Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Yaani anajikatia tu tiketi, no visa no "nothing"!! Strange bro
Mkuu sikuweza kueleza kila kitu, ukweli ni kwamba huyu mdada alianza muda kusema kuwa nitarudi naye Tz mimi nikawa nadhani anatania. Tukawa tumefika muafaka kwamba mimi nitatangulia ili nimtengenezea mazingira ya yeye kuja Tanzania na pia ningemwalika kama business partiner ili apate visa hata ya miezi miwili kwanza lakini akija Tz atafanya process ya kuomba kuongezewa visa. Tukawa tumeelewana hivyo ndipo akaenda kufanya booking. Ajabu akarudi na akiwa amefanya booking mbili yangu na yake. Nikamuuliza kuhusu visa atafanyaje akasema hakuna shida anaomba kama mtalii na kesho ndo anaenda kwa wakala iliamtumie maombi yake ya visa kwenye ubalozi wa wetu ulioko Japan. Nataka nifanye mchezo kama nitapata mtu pale ubalozini aweke pending application yake.
Ukweli ni kwamba baada matatizo ndio nimegundua kuwa the girl is so smart.
 
Lil Wayne Mkorea siyo mzungu na hata tabia hawafanani. Ni angalizo tu.
 
Kweli kaka damu yangu ni muhimu sana, ila cha muhimu ni kutafuta suluhisho wa tatizo hili lilipo kwanza.
KumkimbiA sio suluhisho, fikiria yafuatayo
1:huyo mkorea kagombana na mama na ndugu kwa ajili yako ukimuacha atakua katika hali gani

2:wewe umebaguliwa je mtoto itakuwaje,atapendwa na mama yake pamoja na ndugu wa mama

3;ikitokea kaolewa tena mtoto ataishi vipi?na ni mweusi?

4:KARMA is a BITCH!kamwe hutofanikiwa kwa masononeko utakayomuachia huyo binti

Ushauri wangu;maliza mtihani then muombe msamaha kwa kumdanganya na umwambie ukweli then mwache aamue kuja na wewe awe bi mdogo au atabaki kwao na hapo ndo utajua cha kumwambia mkeo kwani ushalikoroga hiloo...usitelekeze damu nyeupe hio
 
Mkuu sina mpango wa kumuacha mke wangu natafuta namna ya kumueleza huyo mkorea ili anielewe na tuachane kwa amani.
Haiwezekani muachane kwa amani wakati unamuachia msala mkubwa? Msala wa mimba, kukataliwa na ndugu, kunyanyapaliwa, na pengine akajiua pamoja na kiumbe kilichopo tumboni.

You have to think beyond man, huyu binti amekufadhili sana kipesa, akakupenda mpaka kukataa ushauri wa ndugu pamoja na mama yake halafu leo wataka kutelekeza bila kuhakikisha umemweka sawa Kisaikolojia?
Ndani ya Korea unadhani ataweza kujifungua mtoto mwenye mchanganyiko wa Kimakonde na athaminike?

Hili tatizo ulilitengeneza mwanzo kukosa kumwambia kama umeoa, kitu ambacho kingemfanya ahakikishe anaepuka kubeba mimba. Unasema eti hajawahi kukuuliza kama una mke na familia. Kwa maelezo yako unamzidi umri kwa mbali huyu binti, ulitakiwa uwaze badala yake yale maswali alopaswa kukuuliza kisha uyajibu kwake pasi yeye kukuuliza, kwa ujumla alihitaji Uongozi kutoka kwako.

Kutelekeza binti na mwanao aliyeko tumboni, baadaye wakajapatwa na madhara ni dhambi ambayo inaweza kukutafuna na kukuletea majuto maisha yako yote.
Unawajibika kwa mkeo pia na kwa huyo binti, wote ni familia yako unawajibika kwao.

Haiwezekani mtu aliyekutendea mema ukamlipa ubaya uliopitiliza kiasi hiki, nasema tena, mkeo wa TZ na huyo mkeo wa Korea wote ni familia yako unawajibika kwao

Mwisho nikushauri! Fanya maamuzi ambayo hata yakileta madhara yawe ni kidogo au wastani, yasigharimu maisha ya mtu/watu.

Nachukizwa sana na wanaume wanaowatwisha mabinti/wanawake mimba na kuwatelekeze.
 
Ila inauma eeh!!! Wengi mmemshauri amwambie mkewe ukweli kua anaoa mke mwingine yaani huyu Korea hamjawaza kua hata mke nae ataumia amelea familia toka 2014 akijua mmewe yuko masomoni
Leo fadhila yake kuletewa mke mwingine? Kweli? Wewe kaka bora hiyo ndege utakayopanda ipoteze mawasiliano huko angani familia italia weeee eeee baada ya
muda watazoea kuliko kuwaletea mke mwenza atayeleta ufa ktk hii familia.
 
Toloka wakutumie wale jamaa wa Iris hahaha hv lakini sinasikiaga ngozi hzo wabaridi ilikuwa hadi ukajisahau hvyo hadi ndom hutumii ?anyway umeanzisha vta pgana mpana mwsho
 
Na wanawake wa bongo hakuna asiejua kwmba mume anachepuka ataskitika ila atakubali tu ishu ni kumpanga mkorea nae akubali kuwa bi mdogo
 
Mkuu nilushie contact zake nkusaidie kumpokea akija bongo
 
My God!! Moja, Kwa hivyo amefanya taratibu zote za visa nk kisirisiri, bila wewe kujua? Yaani tuseme barua ya mwaliko amepata wapi? Mwaliko wake unaonesha atafikia wapi? Pili, Tz anakuja kama nani? Maana unaposema anakufuata, anakufuata kama nani? Anakaa mpaka lini? Tiketi amenunua return au one way? Kwa nini? Maana kama analazimisha kuja kama unavyosema, then anakuja kama visitor tu, ambapo lazima awe na tarehe ya kurudi. In fact lazima awe na return ticket. Sidhani kama mtu anaweza kuamka na kuamua kununua tiketi, kisa umemtuma kwenda kununua tiketi yako. Funguka ili watu wakushauri zaidi
 
Mkuu akiwa mbogo ataanza kushtuka na kuwa nae makini zaidi tena ukute ashajua ana mke now anamchora tu
 
Lini jamani watu tutajifunza kuwa sincere kwenye maneno na matendo yetu??? Mnatunga mimba za uongo mnazaa uongo! Ndiyo maana tumezungukwa na jamii iliyojaa uongo tu sababu ya wazazi kuwa ndiyo wapika uongo namba moja! Haya uliyoyafanya yanaakisi mahusiano mengi tuliyonsyo siyo wanaume wala wanawake. It's really sickening! Sasa mtu amwamini mwingine kwa lipi kama tunaweza kutunga uongo mkubwa nakuweka maisha ya wengine hatarini bila hata kujali! Ila kabla hujamwogopa mkeo muogope Mungu ambaye anakujua kuliko hata unavyojijua. Na kumbuka asemaye uongo huyo ni wa ibilisi sababu yeye ndiyo baba wa uongo. Na mwisho kabisa ujue your putting your life at risk more than you could imagine! Huyo dada akijua unamdanganya na hivi uko nchini kwao ujue maisha yako yanaweza kuishia hapo na mkeo na watoto hata usiwaone. Kumbuka mcheza kwao hutunzwa!
 
Mh haya kheri ayafanye wakiwa ana kwa ana. Anaweza kuchukua uamuzi wa kipuuzi siku mbili hizi jamaa hajarudi.
Tatizo ni MKOREA....kamganda jamaa kama LUBA....bila shaka kashamstukia MMATUMBI....
Kwamaana hiyo kufanya ana kwa ana haiwezekani.....kwani MKOREA hata mpa jamaa nafasi kamwe.
 
TUNAZIDI KULIFANYA TAIFA LETU LIZIDI KUWA JUU KWA UONGO....
Binafsi huwa najivunia sana kusema kuwa nimeoa.....na hata wedding ring toka nimeoa sijawahi IVUA....
 
Dah unamtihan mzito lakin nakushaur huna budu kimwambia ukweli mkorea tafuta njia nzur mweleze ukweli kua unamke lakin pia nakishaur kama unajamaa yako yyt huku bongo tafuta nyumba ya kupanga kwa ajili ya mkorea na umtafutie biashara ya kufanya pia isisahau kumwambia ukweli kama unamke
 
Kweli? Wewe kaka bora hiyo ndege utakayopanda ipoteze mawasiliano huko angani familia italia weeee eeee baada ya
muda watazoea kuliko kuwaletea mke mwenza atayeleta ufa ktk hii familia.
......IYO NDEGE ITAKUWA IMEMBEBA PEKE YAKE?
 

duuu hatari sana
option zako kiboko nmekubali.
magufuli ana kazi sana kama upo mtandao wa mafisadi
MBONGO NI MBONGO TU HATA AWE UGHAIBUNI hakosi njia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…