mdogo Mdogo wew utashangaa watu wanacheka tu ilhali akili yako yote imezama kutafakari utachomoka vipi ktk hilo draft
 
1483640087598.png

Hilo draft ni balaa
 
Inakubidi uwe makini sana,Ukiweza kumpiga mpinzani wako.Tutusa"Mbara mbili.Jua game ni yako.Tutusa"Ni kula kete tatu kwa wakati mmoja.
 
Hakikisha unaweka chambo kizuri kumvutia mpinzani ili aingie kwenye huo mtego wako...hasa hakikisha huo mtego uwe wa kumpiga kete kuanzia tatu...na hakikisha mashambulizi yako yaongozwe na wachezaji kama wa simba ukiweka kama wayanga umekwisha kila siku utapigwa super
 
Hobi Yangu Namba 1 Ni Mchezo Wa Draft, Hata Kula Huwa Sikumbuki Kwenye Draft. uzuri wa draft hata kutazama tu ni burudani tosha, changamoto ni nature ya kazi yangu, kwa sasa ni nadra sana kucheza draft mpaka likizo ivi. miaka ya nyuma nimecheza Vijiwe Kadhaa Dar, Nilichogundua Vijana Wanaocheza Draft Dar Wamegeuza Draft Kama Kitega Uchumi, Wanacheza Kamari Sana! Kazi Yao Ni Kuchukua Copy Kwa Kina Juma Mchafu, Mangwerere na wakongwe wengine ili wapige hela, wengi wanakariri copy, kumbe draft ni hesabu zaidi. Wanasahau Kuwa Draft Ni Burudani Tofauti Na Mchezo Kama Mpira, Kibaya Zaidi Hawafikirii Alternative Ya Maisha, Hiki Ndicho Kilichonisikitisha Zaidi! Napenda Sana Mchezo Wa Draft Kwa Kweli
 
Moja ya mchezo ninao uhusudu ukitoka chess.
Ni simple tu... Draft linachezwa kwa copy na linacopy 12.
Kwa magwiji hawatumii tena copy ni mahesabu makubwa unabidi utumie otherwise utatoa suluhu nyingi na mpinzani wako.
Kwa kuanza download app ya draft kwenye simu yako ya kupyatila pyatila.
 
Draft ni mchezo wa akili tu. Kuna formula (copy)nyingi tu. "Mguu wa jini, kilosa, five ball, kingi fala, na mingine. Mtu akikuwekea copy ya fiveball tayari yeye ana sare wewe utafute. Mguu wa jini ukiuingia hutoki. Kilosa huu mimi ndio naukubali, ni full msuli. Ukiuangalia unaona kila mtu ana nafasi ya kushinda. Ila mara nyingi aliyeanxa kucheza anashinda.

Hawa ndio mabingwa wa Tanzania.

1. Mangwelele. Huyu anapatikana buguruni.
2. Juma mchafu huyu hana kijiwe maalumu. Yeye kacheza draft dsm nzima kila kijiwe.
3. Ronaldo huyu yupo sinza nadhani palestina. Ni sheeder.
4. Godziller huyu maskani yake ifakara. Ila yeye anatembea mikoani. Hii ni kazi yake na inamwingizia kipato.

Note

Ili ijue draft ukubali mambo mawili.
1. Uwe mchafu kwa maana unashinda vijiwe vya draft huna muda wa kufua na kuoga.
2. Ukonde. Maana huna muda wa kula. Muda wooote unagonga kete tu.

Ref. Juma mchafu niliyemtaja hapo juu, jina lake ni juma. mchafu ni nick name yake. Na ni kweli ni mchafu. Hafui wala haogi.
Mangwelele hajui sana siku hizi... Christiano Ronaldo yupo vizuri ila kuna hawa watu wanapatikana mbezi mwisho Mzee salehe (Mangwelele hutafuta sare kwa huyu mzee, ni fundi mno),James Mapigo na Jamaa mmoja anaitwa white.
Na mbeya kuna jamaa anaitwa teacher ndio bingwa wao anapatikana ilomba kwa mwakibete.
 
Ninayo draft moja kwenye PC yangu kuna mdada wa stage ya pili kila siku ananichapa Supa mpaka wife ananiulumia yani natafuta kijiwe nijipige msasa ili nipambane naye tena mpaka avue kyupi
 
Back
Top Bottom