SoC02 Mchawi wa vipaji vya mtu mweusi

Stories of Change - 2022 Competition

Mr Kachila

Member
Jul 31, 2022
5
1
MCHAWI WA VIPAJI VYA MTU MWEUSI

Kipaji
, ni uwezo wa asili wa kutenda mambo makubwa na yenye matokeo bora, kwa kutumia nguvu na rasilimali ndogo ukilinganisha na watu wengine. (tafsiri kwa mujibu wa kitabu cha KIPAJI na Emilian busara na mrembo Grace, 2015 ). Kwa ujumla kipaji huambatanisha uwezo wa kuzaliwa nao wakufanya kazi fulani lakini kinaweza kikaendelezwa au kutoendelezwa. Kipaji hakirithishwi wala huwezi kujifunza sehemu yoyote.

Asili ya ndani ya kipaji ni kuonyesha ujuzi na mafanikio, ambayo huwakilisha maarifa au uwezo unaopatikana kupitia kujifunza, mfano wa vipaji ni kuchenza mpira, riadha, masumbwi, riadha, kuimba, kuchora na vingine vingi.Asili ya kipaji, kipaji cha mtu hutokana na kuzaliwa nacho na hawezi kukirithisha kwa mtu, kila mtu ana kipaji cha aina yake. Mtu anaweza kuwa na kipaji na asikijue? Ni kweli wapo watu wengi wanaishi na kipaji bila ufahamu wa vipaji vyao au wapowanao ufahamu lakini hawavitumii. Watu weusi pamoja na kujaliwa zawadi adimu ya vipawa kutoka kwa mwenyezi Mungu lakini hadi wa leo ni wachache kati yao wamekuwa wanufaika wa vipaji hivo. Hii kwa sababu hawanufaiki na vipawa kisa tu hawana mazingira ya kuwawezesha kufanikisha vipawa hivo na kuviibua. Zifuatazo ni moja ya hoja zinazo pelekea vipaji vya mtu mweusi kutotambulika katika uliwengu tulionao wa vipaji;

Utumwa wa kielimu, katika bara la afrika watu (wazazi au walenzi) ambao huenda wangetambua na kuviibua vipawa vya mtu mweusi angali mtoto, wamekuwa wakijikita Zaidi katika kuhakikisha mtoto anapata elimu hata kama ataonesha kipi mtoto alicho nacho toka tumboni mwa mama yake. Hali hii ya kuthamini elimu bila kujali kipajicha mhusika imekuwa ni chanzo za ufifiaji hata upoteaji wa kipaji kwa wakati mwingine.

Utumwa wa kazi, jamii nyingi za afrika zimekuwa zikibangua kazi zinazotokana na vipaji, na kuamini kazi zitokanazo na kusoma ndo bora Zaidi, mfano kazi ya udaktari, ualimu, uanajeshi zimekuwa na nguvu katika jamii za mtu mweusi na kupelekea wazazi na walenzi wa mtoto mweusi kupiga vikali vipaji vitokanavo na michezo kama vile mpira, mieleka, uigizaji, uchekeshaji na kadhalika.

Ukosefu wa hamasa kutoka kwa watu ambao tayari wamefanikiwa kupitia vipawa vyao, katika hali ya kawaida kila kitu kukua na kuonekana hususani vipawa kwa dunia ya leo lazima kuwepo na hamasa kotoka kwa wafanikiwa. Ukosefu wa hamasa kwa vijana wa mtu mweusi kumesababisha ufifiaji wa vipaja kwa mfano, katika sekta ya michezo ya mpira kama mpira wa miguu, kikapu tunaona watu weusi waliofanikiwa wapo ughaibuni wanasahau kutoa hamasa ya maendeleo yao kimaisha badala yake wanaposti picha wakiwa vilabuni na vidungu vyao kichwa, wakati huo tunaona mtu mweupe anaposti mali anazo miliki kupitia kipawa chake.

Uwekezaji mbovu, katika uwekezaji wa kuibua vipaji vya mtu mweusi unaonekana kutokuwa shupavu ambapo ukija katika sekta ya elimu utaona ni shule chache katika nchi zinakwepo na kipaji, hata miundo mbinu kwa ajili ya kuibua vipaji ni mibovu. Miundo mbinu hiyoni kama viwanja vya michenzo, maktaba na maabara za kisasa hazipo.

Ungumu wa maisha, moja ya sababu ya ungumu wa maisha unachangia katika kiwango kikubwa ambapo kijana mweusi anashidwa kujiendeleza kipawa chake, mfano kijana anaweza akawa na kipaji cha uinjinia lakini akakosa vifaa muhimu kwa ajili ya kukiendeleza kipaji chake kutokana na hali ya ungumu wa maisha. Nini kifanyike ili kunasua vipaji wa kijana mweusi? Kuna haja kubwa sana katika kuvitambua na kuviibua vipaji hivi vya ngozi nyeusi kwa ajili ya manufaa ya kitaifa kwa ujumla. Zifuatazo ni hoja pendekezi kwa ajili ya kuvitambua, kuviibua na kuviendeleza vipaji vya mtu mweusi;

Usimamizi kutoka serikalini, serikali husika inapaswa kushughulika na vipawa vya vijana wake, katika kusimamia na kutengeneza mazingira rafiki kwa vipaji vyao. Sambamba na kuwezesha mtaala wa elimu kuwapa fursa vijana wake, pia serikali itafute namna ya kuwa hamasisha kama vile utoaji wa zawadi na kuwa somesha vijana wenye vipaji.

Uhamasishaji kutoka kwa wafanikiwa wa vipaji, watu ambao tayari wananufaika na matunda ya vipawa vyao wanatakiwa kutoa hamasa kwa vijana wenye vipaji mfano, msanii kama Diamond platinum, Alikiba na Harmonize kwa upande wa miziki, pia Bwana samatta kwa upande wa mpira wa mguu hawa watu wanatakiwa kuwa chachu ya kuibua vipaji vya vijana weusi.

Kuboresha miundo mbinu saidizi kwa kuibua vipawa, hapa wadau mbalimbali na serikli wanatakiwa kuhakikisha miundo mbinu na vitu vingine kwa kuibua na kuendeleza vipawa vya vijana vinajengwa na kuwepo katika ubora wa hali ya kisasa, ili kuhakikisha vipawa havipotei na badala yake vinatambulika na kuishi katika uhalisia wa maisha ya vipawa. Nini kinatakiwa kufanyika kuvipeleka mbele vipawa vya mtu mweusi ni vingi huenda visihesabike.

Kwa kuhitimisha, kipaja ni ufunguo wa maisha ya mafanikio, pamoja ya kwamba kila mtu ana kipaji lakini si wengi wanahusianisha vipaji vyao na mafanikio yao kimaisha. Waliofanikiwa Zaidi katika maeneo mbalimbali kwa sehemu kubwa wamefanikishwa na vipaji vyao. ndio maana tunaona wanamichezo mbalimbali katika mpira wa miguu, kikapu, masumbwi, riadha na kadhalika, wamefanikiwa Zaidi kwa sababu ya vipaji vyao na si elimu zao.
 
H

Hakika, mkuu. Hatujanufaika ipasavyo kutokana na vipaji vyetu
 
Back
Top Bottom