Mchele kutoka nje na hatma ya wakulima wetu

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Mchele kutoka nje.

Je tumejiridhisha kwamba uliopo nchini hautoshi?
Je uzalishaji wetu wa mchele ni kiasi gani, mahitaji kiasi gani na upungufu kiasi gani
Hizo tani elf 90 za mchele zitaingizwa kwa muda gani
Je wakulima walioko shamba kwa sasa mchele wao watauza wapi wakikutana na huo wa nje?

Mchele wa nje inaweza kuwa jambo jema ila nakumbuka wosia wa Mwigulu bungeni hivi majuzi alisema mambo ya dharura ni lazima kuwa nayo makini vinginevyo unaweza kubeba na Deal za watu.
 
Sisi wakulima wa alizeti tulilalamika,pale mafuta yalivyo ingizwa kutoka nje,ikapelekea mafuta tunayo zalisha ndani kuporomoka bei kwa kiwango kikubwa..hakuna aliye tutetea. Kila mmoja ashinde mechi zake nadhani!
 
Mmoja anasema:
Mama hawezi kukubali kuona wakulima wa nchi hii wakiumia tena, na maghala ya serikali yana chakula cha kutosha karibu tani 150 elfu...☺

Mwingine anasema:
Mama ametoa kibali cha kuagiza tani 90 elfu ya chakula kutoka nje, kwasababu hawezi kukubali kuona wananchi wake wanaumia kwa mfumuko wa bei ya chakula...😊
 
Mchele kutoka nje Je tumejiridhisha kwamba uliopo nchini hautoshi?
Je uzalishaji wetu wa mchele ni kiasi gani, mahitaji kiasi gani na upungufu kiasi gani
Hizo tani elf 90 za mchele zitaingizwa kwa muda gani
Je wakulima walioko shamba kwa sasa mchele wao watauza wapi wakikutana na huo wa nje?

Mchele wa nje inaweza kuwa jambo jema ila nakumbuka wosia wa Mwigulu bungeni hivi majuzi alisema mambo ya dharura ni lazima kuwa nayo makini vinginevyo unaweza kubeba na Deal za watu.
Mchele ulipandishwa na shortage. Hii ni simple demand and supply function. Kama tutaingiza mchele kunusuru pia wanamchi kupata utapiamilo kwa kukosa chakula is okay. Tuache mchele wa nje ushindane na wa ndani. Wale wenye hela wale wa ndani ule unaonukia vizuri na wasio na uwezo wale wa nje usio na harufu lakini afordable na pia wanga content ni ile ile. Cha msingi ninkudhibiti usije ukaingizwa na mchele feki. Asikwambie mtu,mchele bei imepanda kupundukia ni kama wanapandishia sifa.
 
Mchele kutoka nje Je tumejiridhisha kwamba uliopo nchini hautoshi?
Je uzalishaji wetu wa mchele ni kiasi gani, mahitaji kiasi gani na upungufu kiasi gani
Hizo tani elf 90 za mchele zitaingizwa kwa muda gani
Je wakulima walioko shamba kwa sasa mchele wao watauza wapi wakikutana na huo wa nje?

Mchele wa nje inaweza kuwa jambo jema ila nakumbuka wosia wa Mwigulu bungeni hivi majuzi alisema mambo ya dharura ni lazima kuwa nayo makini vinginevyo unaweza kubeba na Deal za watu.
Mtajua wenyewe. Nyinyi mnaona sawa kutuuzia kilo ya mchele kwa shilingi 3600! Si mlifurahia soko kufunguliwa, na hivyo kuuza chakula chenu nje ya nchi kwa bei mnayotaka!!

Sasa inakuwaje mnaanza tena kupagawa mchele kuingizwa nchini? Si ndiyo soko huria lenyewe hili!!! Nyinyi nendeni mkauze mchele wenu nje ya nchi kwa bei kubwa, na sisi tutanunua huo mchele wa kutoka nje kwa bei nafuu.

Ni wakati sasa wa kila mtu kushinda mechi zake. Msianze kulia lia hapa.
 
Ni bore uje nje Ili kuwe na equilibrium katika bei manake Sasa ni kama watu wanafanya kusudi
"Msije kutuletea tena ule wa Thailand Nusu kilo manakula watu 18 na unabaki kiporo cha chai"🙌.......pitia Account za Instagram na Facebook za ITV zilizopost hii taarifa usome maoni utajifunza vitu vingi sana. hiyo ni moja ya comment
 
Mchele wa plastic huo.

Kansa kwa sana. Nunua mchele wetu wa kuzalisha wenyewe.
 
Mtajua wenyewe. Nyinyi mnaona sawa kutuuzia kilo ya mchele kwa shilingi 3600! Si mlifurahia soko kufunguliwa, na hivyo kuuza chakula chenu nje ya nchi kwa bei mnayotaka!!

Sasa inakuwaje mnaanza tena kupagawa mchele kuingizwa nchini? Si ndiyo soko huria lenyewe hili!!! Nyinyi nendeni mkauze mchele wenu nje ya nchi kwa bei kubwa, na sisi tutanunua huo mchele wq kutoka nje kwa bei nafuu.

Ni wakati sasa wa kila mtu kushinda mechi zake. Msianze kulia lia hapa.
Kwa hiyo kwako bora tuanze kula makapi ya bei rahisi, umenikumbusha wale sangara na sato wa ziwa Victoria waliokuwa wakipandishwa ndege kwenda ulaya, huku wabongo tunakula mapanki, hakika tumeshazoeshwa kula mitumba, afya kwetu sio issue tena, muhimu tumbo lijae!.
 
Tatizo lilianza pale bei ya mchele ilipopanda, solution ikawa kuruhusu mchele wa nje kuingia. Kwa hiyo wanaoumia ni wakulima kwa sababu mchele utakapoingia utashusha bei ya mchele masokoni
Nini maana ya soko huria? Kama wakulima wanafurahia kuuza mazao kokote wapendako, wafurahie pia kupata ushindani kutoka kwa wazalishaji wenzao kutoka nje.

Sisi ambao siyo wakulima, hatuwezi kufurahia kuuziwa kilo ya mchele kwa 3600! Kilo ya maharage 4000! Huku kipato chetu kikiwa hakijabadilika. Ni bora soko liwe huru ili tupate unafuu.
 
Kwa hiyo kwako bora tuanze kula makapi ya bei rahisi, umenikumbusha wale sangara na sato wa ziwa Victoria waliokuwa wakipandishwa ndege kwenda ulaya, huku wabongo tunakula mapanki, hakika tumeshazoeshwa kula mitumba, afya kwetu sio issue tena, muhimu tumbo lijae!.
Una uhakika gani kama huo mchele unaoletwa ni makapi? Nyinyi mchele mnao wauzia Wakenya na Wasomali ni makapi?

Wewe kijana wa Moo mbona unaleta story za kufikirika! Unataka kusema hakuna mamlaka ya chakula na dawa nchini kwa ajili ya kuchunguza ubora wa huo mchele!
 
Back
Top Bottom