Migogoro hii ya biashara baina ya EAC wanachama haitwakwisha leo au kesho, kila mwanachama hataki kufuata sharia na makubaliano yaliyowekwa na EAC, nchi/wananchi wataagiza sukari nje wanasambaza EAC ukiwauliza wanasema hii kitu inazalishwa nchini kwangu, ukimgusa anazuia bidhaa zako pia, kwa hiyo tunajikuta toka EAC ianze matatizo kila siku na hakuna viwanda katika nchi hizi maana bidhaa zinatoka nje zinaua viwanda vyote katika nchi wanachama. Njia pekee ambayo ya kuondoa tatizo hili ni kuangalia maeneo ya ushirikiano ambayo tunaweza shirikiana bila tatizo, mengine yaliyobaki tunaachana nayo, hili swala la biashara ikiwezekana ni eneo gumu kwa kila nchi kukubali, hivyo walitazame upya, ikibidi bidhaa zote bila kujali zinatoka wapi zipigwe tax tu biashara iishe ukiweka ushuru watu watajipanga tu.