Wazazi mnapaswa kutambua vipaji vya wanenu

de Gunner

JF-Expert Member
Nov 2, 2021
917
1,885
Katika dunia tuishiyo leo, ni bora kuwa vizuri katika jambo fulani(kuwa expert) kuliko kuwa na ma vyeti mengi lkn uko shallow! Yaani unatakiwa kuwa mjuzi katika filed husika.

Mfumo wa elimu hauna specifications kwamba wewe una kipaji gani bali ni one fits all. Hivyo basi wazazi wanapaswa kutambua vipaji na uwezo wa watoto wao na kuwa support katika ku fulfill destiny zao.

Wazazi wengi ambao wapo humu atleast wanauelewa na kile nacho ,maanisha, unakuta mzazi kasoma kabisa na anajua kuna deficiency ya ajira lakini bado ana cling na vitu vya kipiuuzi no disrespect ila mnakosea sana. Waacheni watoto wafwate kile wanapenda na pia muwa support. Kama mwanao anapenda arts kwann umforce akasome sayansi? Kisa mtoto wa jirani kachaguliwa shule za special? Acheni kufwata mikumbo.

Mwishoni mtoto kamaliza chuo, anakuja home ajira hakuna mnaaza kumzonga na kumwona mzigo. Anzeni harakati za kumjengea mazingira akiwa bado mdogo kwa kumdirect kwenye vile vitu yupo gifted. Anapo fikia level za elimu ya juu anakua tyr yupo kwenye njia sahihi, vijana wengi wameshindwa kujiajiri simply becoz wanavyeti bandia, yaani wamesomea vitu hawana interest navyo. So anasubiri aajiriwe tu, huko ndo atapata experience.

Hivyo basi wazazi kuweni bega kwa bega na watoto wenu hasa katika kuwasaidia kufanikisha ndoto zao. Mambo ya kuachia shule na walimu wafanye hiyo kazi, they know nothing about your children and their future. Ni hayo tu, nakaribisha maoni na nyongeza!
 
Ni umasikini ndo unatufanya tusizingatie hizo talents za watoto!

Extra curriculae kwenye shule za ada ndefu ndo zimewatoa watu kama kina PFunk, mtoto wa Rchuga kaenda UN kama sehemu ya extra c, tukamuona ni intellectual!

At the age of 4 mtoto alishakabidhiwa kwa waalimu, mzazi anaonana na mtoto kwa kuvizia! Mzazi akikumbuka, atamwambia dada awaandae watoto, anawapeleka beach, jumping castles etc!
- Saa ngapi ataona hivyo vipaji?
-Nani analipa 40m kwa mwaka kama ada huku uswahilini kwetu? Kila kukicha tunakutana na school bus mbovu road, ndo watakuwa na extra c?
  • Umitashumta ulishafutwa
  • Makongo is no longer makongo ile

Mfumo wa nchi unataka vipaji vizingatiwe baada ya mtu kufeli academically!
 
Walimu unaosema "know nothing"ndio wamekuwa mstari wa mbele kung'amua vipawa vya watoto na kuwasaidia kuwajenga na huko nyumbani ndio mnakuja kujua baadae na kusema ana kipaji flani
Tena walimu wangekuwa wanasikilizwa na wazazi watoto wangefika mbali tena vizuri
We mtoto anapata four ya 31 form two mzazi anaenda kumtafutia tuition ya math na physics
Ukimwambia mwanao ni best runner tumjenge mzazi atakwambia unamuharibu then you say we know nothing
 
Watoto wanakua na influence mbalimbali kadri ya ukuaji wao. Mtoto akiwa nursery mpaka darasa la saba wengi huwa wanataka kuwa marubani au walimu au polisi au daktari hii ni kutokana na influence ya walimu wao na jamii iliyowazunguka. Kadri anavyokua na kupata ilimu basi mawazo hubadilika kutokana na uhalisia.
Watoto wengi wafikapo level ya kuchagua tahasusi uhangalia nini kinavuma kipindi hiko. Lakini wazazi kama walezi na watu wamepitia mengi wana nafasi kumshauri mtoto kufuata mkondo fulani. Si mbaya kumtakia mwanao mema.

Mimi nasema wanangu kama atakua mhandisi asome civil au mechanical. Kama atakua art atasoma communication kama atakua sayansi asome udaktari. After that atajiamulia.
 
Hoja yako inamsingi lakini ime base kwenye fact za utajiri. Sidhani kama utajiri ni factor kubwa!

Sio mpk mzazi aweze kuafford hizo expensive schools, ingawali zina play pakubwa sana. Ila mimi nahisi ni ignorance tu ambayo wazazi wanayo! Unakuta mtoto ameonesha dalili kabisa kuwa yupo creative kwenye aspect fulani. Lakini mzazi anaforce tu aendelee kusoma kada ambayo yeye ana hisi ipo sokoni au ina mshahara mnono. Bila kuangalia in m affect kivipi mtoto.

Swala la kina P funk, na wengineo kama kina jux, hizo ni wealthy family na wazazi wapo open minded. Ila sio factor kuna wazazi nawaona mtaani wapo rich, but closed minded. Sidhani mpk uwe na maisha mazuri sana et ndo mtoto afwate kile anapenda. Na hilo sio swala la kutegemea eti serekali ndo ifanye marekebisho, kada za kusomea zipo nyingi, vyuo vipo vingi. Wazazi waangalie mtoto anapenda nini wam support kwa kidogo walicho nacho, hii pia ina ambatana na kumwacha achague kile anapenda kusomea.

Umitashumita na makongo zimebase sana kwenye michezo, na michezo sema kweli tupo nyuma. Nyie wenyewe mashahidi bado hata ligi zetu za ndani zipo nyuma, investments zimeanza kufanyika hasa kwenye mpira ila itachuka miaka mingi. Hata kama zingeendelezwa bado kungekua na uwezekano mdogo wa hao watoto kufikia ndoto zao. Wenzetu wazungu wapo vizuri kwenye hili ndo maana mtoto anaanza accademy akiwa mtoto kabisa. So hapo ni tatizo la nchi zinazoendelea....
 
Walimu unaosema "know nothing"ndio wamekuwa mstari wa mbele kung'amua vipawa vya watoto na kuwasaidia kuwajenga na huko nyumbani ndio mnakuja kujua baadae na kusema ana kipaji flani
Tena walimu wangekuwa wanasikilizwa na wazazi watoto wangefika mbali tena vizuri
We mtoto anapata four ya 31 form two mzazi anaenda kumtafutia tuition ya math na physics
Ukimwambia mwanao ni best runner tumjenge mzazi atakwambia unamuharibu then you say we know nothing
Kiuhalisia kama wewe ni mwalimu, basi lazima ungesema haya.

Acha kupotosha watu, imagine upo darasani na watoto 50, utajuaje personality ya kila mtoto? Pia wewe utamjua zaid mtoto kwenye angle ya performance aoneshayo kwenye somo lako, so acha kudhani unamjua mtoto. Huishi na mtoto bali unamfundisha mtoto kwa masaa au dakika kadhaa kwa siku, so humjui mtoto.
 
Watoto wanakua na influence mbalimbali kadri ya ukuaji wao. Mtoto akiwa nursery mpaka darasa la saba wengi huwa wanataka kuwa marubani au walimu au polisi au daktari hii ni kutokana na influence ya walimu wao na jamii iliyowazunguka. Kadri anavyokua na kupata ilimu basi mawazo hubadilika kutokana na uhalisia.
Watoto wengi wafikapo level ya kuchagua tahasusi uhangalia nini kinavuma kipindi hiko. Lakini wazazi kama walezi na watu wamepitia mengi wana nafasi kumshauri mtoto kufuata mkondo fulani. Si mbaya kumtakia mwanao mema.

Mimi nasema wanangu kama atakua mhandisi asome civil au mechanical. Kama atakua art atasoma communication kama atakua sayansi asome udaktari. After that atajiamulia.
Umeongea point mkuu, influence za nje pia zinamchanganya mtoto, na mzazi kwasababu ameish naye yy ndo anamjua mwanae vizuri hivyo inapaswa kumshauri kulingana na vile mtoto wake hupendelea. Ila mm nadhan wazazi wengi huichkulia hii dhana bila kumjali mtoto kama wewe.
 
Back
Top Bottom