Mchemko mwingine wa STRABAG huu hapa

Mchemko mwingine wa STRABAG huu hapa

Kwa hili pia naweza kusema STRABAG wamechemka sana. Iko hivi kuna hivi vituo vya kisasa katika njia mpya za mabasi yaendayo kasi zinazojengwa na kampuni ya STRABAG baadhi ya hivi vituo vimejengwa na kuwekewa madirisha na milango ya alluminium na VIOO vizuri tu, kuna kituo kipo pala Ubungo urafiri karibu na big brother na kingine kipo maeneo ya Kimara hivi vituo vimewekewa madirisha na milango mizuri ya VIOO.

Sasa tatizo ni kwamba navyowajua wabongo tusivyo wastaarabu walah vile vioo havina maisha marefu vitarushiwa mawe na kuvunjwa vyote ni bora wangeweka nyavu kama walivyoweka katika baadhi ya vituo vyao. Ila tukubaliane hapa lazima mateja watavipopoa vioo vyote.

KWA HILI STRABAG MKAE CHINI NA KUTAFAKARI UPYA.

Mkuu, vituo vya barabara hiyo vinajengwa na kampuni nyingine (sub-contractor), sio Strabag.
 
Wewe mleta mada strabarg hana tatizo yeye katimiza wajibu wake wakujenga sasa kuhusu kuvamiwa na watu na kufanya makazi hiyo ni issue ingine, manispaa ndy iwatoe hao wavamizi iwaptafutie mahala pengine.
Kuhusu kuweka vioo kuoga kuharibiwa kwanza sisi wa tz lazima tubadilike tuwe wastarabu
 
Back
Top Bottom