Safi sana tena huyo dada hajakomaa vizuri,
utakuta hapo alikua anamwambia mchepuko i love you i'll marry you etc
leo hii anambadilikia na ningekua mie huyo mchepuko namwaribia mpaka kwa mke mtarajiwa,
wanaume jifunzeni kutuliza dushelele zenu,
angekuwepo shemeji hapa angekuumua bonge la kibao.."weh, acha uwongo nimekuta watu walishazindua"...kwikwikwiii!
Kwani responsibility kwa mimba ni kuowa? kuowa ni responsibility kwa "mke", responsibility kwa mimba ni kulea.
mkuu, dini yake hairuhusu kuoa wake wengi na anadai hana mapenzi na mchepuko(alikuwa wa kuzugia)
Abadili dini ili aoe wote..na wa 3 anaweza kuongeza
Hapa ndo huwa nashindwa kuwaelewa wanaume...kumfanya mtu wa kuzugia duh...mchepuko na ukomae kabisa
Yupo..nimuite atoe ushuhuda?
hiyo mimba ametangaza baada ya ndoa kutangazwa?!!...walivyokuwa wanafanya alimwahidi kumwoa au alimwambia ana mchumba wake? Huyo jamaa anaonekana nyenyenye tu,kutishiwa kuuwawa na demu...bwahahahah, mwambie aache ujinga yeye ni mwanaume, aowe anayempenda.
wewe kila anayekufanya anakuowa?!!
kuna wakati mwingine se ni kwa ajili ya starehe tu, watu mmetongozana kustareheshana, hamjaambiana mambo ya kuowana lakini jitu linajirengesha mimba ili mwanaume asiwe na pakutokea, hapo unakuwa unamlaghai na kumchezea mwanaume!
Mpaka mimba bado siyo ukweli? Na nyie muwe siriaz siyo kuchezea watoto wetu. Hapo ni pingamizi tu.
Safi sana tena huyo dada hajakomaa vizuri,
utakuta hapo alikua anamwambia mchepuko i love you i'll marry you etc
leo hii anambadilikia na ningekua mie huyo mchepuko namwaribia mpaka kwa mke mtarajiwa,
wanaume jifunzeni kutuliza dushelele zenu,
Ni shidaaaaaaaaaa. sasa kampatia mchepuko mimba anataka akaolewe na nani?
Mi naona bora aendele na mchepuko akiwa na naafasi ile ile ya mchepuko ili naye apate huduma huku naye wife akichukua nafasi yake makao makuu.
jamaa ana mpenzi wake wa long time kitambo. msichana alikuwa nje ya nchi kimasomo mawasiliano na maelewano kama kawaida(kiufupi wanapenda sana). walipanga mchumba akimaliza wafunge ndoa. mchumba amerudi ndoa tarehe 28/9.
wakati mchumba yupo masomoni jamaa akaona si mbaya kutafuta wa kuzugia(mchepuko). mpaka sasa mchepuko anadai ana mimba ya jamaa na anasisitiza kuwa ndoa haitafungwa na hata ikifungwa hawataishi pamoja atamuua jamaa.
jamaa analia kama dame hajui afanye nini anaona kama mchepuko anaingilia mapenzi yake hivi.
me kama rafiki nimeshindwa kumshauri ila nikaona si mbaya kuwashirikisha wana MMU tumsaidie ushauri kijana wenzetu afanye nini?
jamaa ana mpenzi wake
wa long time kitambo. msichana alikuwa nje ya nchi kimasomo mawasiliano
na maelewano kama kawaida(kiufupi wanapenda sana). walipanga mchumba
akimaliza wafunge ndoa. mchumba amerudi ndoa tarehe 28/9.
wakati mchumba yupo masomoni jamaa akaona si mbaya kutafuta wa
kuzugia(mchepuko). mpaka sasa mchepuko anadai ana mimba ya jamaa na
anasisitiza kuwa ndoa haitafungwa na hata ikifungwa hawataishi pamoja
atamuua jamaa.
jamaa analia kama dame hajui afanye nini anaona kama mchepuko anaingilia
mapenzi yake hivi.
me kama rafiki nimeshindwa kumshauri ila nikaona si mbaya kuwashirikisha
wana MMU tumsaidie ushauri kijana wenzetu afanye nini?
kwanini mkuu? ifike mahali wanawake mjue kutofautisha kati ya mapenzi ya kweli na uongo. msikurupuke
me labda sijui maana ya mchepuko.