Mchemko mwingine wa STRABAG huu hapa

Mchemko mwingine wa STRABAG huu hapa

Kwa dunia ya sasa hatuwezi kukwepa maendeleo kisa ustaarab wa watu. Hata matumizi ya vyoo vya kisasa ilikuwa na changamoto hapo awali. Maendeleo hayawezi kuahirishwa kwa sababu ya wajinga wachache bali hao wachache ndo waaihirishe ujinga wao. Sheria na taratibu zitawanyoosha.
 
Waombe radhi watanzania. Ina maana wao ni washamba wa milango ya vioo?
Hakuna cha kuomba radhi, baadhi yetu waTZ tumekosa ustaarabu au elimu dunia. Hilo la kuiba vioo linawezekana kabisa. Kumbuka hata daraja la mkapa watu waliiba taa hata kabla halijaisha!! Tunatakiwa tubadilike. Kama watu wanaiba mafuta ya transformer na nyaya za umeme watashindwaje kuiba vioo?
 
Nakumbuka walivyong'oa viti na vitu vingine vya thamani walipoingia uwanja mpya wa Taifa kwa mara ya kwanza, koki, vitasa nk; ziling'olewa hasa chooni. Kwa hili ni kweli kabisa
 
Siyo lazima wavivunje hivyo vioo. mbona kuna majumba ya vioo pembezoni mwa barabara Dar na hayajapopolewa mawe.

Inategemea tu uangalizi na utunzaji na ulizi utakuwaje
 
Tusiwe sana negative thinkers sana. Na Mungu akijalia UKAWA ukakamata nchi, basi kutakuwa na nidhamu kubwa na usimamizi mzuri wa mali za uma
 
Tatizo syo strabarg tatizo ni sisi kutokuwa wastarabu wa kutunza mali zetu

.... na issues za law and order. Hii ni ya leo asubuhi. Very sad!
 

Attachments

  • Jangwani.jpg
    Jangwani.jpg
    110.2 KB · Views: 189
Waombe radhi watanzania. Ina maana wao ni washamba wa milango ya vioo?

Mkuu huu ustaarabu wa vioo siyo wetu...! Kama ujuavyo ugomvi wetu ni mawe maana hatuna nguvu za kutupa masumbwi afya mbovu sababu ya lishe mbovu ilipelekewa na umasikini ni shida sana! Lakini ujue vituo ni nyumba za mateja hapo fujo mbelembele....!
 
! Ni kweli ! "huu mradi kuna ubabaishaji mkubwa kwa ujumla!" Barabara gani hizi hazina mitaro / mifereji ya kusafirisha maji taka!

Mkuu hamna mitaro au huioni?! Ipo imefunikwa,sio kama ile mliyoizoea inaachwa wazi na mikubwa kiasi vits ikiingia inazama.
 
Kwa hili pia naweza kusema STRABAG wamechemka sana. Iko hivi kuna hivi vituo vya kisasa katika njia mpya za mabasi yaendayo kasi zinazojengwa na kampuni ya STRABAG baadhi ya hivi vituo vimejengwa na kuwekewa madirisha na milango ya alluminium na VIOO vizuri tu, kuna kituo kipo pala Ubungo urafiri karibu na big brother na kingine kipo maeneo ya Kimara hivi vituo vimewekewa madirisha na milango mizuri ya VIOO.

Sasa tatizo ni kwamba navyowajua wabongo tusivyo wastaarabu walah vile vioo havina maisha marefu vitarushiwa mawe na kuvunjwa vyote ni bora wangeweka nyavu kama walivyoweka katika baadhi ya vituo vyao. Ila tukubaliane hapa lazima mateja watavipopoa vioo vyote.

KWA HILI STRABAG MKAE CHINI NA KUTAFAKARI UPYA.

Kukosa kwenu ustaarabu umlaumu mkandarasi kuweka vioo?!
 
Kwa nini mnamlaumu sana contactor? Hilo ni kosa msanifu,yeye anatekeleza kilichomo kwenye michoro tu.
 
Nakumbuka walivyong'oa viti na vitu vingine vya thamani walipoingia uwanja mpya wa Taifa kwa mara ya kwanza, koki, vitasa nk; ziling'olewa hasa chooni. Kwa hili ni kweli kabisa

Plus mapazia na mishikio ya milango kwenye tren
 
Back
Top Bottom