TANZIA Mchekeshaji Jumanne Alela maarufu kama "Mzee Matata" wa Mizengwe afariki dunia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,741
218,330
Taarifa zinaeleza kwamba amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Muhimbili alikolazwa tangu tarehe 13 June

========

WhatsApp-Image-2021-06-16-at-8.20.37-AM.jpeg

MWIGIZAJI wa Kikundi cha Maigizo cha Kashkashi kinachorusha mchezo wao wa kuchekesha wa Mizengwe kupitia Televisheni ya ITV, Jumanne Alela almaarufu Mzee Matata amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 16, 2021 Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar alipokuwa amelazwa kwa matibabu toka Juni 13, 2021..

Kwa mujibu wa mwigizaji maarufu nchini, @madebelidai, mazishi ya Mzee Matata yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Buguruni,Malapa jijini Dar.

“Mwanatasnia mwenzetu Mzee Jumanne Alela (Mzee Matata) yatafanyika kesho saa saba mchana kwenye Makaburi ya Buguruni-Malapa.

“Msiba upo kwa ndugu zake, Chamazi kwa Mkongo (jijini Dar),” taarifa kutoka kwa @madebelidai.

Chanzo: Global Publishers
 
poleni sana wana kashkash group kwa msiba mkubwa wa kupoteza mwenzenu lkn pia kwa washabiki wake wote nikiwemo mimi.
huwa sikosi kipindi cha kashkash kila siku ya J.pili saa mbili na nusu ITV.

Mzee Matata amefanya kazi kubwa sana ya kuelimisha jamii kupitia maigizo yao.

Apumzike kwa amani.
 
poleni sana wana kashkash group kwa msiba mkubwa wa kumpoteza mwenzenu lkn pia kwa washabiki wake wote nikiwemo mimi.
huwa sikosi kipindi cha kashkash kila siku ya J.pili saa mbili na nusu ITV
Mzee Matata amefanya kazi kubwa sana ya kuelimisha na kuifundisha jamii kupitia maigizo hayo ya kashkash/mizengwe.
Apumzike kwa amani.
 
Taarifa zinaeleza kwamba amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Muhimbili alikolazwa tangu tarehe 13 June

========

MWIGIZAJI wa Kikundi cha Maigizo cha Kashkashi kinachorusha mchezo wao wa kuchekesha wa Mizengwe kupitia Televisheni ya ITV, Jumanne Alela almaarufu Mzee Matata amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 16, 2021 Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar alipokuwa amelazwa kwa matibabu toka Juni 13, 2021..

Kwa mujibu wa mwigizaji maarufu nchini, @madebelidai, mazishi ya Mzee Matata yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Buguruni,Malapa jijini Dar.

“Mwanatasnia mwenzetu Mzee Jumanne Alela (Mzee Matata) yatafanyika kesho saa saba mchana kwenye Makaburi ya Buguruni-Malapa.

“Msiba upo kwa ndugu zake, Chamazi kwa Mkongo (jijini Dar),” taarifa kutoka kwa @madebelidai.

Apumzike kwa amani mzee huyu.

Ila chelewa chelewa hii ikiyahusu pia yale mambo yetu ya chanjo, tutakuja kuta wana si wetu.
 
Back
Top Bottom