Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 18,752
- 21,163
Tuache kuonyesha ujinga wetu katika ngazi ya kimataifa juu ya uwezo wa akili zetu kufikiri, tumepewa msaada na marafiki zetu wa muda mrefu, waliwahi kutupatia, mafuta, mahindi, samaki na vingi tu ndani ya nchi yetu,
Pia izingatiwe wangelikuwa na uovu, basi kwa kuwa chanjo, dawa na vingi tu hupata kutoka western countries, wasingeweza kutukosa katika kufanya ubaya wa aina yoyote waupendao, sisi wa enzi hizo tulikula ugali wa njano ukiwa ni msaada toka kwa marafiki zetu hawa wa damu na hakuna baya lolote lilitupata.
Tupuuze akili zisizo na msingi wowote na ukweli halisi, tunaishi kwa hisia hasi na mawazo hasi,Akili zetu negativity tumeweka kwa 85%.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
#HABARI Shirika la Viwango nchini Tanzania (TBS) limesema kwamba chakula cha msaada kilichoongezwa virutubishi kilichotolewa na Wizara ya Kilimo ya Marekani, kwa ajili ya baadhi ya shule za mkoa wa Dodoma kilifuata taratibu za uingizwaji wa chakula nchini na kilipofika kilifanyiwa ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa matumizi.
Taarifa ya TBS imekuja saa chache tu mara baada ya Waziri wa Kilimo @bashehussein kuitaka taasisi inayofanya mradi wa kutoa misaada ya chakula ikiwemo mchele ulioongezewa virutubisho katika shule mbalimbali mkoani Dodoma, waiambie Marekani kwamba Tanzania kuna mchele na maharage kwahiyo zile fedha wanazowapa wakulima wa Marekani wawape wakulima wa Tanzania na virutubisho viongezwe hapa nchini wakati Watanzania wakiwa wanaona.
Aidha TBS wameongeza kuwa, utaratibu wa kuongeza virutubishi kwenye chakula (food fortification) unakubalika kitaalamu na hufanyika kwa lengo la kuboresha hali ya lishe kwa walaji.
"TBS itaendelea kusimamia kikamilifu jukumu la kuhakikisha kuwa chakula kinachoingia nchini kinakidhi vigezo vya usalama na ubora kwa mujibu wa matakwa ya viwango ili kuendelea kulinda afya za walaji," imeeleza taarifa ya TBS
#EastAfricaRadio