Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Rudi nae Bongo waweke chini wake zako waeleze ukweli. Omba radhi. Hiyo ndo imani ya kikristo kaka. Hata MUNGU atakusamehe. Usiongeze dhambi zaidi kwa kumkimbia mkorea.
 
Nimelipenda hili wazo, nitalizingatia. Ila itabidi niache baadhi ya vitu vyangu ili asishitukie mapema.
Safirisha vitu kabla kwa ndege kabla siku hazijaisha mwambie unatanguliza vitu nyumbani ili mkiondoka msiwe na mizigo ataingia king. Usiache kitu chako ulichoangaikia huku bongo Magu kabana sana
 
Mkuu mwambie mkorea ukweli mwoneshe picha za watoto ..mke na harusi...usikilizie response yake......ukweli utakuweka huru
 
Dah kila nikisoma sielewi nikushauri nini ni kama umeamua kukomesha washauri, kama mwalimu anayetoa swali gumu lisilo na jibu. Tukisema uwambie mke+mchepuko au mmoja wapo bado ni full varangati, tukisema usiwambie wote bado ni full varangati, ushauri pekee ni wewe kuombea hiyo ndege ipotelee angani kama ambavyo huwa tunaombe ardhi ipasuke tunapokutwa na jambo la aibu ya karne.
 
Patamu hapo! Ongea na wazazi wako, uwaambie ukweli, then waambie wafanye mbinu wachukue watoto! Telekeza mke, chukua watoto kwa wazazi wako, then mdanganye Mkorea kuwa hao ni watoto wa KAKA yako marehemu, unawalea. Period

Wanawake wa kibongo hawana dhamana...!
 
Labda Malaya wanaojiuza
Umefika Korea Kusini mkuu? wanawake wa huku wako very charming sana muda wote wanatabasamu. Unaweza kuwa unaongea nao wanakujibu kawaida vizuri tabu huwa ni lugha tu wengi kingereza wanapata shida. Wako free sana binti kukutembelea chumbani si jambo la ajabu. Kama ni mwepesi unaweza ukabaka maana yeye kuja chumbani unaweza kudhani kuwa ameelekea kibra. Wao kwa wao wanaishi maisha ya kujirusha sana, hata mzungu anaweza kuja leo kisha akachukua mrembo hayo nimeyaona. Ngozi nyeusi huku japo hawatuambii waziwazi utajitambua tu kuwa wewe uko daraja lipi. Mara nyingi sana nimewahi kuona mrembo wa kikorea amekumbatiana na mzungu au na mkorea mwenzake huku wakitembea barabarani mchana kweupe, lakini huwezi kuona mweusi anatamba na mkorea ila tunawagonga kwa siri sana. Huyu yeye sana alikuwa amevuka mipaka hawezi kufanya siri. Ni mimi tu huwa namlazimisha iwe siri kwa ajili ya usalama wangu. Anataka twende beach, sehemu mbalimbali.
 
Yaani sasa hivi count kwamba una wake wawili na mtoto mwingine ambaye hajazaliwa!!!

Ninachojua ni kwamba mpaka mwanaume anafikia hatua ya kuomba ushauri ujue tayari ameshafanya maamuzi hivyo anataka kujiridhisha tu.
 
huu uboya kabisa ndio mnafanya tuonekane race ya ovyo....sa ya mimi hayo ya kumdanganya mtu aliyejitoa nakukupenda....bora ungemuambia una familia angejua cha kufanya ...umemdanganya huna mke mwisho ujauzito na mtu ameweka matumaini kwako.....hapo ngumu kumeza...mchukue tu maana huko kwao hujui balaa gani linaeza kukukuta kutoka na mapingamizi ya ndugu zao...af ugenini sio ukiharibu ishu
 
Yaani sasa hivi count kwamba una wake wawili na mtoto mwingine ambaye hajazaliwa!!!

Ninachojua ni kwamba mpaka mwanaume anafikia hatua ya kuomba ushauri ujue tayari ameshafanya maamuzi hivyo anataka kujiridhisha tu.
Kweli mkuu nilikuwa nimefikia maamuzi fulani lakini comment za wadau humu zinanipa mwanga kiasi kwamba ule uamuzi niliokuwa nimepanga awali nimeuona haufai. Bado naendelea kupokea comment maadamu bado nina muda. Muda muafaka ukifika nitafanya maamuzi kwa kuzingatia ushauri nilioupata.
Ukweli ni kwamba sijutii kufungua uzi huu japo wengine wamenikejeli, wengine wameniona mwongo yote nasema ni ya heri, maana kwa kosa hili pamoja na kejeli za wadau nimejifunza jambo kubwa sana.
 
UMELIKOROGA MWENYEWE NA UTALINYWA MWENYEWE
 
Kunamtu kakushauri ujiue wakose wote.mi naunga mkono hoja yake au we unasemaje?
 
Korea ipi Seoul au Pyongyang? Kama ni kwa bwamdogo Kim jisalimishe kwenye vyombo vya usalama mwenyewe kabla hujakabidhiwa kwenye executed machine.
 
Ninachojua ni kwamba mpaka mwanaume anafikia hatua ya kuomba ushauri ujue tayari ameshafanya maamuzi hivyo anataka kujiridhisha tu.
hahahah..kwa muono wako..kashachukua yapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…